BBC wamechelewa sana kumchafua T.B Joshua, Afrika imekua sana kiroho

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Documentary iliyoachiliwa na Shirika la habari Duniani (BBC) ikionesha mashahidi wanaoonesha maovu dhidi ya Mtumishi wa Mungu mwendazake T.B Joshua ni ishara tosha kuwa nguvu ya Imani na ukuaji wa kiroho Afrika ni tishio Kwa kikundi fulani cha watu kutekeleza ajenda zao.

Ukweli ni kwamba Afrika imefikia kiwango cha ukuaji wa kiroho ambacho haiwezi kurudi nyuma "point of no return". Imani juu ya Mungu katika bara hili ni hatari sana wa watu walioamua kugeyza mahekalu kuwa kumbi za starehe.

Watumishi wa Mungu Afrika wanaonekana kama kikwazo kikubwa sana na wacheleweshaji wa matukio makubwa mabaya yanayopangwa kutokea kwa jamii ya wanadamu wakaazi wa Dunia.

Kinachowaumiza zaidi ni uhalisia kupindika katika namna ambayo upepo wa imani juu ya Mungu unaonekana kutoka Afrika kuelekea Ulaya, ni kama historia imejigeuza na iliyoitwa kuwa nyeusi wakati ni nyeupe inajionesha uhalisia wake.
 
Sawa ila tb joshua makenzi mwamposa na wengine wanamna yake ni matapeli
Kuna tapeli mwengine taipu ya tb nasikia kakamatwa huko Tanzania anawahubiria watu eti wasisome huu si utapeli
Wakristo munatakiwa muamke shauri lenu nyie mkweli munamuona mamba tuuuu 😀
 
Acha kuishi kwa habari za kusikia,tafuta ushahidi...
 
Acha kuishi kwa habari za kusikia,tafuta ushahidi...
Kwamba mwamposa hawapigi kondoo wake pale kawe
Siajabu nawe kaishawahi kukupiga ila unaona sawa
Hata gwaji boy aliwaaminisha kama anafufua wafu nanyie wakristo mkamkubalia 🤣😀🤣
 
Africa imekua kiroho na kiimani kwa kuwa mazuzu na misukule
Wanajidhirisha kuwa ni aina ya binadamu wenye kiwango kidogo sana cha ki akili na hawakukosea kutufananisha na nyani.
Kwa ujumla ni aibu tupu
 
Back
Top Bottom