Yepi? Awamu ya nne haikuwa na character assassination kama hii. Imejenga miundombinu mingi, imepandisha mishahara kwa kiasi kikubwa, imetoa fursa za elimu nyingi, ilikuwa na ubinaadamu mwingi, imetoa ajira nyingi, imekuza biashara nyingi, imejenga mashule mengi, imeanzisha vyuo vingi, imevutia wawekezaji wengi, imesomesha watumishi wengi, wengi walipata fursa ya kujijengea vibanda vya kuishi, imekuza ushirikiano vizuri sana na mataifa ya nje kwa ajili ya maendeleo, imeibua fursa nyingi za kilimo, biashara na sanaa. List haina mwisho.
Mwaka na nusu huo, tuna barabara moja ya mwenge tu, utapata wapi jeuri ya kuisema awamu ya nne? Acheni kutafuta visingizio uchumi unakufa huo.