Ukiacha kusikia sauti za watu wengi zikikupigia kelele za mwizi huku zikikujia na hatimaye ukakimbia, kituko gani kingine bangi imewahi kukufanyia?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Dec 18, 2022
2,301
4,243
Ilikuwa 2000 hiyo. Nimetoka shule kama kawaida, baada ya kubadilisha tu sare na kupata msosi, nikaelekea kijiweni tulikokuwa tunacheza mpira kukiwakilisha kitaa timu yetu ya mtaa. Hapo tulikuwa na kocha wetu na timu ilikuwa na mchanganyiko wa watu mbalimbali; wavuvi, wa vijiweni tu na siye wanafunzi.

Kama kawa, wa mtaani walikuwa wanaendelea na mambo yao bila kujali uwepo wetu watoto. Wasiojali walikuwepo pia, tulikuwa tunashawishiwa hapa na pale. Sikuwahi kushawishika kujaribu chochote ila siku hiyo mambo yalikuwa tofauti.

Nimefika nimejumuika na wenzangu niliowakuta, tukatulia tunapiga stori mbili tatu huku tukiwasubiri waliochelewa. Kama kawaida, wazee wa kumuenzi Bob marley walikuwa wanaendelea na mambo yao. Mmoja, niliyekuwa naelewana nae sana tu akanipasia kitu. Nikajisemea, ''mbona wao wanavuta na wako vizuri tu, ngoja nijaribu nione ina ladha gani''. Nikapokea kijiti na kuendelea kukiwasha.

Nimepiga 'pafu' Kama tatu tu hivi nikaanza kuhisi masikio Kama yanasikia vishindo fulani hivi kwa mbaaaali. Nikataka kushangaa kidogo lakini nilipoona kuna wenzetu kadhaa walikuwa wanapasha basi nikajisemea tu kuwa watakuwa ni wao ingawa bado nilikuwa ndani ya kasintofahamu kidogo. Nikaendelea kupiga kitu........pafu la saba, nane, tisa, kumi mara nahisi masikioni vile vishindo vikizidi kuwa karibu tena vikiwa vingi huku kukiwa na sauti flani za watu nazisikia kama wanazoza. Nikaona hata hapa kuna jambo, nikanyanyuka. Ebwana ile kusimama tu nasikia, 'mwizi huyoooo! mwizi huyooooo! Mwizi huyooo!' Zile kelele zilikuwa zinanijia mimi. Nikaona ukisikia kuchomwa moto ndiyo huku, nikatimua mbio nikiwa sielewi tu hata ninakokimbilia.

Kilichofuata hata sikukijua mi nilijikuta tu nimeamka nikiwa nyumbani usiku sana huku Mama yupo karibu yangu ananiangalia. Siku iliyofuata nikala mabanzi na viboko vya kutosha na ndo ukawa mwisho wa kujaribu ile kitu.

Karibuni tushirikishane vituko vya bangi tulivyowahi kushuhudia.
 
Sikuwahi kupata changamoto yoyote ya huu mmea mara ya kwanza kabisa 1979 huko jandoni musoma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom