Tazama Kanda ya Ziwa ilivyobarikiwa na Mungu

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
479
665
JF Salaam!!

Ninaposema Kanda ya ziwa bila shaka tiyari unakuwa umepata taswira yake.

Siyo kwamba mikoa mingine haijabarikiwa la hasha lakni Kwa Kanda ya ziwa Kuna neema ya pekee sana.

Hapa nitataja baadhi ya vitu vinavyopatikana Kwa wingi Kanda ya ziwa.

Kwa akiri yangu japo Sina takwimu sahihi nakiri ya kuwa zaidi ya 73% ya Nchi kavu Kanda ziwa Ina madini ya dhahabu hapa nitataja sehemu chache tu ninazo zifahamu na nimewahi fika.

Shinyanga karibia 67% ya mkoa wa shinyanga Ina madini ya dhahabu na Alimasi. Mfano wa sehemu hizo ni kahama. Wilaya hii huenda ikawa wilaya ya kwanza Kwa Tanzania yenye uchumi unao kua Kwa Kasi sana.

Yote hayo sababu kuu ni dhahabu. Tukiamza na mgodi wenyewe wa buzwagi (Kwa Sasa umesimama uzalishaji). Kuna mgodi mwingine wa Bulyanhulu upo kakola.

Kuna mgodi mingine ambayo ni ya wachimbaji wadogo wadogo. Nayo haijapoa Kwa mrefu Sasa mfano

Nyakagwe,nyangalata,nyamishega,Karole,nyamikonze, nk hii ni migodi iliyo karibu tu na kakola **** mwime karibu na mji wa kahama na mengine mingi. (Mtaongezea)

Hapo juu nimetaja mingine ya mkoa wa geita tukianza na geita yenyewe Ina migodi kibao mkubwa ukiwa ule GGM.

Bado pale mgusu, lwamgasa hapa Kuna wachimbaji wadogo na Kuna mgodi mkubwa una mwekezaji company kama sio Buclif (Sina uhakika na jina) pale bukoli Kuna mgodi mdogo na nayrugusu vilevile ukija busolwa Kuna dhahabu ya kuona pale. Hizo ni sehemu baadhi tu nilizowahi fika mwenyewe

Huko mara napo Kuna mgodi wa North mara Kuna dhahabu ya kuona pale waliowahi fanya kazi pale basi watakubaliana namimi.

Kwakweli Kwa upande wa madini hasa dhahabu Kanda ya ziwa umeshehen na huenda takwimu zangu zikawa sio sahihi yaani ziko chini.

Nimewahi kuwa Geology Assistant Moja ya mgodi flani mkubwa niliogopa kuona sehemu karibia yote ya maeneo ya kahama Kuna dhahabu ni baada ya kukaa na senior wangu karibu akanionyesha ramani ambayo wamewahi fanya research company iliwatuma na wakagundua kuna dhahabu.

Maeneo hayo ni kama jomu, mwakitolyo. Burige, Igalula, Kitongo, Mwingiro, Segese na mengine nimeya sahau.

Maeneo mengine ambayo yansemekana Yana dhahabu Kwa wingi ni Serengeti,mlima wa fedha, hiyo milima ya geita Ina dhahabu ya kutosha nk

Itoshe kusema Kwa upande wa dhahabu Kanda ya ziwa Haina mpinzani.

Tukija kwenye kilimo na ufugaji
Kanda ya ziwa ipo vizuri na hii imepelekea Hadi kufanya uharibifu wa kuahribu mazingira Kwa kukata miti Kwa ajiri ya kilimo na ufugaji.

Kanda ya ziwa Ina mbuga Kwa ajiri ya kilimo Cha mpunga na dengu na hii imekuwa ikifanya vizuri miongo na miongo.

Kwa upande wa mahindi,pamba na mazao mengine Kanda ya ziwa Iko vizuri pia ila changamoto inayowakabili Kwa Sasa ni rutuba mashamba Kwa Sasa hayana rutuba.

Tukija upande wa ziwa hapa Sasa hata sita elezea wakuu Kila mtu anajua wazi kwamba samaki ni dhahabu ya majini ambapo kg1 ya sato Kwa mwanza na mganza huuzwa 7200-800+ inategemea na msimu(upatikanaji wake)

Bado Kuna dagaa na samaki wengine ambapo huku Kanda ya ziwa wenyeji Wala hawajui kuwa samaki anauzwa Kwa Kila wao wanajua anauzwa Kwa mafungu au Kwa vipande hasa wale sangara wakubwa (mbuta) hukatwa vipande vipande.

