Ukienda kwa Nabii T.B. Joshua, jihadhari sana

mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.

Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.

T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo, ni wazi watakuwa ama wamesikia au kuona vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakitoa shuhuda za uponyaji baada ya kuombewa na T.B. Joshua. Sio mhubiri huyo tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea watu wenye magonjwa mbalimbali. Kuna mhubiri fulani, Tanzania, yeye sio tu anaombea wagonjwa, amewahi kuonekana pia akiombea mtu aliyekufa, kisha mtu huyo akafufuka!

Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).

Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.
 
testifier

Member
Apr 21, 2021
47
125
Mtu akienda kuombewa akaambiwa atoe kwanza pesa ndio aombewe, asikubali. Yesu hakuwalipisha pesa wagonjwa. Hata wanafunzi wake alipowapa mamlaka ya kupoza wagonjwa, aliwaambia amewapa mamlaka hayo bure hivyo watoe huduma hiyo bure. Sadaka tu ndio mtu anaweza kutoa, tena kwa hiari na moyo mkunjufu, sio kwa kulazimishwa.
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,045
2,000
Yaani ningekuwa nakujua ningekupa.zawadi kwa some ulilolitoa. Shida wengi hawajui.neno wala.hawasomi neno.Mungu huponya wote bure ila gharama yake ni kuacha dhambi. Kingine na mazingira ya kupata ugonjwa binadamu anatakiwa ujihoji, utubu na kuacha dhambi.
 
Banjuka

JF-Expert Member
May 7, 2021
440
1,000
Watu watafute maarifa wenyewe binafsi kwa sababu hata hawa watumishi ni binaadam kama wewe, kama dhambi wanatenda kama wengine, hivyo kwanini uombewe na mtenda dhambi mwenzio, tafuta maarifa ya kuacha dhambi wenyewe. Na mzigo wa dhambi ni mzigo ambao ukiubeba huwezi jua kama ni mzigo utatembea nao miaka nenda rudi, mpaka ugundue utakua umeshamaliza waganga wote kwa ajili ya kukuagua.
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
6,503
2,000
Mtu akienda kuombewa akaambiwa atoe kwanza pesa ndio aombewe, asikubali. Yesu hakuwalipisha pesa wagonjwa. Hata wanafunzi wake alipowapa mamlaka ya kupoza wagonjwa, aliwaambia amewapa mamlaka hayo bure hivyo watoe huduma hiyo bure. Sadaka tu ndio mtu anaweza kutoa, tena kwa hiari na moyo mkunjufu, sio kwa kulazimishwa.
Hii umepiga chini ya mkanda. Eti nikafanyiwe naombi na Gwajima au Masanja Mkandamizaji🙄🙄🙄! Hawa wanaojiita manabii na Maaskofu uchwara wanawapiga sana watu wanaomtafuta Mungu.
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,321
2,000
Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.

Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.

T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo watakubaliana nami kuwa wameishasikia shuhuda za vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakipona baada ya kuombewa. Sio T.B. Joshua tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea wenye magonjwa mbalimbali.

Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).

Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.
Na wengi wamekuwa wakipuuzia hili,halafu magonjwa yanapowarudia wanaanza kusema mchungaji flani ni fake kwakuwa bado hajapona,wakati ameshasahau alishapona na akatoa na shukrani.Kizuri ni kuwa TB Joshua ukienda kwake kabla ya maombezi huwa anawatahadharisha mapema hili kabla ya maombezi...
 
Umenena vema
 
Abby Newton

JF-Expert Member
Nov 12, 2017
1,209
2,000
Na wengi wamekuwa wakipuuzia hili,halafu magonjwa yanapowarudia wanaanza kusema mchungaji flani ni fake kwakuwa bado hajapona,wakati ameshasahau alishapona na akatoa na shukrani.Kizuri ni kuwa TB Joshua ukienda kwake kabla ya maombezi huwa anawatahadharisha mapema hili kabla ya maombezi...
Tb Joshua is an Agent of the devil .Nakushangaa uliekuja hapa kupigia kampeni jitu jizi na tapeli km Tb Joshua. Kwanza mahubiri yake yamejaa udhalilishaji akionyesha "live" wanawake wakijifungua baada ya kupokea maombi,na anatumia matukio haya( ArrangedMiracles) km chambo ya kuwavuta watu wengi wenye dhiki mbalimbali,hasa ukizingatia ulimwengu wa sasa watu wana dhidi na shida za kila aina.

Lakini pia hata imani yake ni ya kutia shaka.Mara awafundishe watu kufanya maombi kutumia shanga,maji na stika yenye picha yake.Je ndo maandiko yameagiza ivo? Je hayo ndio mafundisho ya WOKOVU? Wizi mtupu!!

Kibaya zaidi anaviuza hivo vitu km bidhaa,japo amekuwa akidanganya kupitia TV yake kuwa anagawa bure. Muongo! Hakuna kitu anachotoa bure hata kimoja! "You will have to pay for either direct or indirectly".Wajinga wengi wasiojua kutafakari maandiko wameamini na kuishia kupigwa pesa nyingi.

Tb Joshua anatumia uchawi na ujanja ujanja katika kuwateka watu. Nakushauri acha kupoteza muda na manabii wajanja wajanja km Prophet Bushiri,TB Joshua,Mwamposa,Gwajima, Suguye na wengineo utapoteza mda na pesa zako bureee.
 
Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,736
2,000
Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.

Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.

