Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

1472795936915.jpg
Kuna aina nyingi ya kulipa kisasi hata kuvizia ama kutumia watu wa kulipwa wakaangamize mbaya wako ni njia mojawapo
 
kaka mshana jr mi kuna mjuaji mmoja, tena gabachori, kaniingiza King, yaani mtoto wa mjini nimetendwa na wakuja, kumsamehe nimeshindwa na nguvu ya kulipiza kisasi sina, ktk hali kama hiyo nafanyaje?
 
kaka mshana jr mi kuna mjuaji mmoja, tena gabachori, kaniingiza King, yaani mtoto wa mjini nimetendwa na wakuja, kumsamehe nimeshindwa na nguvu ya kulipiza kisasi sina, ktk hali kama hiyo nafanyaje?
Hapana inabidi kuchagua moja ili upate nafuu ya roho lakini pia unaweza kumuandikia barua ya kumkumbusha kitu alichokufanyia na kunjulisha kwamba hujamsamehe na utadai pesa yako hata maiti yake
Barua hiyo imfikie yeye na ndugu zake
 
Mie kuna mtu nashindwa kumsamehe na nashindwa kusahau nikifika kwenye kulipa kisasi dini inakataza nimebaki njiapanda.Hili jambo ni kweli na usiombe likakukuta.
unaposamehe inabidi usahau vinginevyo unakua hujasamehe. Kinachofanya tushindwe kusahau ni pale mtu anapokukosea mwingine atakuomba msamaha lakini baada ya muda anarudia lilelile halafu anakuomba tena msamaha. Hapo kisamehe mtihani
 
Msamaha unaanzia nafsini. Kitu kinachochanganya watu Ni kusamehe na nafasi. Mtu anataka ukimsamehe uendelee kumchukulia alivokuwa mwanzo. Hapana ndo maana hata maneno matakatifu yanasema pendani yakimaanisha Ni lazima umepende binadam mwenzio na ukimpenda utamsamehe. Na wanaposema wapendeni adui zenu inahusika na adui yako Ni yule aliekuumiza aliekufanyia uhaini nakadhalika. Mpende msamehe usimtendee baya mlipe wema. Ila yote fanya si lazma unaemsamehe umrudishe kuwa vile. Msamehe maisha ya aman yaendeleee. Kuna mwalimu anasema unapoambiwa Mpende adui yako wanamaanisha tunza utu wake mthamini muheshim kumbuka tu yule Ni adui yako si rafk ako
 
Kama tungekuwa tukiishi kwa visasi basi ingekuwa dunia ya vita
 
Kama tungekuwa tukiishi kwa visasi basi ingekuwa dunia ya vita
Visasi vipo sana kinachotunusuru ni unafique wa kujifanya tumesamehe kumbe tunalo rohoni ndio maana wengi wanakufa wamepinda utafikiri wa ugonjwa wa ngiri
 
Niliapa lazima nilipe kisas lakin sasa nmemsamehe ... Lusy elly nmekusamehe ingawa ilikua ngumu sana ...
 
Huu uzi umenigusa sana, kuna muhuni kanifanyia umafya wa ajabu sana (dhuluma) kumsamehe nimeshindwa kbs namvutia kasi, ni lazima nimuwajibishe ili nafsi yangu ipate amani!
 
Back
Top Bottom