mediaman
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 451
- 687
Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.
Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.
T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo, ni wazi watakuwa ama wamesikia au kuona vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakitoa shuhuda za uponyaji baada ya kuombewa na T.B. Joshua. Sio mhubiri huyo tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea watu wenye magonjwa mbalimbali. Kuna mhubiri fulani, Tanzania, yeye sio tu anaombea wagonjwa, amewahi kuonekana pia akiombea mtu aliyekufa, kisha mtu huyo akafufuka!
Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).
Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.