Ukimya na Usiri wangu unanifanya nionekane Usalama wa Taifa

sanalii

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,434
5,099
Iko hivi

1. Mimi sinywi pombe, sigara wala siendi club hivyo sina sababu ya kwenda sehemu za starehe kama bar.

2. Sina ushabiki wa mpira, hivyo sina sababu ya kujichanganya kwenye stori za mpira au mabanda ya mpira.

3. Sina account ya mitando ya kijamii kama instagram, Facebook au Twitter, nk hivyo hawanioni huko.

4. Nashiriki kwenye misiba na matatizo mengine ya kijamii lakini sipendelei sherehe za harusi na burudani nyingine. Mambo ya Gettogether siyapendelei sana kazini.

5. Nikitoka kazini niko ndani na familia yangu, kifupi kutulia ndani hakunichoshi.

Kwa tafsiri ya jamii mimi naingia kwenye sifa mbili

1. Sijichanganyi
2. Ni msiri sana

Kwa mawazo yao eti mimi ni Usalama wa taifa ila ukweli ni kua

1. Sina hata mtu mmoja ninaemjua anafanyia kazi idara ya usalama wa taifa.

2. Sina connection yoyote hata kazi yenyewe nilipata kwa mbinde sana. Jinsi ninavyoishi ni maamuzi yangu tu.

Hofu yangu mi kua wafanya kazi wenzangu au jamii wataniona kama snich/ shushushu ambae kuda wote nitakua tayari kukusanya taarifa za watu kitu ambacho sio sahihi kabisa.
 
Toka zungumza na watu mkuu hao ndyo ndugu zako, yakikufika kwa kuwa kila mmoja humfika watakusaidia!!
"Kwenda msibani tu kusaini ni hajamaliza, huenda raia wanakupimia tu"

Ikiwa wewe huwezi, angalau mkeo awe mtu wa watu, itakufaa sana siku za majonzi na furaha!
 
Iko hivi

1. Mimi sinywi pombe, sigara wala siendi club hivyo sina sababu ya kwemda sehemu za starehe kama bar.

2. Sina ushabiki wa mpira, hivyo sina sababu ya kujichanganya kwenye stori za mpira au mabanda ya mpira.

3. Sina account ya mitando ya kijamii kama instagram, Facebook au Twitter, nk hivyo hawanioni huko.

4. Nashiriki kwenye misiba na matatizo mengine ya kijamii lakini sipendelei sherehe za harusi na burudani nyingine. Mambo ya Gettogether siyapendelei sana kazini.

5. Nikitoka kazini niko ndani na familia yangu, kifupi kutulia ndani hakunichoshi.

Kwa tafsiri ya jamii mimi naingia kwenye sifa mbili
1. Sijichanganyi
2. Ni msiri sana

Kwa mawazo yao eti mimi ni Usalama wa taifa ila ukweli ni kua

1. Sina hata mtu mmoja ninaemjua anafanyia kazi idara ya usalama wa taifa.

2. Sina connection yoyote hata kazi yenyewe nilipata kwa mbinde sana. Jinsi ninavyoishi ni maamuzi yangu tu.

Hofu yangu mi kua wafanya kazi wenzangu au jamii wataniona kama snich/ shushushu ambae kuda wote nitakua tayari kukusanya taarifa za watu kitu ambacho sio sahihi kabisa.
Kiufupi ungeandika kuwa wewe ni camouflage animal specie. Waliosoma sayansi za wanyama wangekuelewa vizuri zaidi.
 
Vyote ulivyovitaja hakuna sifa hata moja ya classified! Isipokuwa unapendelea kuwa ndani ya idara hiyo kama mtiririko wa undani wako!
 
wewe unajishtukia tu siku hizi kila mtu na mambo yake unadhani nani wa kukuhisi wewe ni usalama wa taifa kama sio unajihisi mwenyewe. Fanya kazi
 
Back
Top Bottom