Kuna mazao mengine ambayo zamani hayakujulikana sana lkn Kwa Sasa ni dili mfano uduvi,konokono nk Kwa Sasa ni dili sio kama zamani.

MAENDELEO:- Kanda hii hata Kwa maendeleo haiko nyumba ukilinganisha na mikoa mingine.

Utakubaliana na Mimi Kanda ya ziwa imezipiku mikoa mingine sana au Kanda nyingi sana hapa Tanzania.

Yote haya ni vile watu wa Kanda ya ziwa sio wavivu. Ni Moja ya watu wanao amini mtaji wa masikini. Ni nguvu zake mwenyewe.

Hapa utakutana na wasukuma. Jamaa Hawa mbeze Kwa vitu vingine lakini sio Kwa kazi lahasha. Nitoe mfano kidogo.

Miaka ya nyuma Hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 wasukuma ni watu walikokuwa na umoja wa kusaidiana sana kazi japo na Sasa Bado ipo baadhi ya maeneo. Ilkuwa Hivi Kila level Fulani ya umri walikuwa na umoja wao wa kusaidiana kazi kama kulima nk

Unakuta wametengeneza vikundi vyao alimaarufu kama "Malika" hapa ukiwakuta wasukuma wanalima kama ndo mala Yako ya kwanza lazima usimame ukaangalie. Kwanza zinaimbwa nyimbo huku wamepanga mistari na majembe yanakata Kwa pamajo na hapo nizaidi ya wa20

Kuna mwingine labda anapiga zeze mwingine anaimbisha asee ilikuwa ni buridani ya aina yake muda huo Kuna wengine wananogesha Kwa kutupa jemba juu na linadakwa akiwa kwenye mstari na kilimo kinaendelea Wala hakuna kukatana.

Ngoja kwanza watu wa dar hii huwezi elewa, ngoja tuendelee sasa.

Mtasema sijawaelezea wahaya nk. Ukweli sijawahi fika tofauti na kusoma history Yao ambayo hata wewe hapo umeisoma.

Watu wa Kanda ya ziwa umoja wao umewafanya kuwa ushirikiano mkubwa sana Hadi Kuna baadhi ya maeneo huo umoja upo wanaita bhuyobhe.

UKARIMU: Sote tukakubaliana Hawa watu especially wasukuma maana ndio wengi.

Ni watu wakarimu sana narudia ni watu wakrimu mnoo. Hawa jamaa haatakagi shida na mtu wewe ukija na element zako utawaona wajinga hawajielewi.ila utawakimbia mwenyewe tu.

Ni watu wa maadili sana. Mfano ukikamatwa ugoni(uzinzi) mtapigwa viboko hadharani na kutengwa,vijana wenye tambia za ajabu ajabu mboko lazima,umeolewa ukatukana watu ovyo mboko, wamealika kwenda kwenye nguvu kazi wewe ukaendelea na issue zako mboko hukoswi au faini au vyote Kwa pamoja.

Ukipata msiba ni mtaa wote (igulya) ikiwa na maana huduma za kupika unapika kwako unapeleka chakula msibani miji yote usipopeleka faini au mboko. Nk.

Kwanza ni watu wasiopenda kesi hata kama umemkosea atadili na wewe kivingine nasio kupelekana mahakamani hii ya mahakamani imekuja Hivi karibuni.

Msukuma hata umkosea vipi atakuambia hakuna shida(nduho tabu) Hilo neno ukilisikia Kwa ngosha na unajua umemkosea fanya kulisolve mapema. Jamii hii inaamini ushirikina kuliko hata Mungu hivo chunga sana.

Sio ajabu kukuta msukuma na pingu mkononi na ukamuuliza jirani **** shida Gani?!? Atakujibu Ndoho tabu (hakuna shida)

Zaman hizo wasukuma kwenye sikukuu walikuwa wakipika chakula ule muda wa kula majirani wote na watoto wao wanakusanyika kwenye familia Moja wanakula pamoja..

Yaani hii Kila family inabeba chakula chake na kupeleka sehemu Moja ambayo wamekubaliana kuwa sikukuu hii tutakaa Kwa flani hii ilikuwa inaonyesha namna Gani Hawa watu wanaumoja na upendo!

Mambo ni mengi muda mchache Kwa Leo ni haya.

Je, wewe unaifahamje Kanda ya ziwa?

IMG_20220428_113553_082.jpg
 
Dhahabu na uvuvi vimechangia pakubwa imani za kishirikina,kanda ya ziwa hawana mpinzani.
 
Back
Top Bottom