T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo watakubaliana nami kuwa wameishasikia shuhuda za vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakipona baada ya kuombewa. Sio T.B. Joshua tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea wenye magonjwa mbalimbali.

Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).

Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.

Mkuu mediaman nakusalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimependa hoja ulizozitoa ILA natatizika kidogo na jinsi kichwa cha habari kilivyokaa; kinaweza kupeleka ujumbe ambao sio.

Ahsante
 
Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,736
2,000
Tb Joshua is an Agent of the devil .Nakushangaa uliekuja hapa kupigia kampeni jitu jizi na tapeli km Tb Joshua. Kwanza mahubiri yake yamejaa udhalilishaji akionyesha live wanawake wanaojifungua baada ya kupokea maombi yake. Anafanya km chambo ya kuwavuta watu kupitia matukio ya kutengenezwa na kupangwa wengi wavutike.

Lakini pia hata imani yake ni ya kutia shaka.Mara awafundishe watu kufanya maombi kutumia shanga,maji na stika yenye picha yake ndo maandiko yameagiza ivo? Kibaya zaidi anauza maji,shanga na stika km bidhaa.

Wajinga wengi wasiojua kutafakari maandiko wameamini na kuishia kupigwa pesa nyingi.Tb Joshua anatumia Nakushauri acha kupoteza muda na manabii wajanja wajanja km Prophet Bushiri,TB Joshua,Mwamposa,Gwajima, Suguye na wengineo utapoteza mda na pesa zako bureee.

Mkuu Abby Newton habari. Ulichoandika hapa kinaeleza mengi ambayo hujayasema. Naomba nikuulize, Je Yesu Kristo ameshafanyika Bwana na Mwokozi wa Maisha yako? Je leo ikiwa ndio siku yako ya mwisho duniani, una shuhudiwa ndani yako Roho yako inaelekea mbinguni au jehanamu?

Mkuu Abby Newton, naomba uelewe kwamba sijakupinga kwa kila ulichoandika ILA ni vyema ukafahamu kwamba mambo ya Rohoni (utambuzi) hutambuliwa na watu wa Rohoni tu (Waliookoka). Kwahiyo Mkuu Abby Newton chukua hatua mapema ya kumpokea Kristo katika maisha yako

Ahsante
 
mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Tb Joshua is an Agent of the devil .Nakushangaa uliekuja hapa kupigia kampeni jitu jizi na tapeli km Tb Joshua. Kwanza mahubiri yake yamejaa udhalilishaji akionyesha live wanawake wanaojifungua baada ya kupokea maombi yake. Anafanya km chambo ya kuwavuta watu kupitia matukio ya kutengenezwa na kupangwa wengi wavutike.

Lakini pia hata imani yake ni ya kutia shaka.Mara awafundishe watu kufanya maombi kutumia shanga,maji na stika yenye picha yake ndo maandiko yameagiza ivo? Kibaya zaidi anauza maji,shanga na stika km bidhaa.

Wajinga wengi wasiojua kutafakari maandiko wameamini na kuishia kupigwa pesa nyingi.Tb Joshua anatumia uchawi na ujanja ujanja katika kuwateka watu. Nakushauri acha kupoteza muda na manabii wajanja wajanja km Prophet Bushiri,TB Joshua,Mwamposa,Gwajima, Suguye na wengineo utapoteza mda na pesa zako bureee.
Nani amekwambia nampigia debe T.B. Joshua? Point kuu ya thread hii ni kwamba ukiombewa (hata na shemasi au jirani yako) ukapona, usitende dhambi tena. Hilo ni Agizo la Yesu, sio la T.B. Joshua.
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,321
2,000
Tb Joshua is an Agent of the devil
emoji48.png
.Nakushangaa uliekuja hapa kupigia kampeni jitu jizi na tapeli km Tb Joshua. Kwanza mahubiri yake yamejaa udhalilishaji akionyesha live wanawake wanaojifungua baada ya kupokea maombi yake. Anafanya km chambo ya kuwavuta watu kupitia matukio ya kutengenezwa na kupangwa wengi wavutike.

Lakini pia hata imani yake ni ya kutia shaka.Mara awafundishe watu kufanya maombi kutumia shanga,maji na stika yenye picha yake ndo maandiko yameagiza ivo? Kibaya zaidi anauza maji,shanga na stika km bidhaa.

Wajinga wengi wasiojua kutafakari maandiko wameamini na kuishia kupigwa pesa nyingi.Tb Joshua anatumia uchawi na ujanja ujanja katika kuwateka watu. Nakushauri acha kupoteza muda na manabii wajanja wajanja km Prophet Bushiri,TB Joshua,Mw
Heri yako hapo unapoamini penye uhakika wa kwenda Mbinguni...
 
mediaman

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
453
1,000
Nimependa hoja ulizozitoa ILA natatizika kidogo na jinsi kichwa cha habari kilivyokaa
Ahsante kama umezipenda hoja. Sidhani kama kichwa kina shida iwapo mtu atasoma(content)mwanzo hadi mwisho kama ulivyofanya wewe. Mtu akiishia kusoma tu kichwa ni wazi anaweza kutatizika.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
10,300
2,000
Kansa ikimrudia mtu ndo easy assumption kuwa Katenda tena dhambi?
Seriously?

Niliposoma title ya huu uzi nilidhani ilikuwa ONYO watu wasiende huko Nigeria kwa T.B. Joshua kwani wangeweza kudhurika!!!
I thought it was a precautionary note!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom