Ukienda kwa Nabii T.B. Joshua, jihadhari sana

Kansa ikimrudia mtu ndo easy assumption kuwa Katenda tena dhambi?
Seriously?
Cancer huwa inaenda into remission, ikirudi inakuwa aggressive kuliko hapo awali.
Nimeuguza ndugu wa karibu, inaumiza SANA!
Kwa maumivu yale, dhambi sijui wanatenda saa ngapi?? Hata wakipata nafuu, siyo watu wale wale, huwa wanyenyekevu na wenye kumtii na kumshukuru Mungu.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Nani amekwambia nampigia debe T.B. Joshua? Point kuu ya thread hii ni kwamba ukiombewa (hata na shemasi au jirani yako) ukapona, usitende dhambi tena. Hilo ni Agizo la Yesu, sio la T.B. Joshua.
Muhimu ni watu kufundishwa kumpokea Yesu na kupata wokovu. Kuugua na kufa ni sehemu ya uwanadamu wetu. Shida watu wa leo wanamlazimisha Mungu awazuie wasiugue wala wasife.Wanamlazimisha Mungu awape gari, nyumba, watoto na ndoa bila kukumbuka kuwa kwenye biblia kuna watakatifu wengi waliokaa bila watoto kwa mrefu,wapo waliokuwa masikini licha ya kumtumaini Mungu kwa dhati,lakini waliendelea kumtumainia Mungu badala kukimbia huku na kule kutafuta uponyaji kwa manabii.

Ukikuta mtu anaombewa halafu anarudia kufanya dhambi baada ya kuombewa basi ujue hajapokea Wokovu bali alifuata uponyaji tu.

Watu wafundishwe kwanza kumjua Yesu Kristo kwanza ndio uponyaji ufuate baadaye.
 
Kwa neema ya Mungu tumeiona tena siku ya leo tukiwa na uzima na nguvu ya kuingia katika jukwaa letu pendwa (JF), ili kupashana habari, kutiana moyo na kushauriana. Wakati sisi tunafurahia mada mbalimbali zinazoletwa humu, tusisahau kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki zetu wana huzuni kubwa kwakuwa wamelazwa hospitalini muda mrefu kutokana na magonjwa sugu au "yasiyosikia dawa" kama vile kansa, ukimwi, kisukari, magonjwa ya moyo, nk. Ni jukumu letu kutafuta namna ya kuwasaidia.

Watu wanaougua muda mrefu hupewa ushauri mwingi sana wa jinsi ya kujinasua kutoka katika magonjwa sugu. Wagonjwa wa aina hiyo mara nyingine hushauriwa waende kwa wahubiri, wachungaji, manabii au mitume wakaombewe. Huaminishwa kuwa wengi katika wale wanaoombewa hupokea uponyaji kwa njia ya muujiza tena bila kulipa gharama yoyote.

T.B. Joshua anafahamika sana ulimwenguni kutokana na maombezi anayoyafanya katika kanisa lake kubwa, lililoko Nigeria. Kwa wanaofuatilia habari za mhubiri huyo, ni wazi watakuwa ama wamesikia au kuona vipofu, viwete, viziwi na wenye magonjwa sugu wakitoa shuhuda za uponyaji baada ya kuombewa na T.B. Joshua. Sio mhubiri huyo tu anayeombea wagonjwa, wapo wahubiri wengine Kenya, South Africa, Korea ya Kusini, USA nk wanaoombea watu wenye magonjwa mbalimbali. Kuna mhubiri fulani, Tanzania, yeye sio tu anaombea wagonjwa, amewahi kuonekana pia akiombea mtu aliyekufa, kisha mtu huyo akafufuka!

Hao wote wanafuata nyayo za Yesu. Siku moja Yesu alipokuwa duniani alimponya mtu aliyekuwa mgonjwa sana kwa miaka 38. Alikuwa hawezi kuinuka kutoka kwenye godoro lake. Yesu alimponya kwa kumwambia tu, "inuka, umekuwa mzima, jitwike godoro lako uende." Akainuka, akaenda zake, mzima kabisa! Baadaye Yesu alimkuta huyo mtu hekaluni akamwambia: "Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi."(Yohana 5:14).

Je, una ndugu, jamaa au rafiki anayeteseka na magonjwa mabaya? Ametibiwa hospitali miaka mingi lakini imeshindikana? Sio vibaya ukimshauri aende akaombewe. Akikubali ushauri wako, akaamua kwenda kuombewa mahali popote - kwa T.B. Joshua au kwa mhubirii yeyote maarufu, mwambie akiombewa, akapona, ajihadhari sana asitende dhambi tena. Mtu akitenda dhambi baada ya kupona kwa muujiza, kuna uwezekano wa kurudiwa na ugonjwa uleule kwa viwango vya juu zaidi au kupatwa na jambo baya zaidi. Nawatakia watu wote maisha ya heri.
Kinachofuata ni kutoa namba ya simu na kujiita wakala wa TB Joshua,hongera kwa promo mkuu
 
Christo hakuja kumponya mtu dunian wala kutenda miujiza yoyote dunian
Yesu alikuwa anakwenda kila mahali wilayani Galilaya, akifundisha katika masunagogi na kuhubiri Habari Njema juu ya ufalme wa Mungu. Aliponya kila namna ya maradhi na magonjwa waliyokuwa nayo watu. Habari zake zikaenea pande zote za Siria. Wagonjwa wote wenye maradhi ya kila namna na wale waliosumbuliwa na kila namna ya taabu: Waliopagawa na pepo, wenye kifafa na watu waliokuwa wamelemaa, walipelekwa kwake; naye akawaponya wote(Mt 4:23-25) BHN
 
Mtu akienda kuombewa akaambiwa atoe kwanza pesa ndio aombewe, asikubali. Yesu hakuwalipisha pesa wagonjwa. Hata wanafunzi wake alipowapa mamlaka ya kupoza wagonjwa, aliwaambia amewapa mamlaka hayo bure hivyo watoe huduma hiyo bure. Sadaka tu ndio mtu anaweza kutoa, tena kwa hiari na moyo mkunjufu, sio kwa kulazimishwa.
Nakazia kwa wino mwekundu
 
Yaani ningekuwa nakujua ningekupa.zawadi kwa some ulilolitoa. Shida wengi hawajui.neno wala.hawasomi neno.Mungu huponya wote bure ila gharama yake ni kuacha dhambi. Kingine na mazingira ya kupata ugonjwa binadamu anatakiwa ujihoji, utubu na kuacha dhambi.
Mkuu kuna watu hawajawahi kutenda dhambi Ila ni wagonjwa taabani,by the way nimeupenda mwandiko wako,hongera!.
 
Waongo tuu Kama watu wangekua wanapona kweli kusinge kua na hospitali huko Nigeria

Wagonjwa wanaoumwa ukwelii wapo mahospitalini wawaombee wao wapone ndo tuamini

Hawa wanaojiita manabii waue siku waende Muhimbili pale wakawaombee wagonjwa Kama watapona
 
Mkuu kuna watu hawajawahi kutenda dhambi Ila ni wagonjwa taabani,by the way nimeupenda mwandiko wako,hongera!.
Umejuaje hawajatenda dhambi kwenye biblia 1Yohana 1:8-10 inasema.mkisema hamna dhambi mnajidanganya.Kwa hiyo ajikague na.kujitafakari Mungu ni mwaminifu atajua wapi kuna shida.Matauo 16:19 tumepewa fungus za kufunga chochote dunuani na.mbinguni kitafungwa.Funga magonjwa na roho zote zilizokinyume huyo ndugu yako atapona
 
Yaani ningekuwa nakujua ningekupa.zawadi kwa some ulilolitoa. Shida wengi hawajui.neno wala.hawasomi neno.Mungu huponya wote bure ila gharama yake ni kuacha dhambi. Kingine na mazingira ya kupata ugonjwa binadamu anatakiwa ujihoji, utubu na kuacha dhambi.
hivi kwani tunapatwa na magonjwa kwasababu tunatenda dhambi?
 
Sio assumption; hiyo ni kwa mujibu wa maneno ya Yesu(Yn 5:14). Kwahiyo kama mtu alipona kansa kabisa kwa muujiza(kwa kuombewa tu) kisha baadaye ikamrudia kuna uwezekano mkubwa mtu huyo baada ya kupona aliendelea na maisha ya dhambi. Kama amedumu katika utakatifu, akaugua tena ugonjwa huo, zipo sababu nyingine(za kibiblia) kwanini watakatifu wanaugua.
kwani watu wanaougua magonjwa km kansa dhambi ndio sababu ya wao kuugua hayo magonjwa?
 
Back
Top Bottom