Ukiolewa Kanda ya ziwa sahau kurudi kwenu

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,540
Kwa wasio wenyeji wa kanda ya ziwa.

Nimeona malalamiko mengi sana kina mama na kina dada wasio wenyeji wa mkoa wa Mara (na kanda ya ziwa ) wakilalamika sana kuhusu swala la kusahau kwao.

Inasemekana kuna UCHAWI mzito sana wanafanyiwa ili kusahau nyumbani kabisa.

Basi nawasogezeeni hili mlichukhlie kwa upana wake;

Mkiona ndugu yenu kaolewa KANDA YA ZIWA huku hasa maeneo ambayo hayaendelea, mjue kuna mizizi mikali sana inatumika kuwazima wasirudi ama wasikumbuke makwao tena

Screenshot_20230513-034227.png
Screenshot_20230513-034153.png
 
labda hao ula uoe mzigua asiende kwao thubutu😅😅😅 Hao kwa mwaka mara chache sana kaenda kwao mara 3 ndani ya mwaka..

Daily wapo Handeni ukioa hao wazigua wanapenda kwao kinoma.
 
Kwani ukiolewa unaenda kujenga ukoo wenu tena au wa kwako na mumeo?! Kaa kwako acha tabia za kurudi rudi kwenu.. Ila kama kuna mambo ya kishirki yanahusika kwenye hilo swala la kumsahaulisha mtu kwao sio vizuri hata kidogo..
 
Kwa wasio wenyeji wa kanda ya ziwa.

Nimeona malalamiko mengi sana kina mama na kina dada wasio wenyeji wa mkoa wa Mara (na kanda ya ziwa ) wakilalamika sana kuhusu swala la kusahau kwao.

Inasemekana kuna UCHAWI mzito sana wanafanyiwa ili kusahau nyumbani kabisa.

Basi nawasogezeeni hili mlichukhlie kwa upana wake;

Mkiona ndugu yenu kaolewa KANDA YA ZIWA huku hasa maeneo ambayo hayaendelea, mjue kuna mizizi mikali sana inatumika kuwazima wasirudi ama wasikumbuke makwao tena

View attachment 2619742View attachment 2619743
Sasa kama umeoa Mzaramo kila mwezi kuna kigodoro mara shughuli, sijui Ngoma na kila akienda anakaa huko wiki 3, utaweza?!

Itakuwa wanapigwa pini na kunyimwa ruhusa tu, siyo uchawi
 
Ndio maisha yalivyo, pia kuna wanaume wa kanda ya ziwa walipoyapata ya ki Tanga wakakwama kabisa hawajarudi kwao, mpaka walipofatwa na ndugu zao. Ni mapenzi tu, utamu, shida za maisha na raha zake 😆

We unadhani hawa wahindi waliokita kabisa Afrika kabla ya ukoloni na vizazi vyao baadae walipigwa pini?😆Walipuuza kwao?
 
Nimeona malalamiko mengi sana kina mama na kina dada wasio wenyeji wa mkoa wa Mara (na kanda ya ziwa ) wakilalamika sana kuhusu swala la kusahau kwao.

Inasemekana kuna UCHAWI mzito sana wanafanyiwa ili kusahau nyumbani kabisa.
Kwani Waafrika wanaolowea Ulaya na Marekani miaka na miaka bila kurudi kwao wamefanyiwa uchawi?
Ni mapenzi ya mtu tuu
 
Naona dalili za kudai urithi watoto wakike zinaanza hivi hivi.
Bora wameongeza somo la dini kwenye elimu mtambue wanawake ni mali ya mwanaume ukishaolewa kwenu sio tena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom