Ukimya uliokuwepo Ikulu umenistua!!

Ukimya uliokuwepo Ikulu umenistua!!

Ukishatambua makam wa rais ni nan inabidi uwe mpole😉
 
Ka makonda kamewatonesha majipu hawa mapapa na vipapa
 
Akiwepo Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye na mawaziri kadhaa wa serikali ambao ni makada nguli wa CCM kwenye kuapishwa kwa viongozi waliokuwa wameteuliwa na Mheshimiwa Rais, nimeona kuna ukimya wa kutisha sana hadi nimejiuliza kulikoni?

Hata Makonda alipopewa Pongezi zake sikuona kama kuna mwitikio toka kwa viongozi wengine wa serikali walipokuwemo mle ndani. utulivu hata wakati Mheshimiwa Rais akijaribu kuwa mcheshi kwa wageni wake makofi yaliyokuwa yanapigwa yalikuwa haba sana. Hii hali imenifikirisha sana. Au kwa kuwa leo ni Week-end watu wana uchovu wa jana?

Kwa mtu yeyote mwenye BUSARA, this is a VERY, and VERY STRONG MESSAGE to MAGUFULI and his HENCHMEN MAKONDA! Nobody is happy in Tanzania at this very hour.
Asiyejua kufa atazame kaburi! Muda utasema tu!
 
Hata kama ungekuwa ni wewe angalia body language ya mkuu the angalia na maneno yake mkuu wa Kaya Akiwa ktk hali kama hiyo huku selikali yote ikiwa pale waziri wa Ulinzi yupo pale, waziri wa mambo ya ndani yupo pale,makamu yupo na PM yupo pale kaimu Jaji mkuu yupo pale na CDF yupo pale halafu mkuu anaongea vile daaaahh hakuna mwenye kuwa na Amani na amesema hii ni vita nadhani hakuna mwenye kushangilia vita hali ni tete mkuu katangaza vita na uelewe neno LA mkulu ni sheria hakuna mwenye Amani moyoni pale hata kama ungekuwa wewe
 
Tangazeni tu. Hata majina ya watu waliojichotea hela kwenye akaunti ya Tegeta-Escrow yalitangazwa tena bungeni!!
Usihamishe magoli,hatupo kwenye Escrow hapa.Mwambie Mbowe kesho awahi,akichelewa atakamatwa,watu hawatanii
 
Kwa kweli hata mimi hilo limenishangaza sana leo. Ikulu ilikuwa imejaa UNYONGE, HOFU, MASHAKA, WASIWASI, UKIWA, SIMANZI, WOGA nk.

Nimewaona mawaziri wakiwa katika hali ya sintofahamu kubwa sana.

What is wrong?
Gari limekata brake kwenye mteremko dereva kawambia abiria hakuna kuruka wala kupiga kelele naye Kaufumba macho
 
Tangazeni tu. Hata majina ya watu waliojichotea hela kwenye akaunti ya Tegeta-Escrow yalitangazwa tena bungeni!!
Usihamishe magoli,hatupo kwenye Escrow hapa.Mwambie Mbowe kesho awahi,akichelewa atakamatwa,watu hawatanii
 
Baada ile kauli siku ile ya kuadhimisha siku ya mahakama kuwa alipata taarifa kuna watu walimpigia IGP simu kumpa ushauri kuhusu zoezi la Makonda kila waziri sasa anajiona hayuko huru wala salama na mawasiliano yao yanakuwa taped 24/7 . Ukichunguza utagundua mawaziri wa sasa hawako pamoja hata kwenye bata kila mtu kivyake .
 
Unafiki mtupu, ni lini ulimuona Mwalivyoicheka cheka Ikulu au ndio mmeanza viji maneno vyenu?

Mkubwa vipi, mbona unakuwa too harsh kiasi hiki?

Jamaa katoa maoni yake tu kwa kadiri alivyoona na unaweza kukubaliana naye au ukapita zako na kuendelea na safari....

Huo ndiyo ustaarabu lakini inavyoonekana tatizo la "kuleta vimaneno neno a.k.a umbeya" liko kwako na si kwa mleta mada
 
Ni nani awezaye kug0nganisha macho na mukulu?
 
Attachments

  • IMG_20170212_224605.JPG
    IMG_20170212_224605.JPG
    44.2 KB · Views: 47
Akiwepo Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye na mawaziri kadhaa wa serikali ambao ni makada nguli wa CCM kwenye kuapishwa kwa viongozi waliokuwa wameteuliwa na Mheshimiwa Rais, nimeona kuna ukimya wa kutisha sana hadi nimejiuliza kulikoni?

Hata Makonda alipopewa Pongezi zake sikuona kama kuna mwitikio toka kwa viongozi wengine wa serikali walipokuwemo mle ndani. utulivu hata wakati Mheshimiwa Rais akijaribu kuwa mcheshi kwa wageni wake makofi yaliyokuwa yanapigwa yalikuwa haba sana. Hii hali imenifikirisha sana. Au kwa kuwa leo ni Week-end watu wana uchovu wa jana?
Huo ukimya ni kwasababu walikuwa wanafuatilia kilichokuwa kinaendelea kwa makini, kwani wewe ulitaka wapige kelele.
 
Back
Top Bottom