SoC02 Ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii

Stories of Change - 2022 Competition

Mr_Isack

New Member
Aug 16, 2022
1
0
UTANGULIZI

Ukatili ni hali ya kusabishwa kwa makusudi mateso na kukosesha raha dhidi ya mtu mwengine, Ukatili baina aya ndugu, wapenzi au watu wakaribu ndani ya jamii unaweza ukawa ni ukatili wa kijinsia au ukatili kwa watoto unaoweza kufanywa na rafiki kwa rafiki, mzazi kwa mototo, jinsia moja kwa jinsia nyingine au baina ya wapenzi ndani ya jamii.

Utafiti umefanyika katika kata ya Mafiga, Mazimbu, Magadu, Kihonda, Mbuyuni na Kata ya saba saba ndani ya manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro nchini Tanzania, Utafiti huu umeenda sambamba na kubaini vyanzo na visababishi vya ukatili, Athali pamoja na njia za kutatua tatizo hili ndani ya jamii ambapo wanajamii walichangia mawazo na maoni yao kwa mapana na kusaidia ukamilishaji wa tafiti hii.

Utafiti huu umefanyika mwezi wa 2 hadi mwezi wa7 mwaka 2022 na mwanafunzi wa shahada ya maendeleo ya jamii mwaka wa pili Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA-MOROGORO ambae pia ni mwandishi wa andiko hili.

NJIA ZA UKUSANYAJI TAARIFA ZILIZO TUMIKA

Njia ya mahojiano imetumika katika ukusanyaji wa taarifa kwa wanajamii ambapo maswali yalikuwa sawa kwa kila mhojiwa ana kwa ana kwa kutumia mdomo, kutokana na kuwepo kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii, utafiti huu umegusa makundi mbali mbali ya wanajamii kulingana na nafasi zao ndani ya jamii kama ifuatavyo
Kiongozi wa dini ya kiislamu mmoja
Kiongozi wa dini ya kikristo mmoja
Kijana wa kike au wa kiume mmoja
Mwanaume au Mwanamke mzee mmoja
Na kiongozi wa chama cha kisiasa


MASWALI YALIYO ULIZWA KWA WAHOJIWA

Ni vitu gani vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii?
Nini kifanyike ili kuweza kupunguza na kutokomeza ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii? Katika ngazi ya ,
Familiya
Dini na
Serikali

Yafuatayo ni mawazo mbalimbali ya wahojiwa juu ya ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya Jamii

KIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU
Kiongozi huyu alitoa mawazo yafuatayo kuhusu vitu vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii;

Mipango ya Ibirisi shetani ambae anapambana kuiharibu Dunia
Ukatili, uonevu, mabavu na uasi wote unao fanywa na wanajamii ni kutokana na roho waovu wanao tawala vichwa vya binadamu wasio mwamini mwenyezi Mungu, Shetani huwatumia kutimiza haja zake na ukatili kuzidi kukithiri.

Kuishi bila Hofu ya Mwenyezi Mungu
Wanajamii wengi wanaishi bila hofu ya mwenyezi Mungu na kuto fata maagizo kama yanavyo tutaka tuishi kwenye maandiko matakatifu, bali wanadamu wamekuwa wakaidi na kuishi jinsi wanavyo taka wao, Hii huchangiwa sana na hali ya wanadamu wa kizazi hiki kutokuhuzuria sehemu za ibada na kujifunza yaliyo mema.

KIONGOZI WA DINI YA KIKRISTO
Kiongozi huyu alitoa mawazo yafuatayo kuhusu vitu vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii;

Imani potofu na ushirikina
Watu wengi wameingiwa na tamaa ya kufanikiwa muda mfupi na bila kutumia nguvu na kujikita katika imani potofu ya kupata pesa kwa nguvu za giza, mfano kuua ili wapate pesa.

KIJANA WA KIKE
Kijana huyu alitoa mawazo yafuatayo kuhusu vitu vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii;

Ukosefu wa Elimu
Ukosefu wa Elimu ni chanzo cha ukatili ndani ya jamii kwani mtu hushindwa kutofautisha mema na mabaya na kushindwa kujua sheria za nchi zianzo tuongoza.

Wivu na tamaa baina ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii
Wivu baina ya wanajamii hua chanzo cha ukatili, mfano mototo anaweza kuua mzazi wake kwa tama za mali.

KIONGOZI WA KISIASA
Kiongozi huyu alitoa mawazo yafuatayo kuhusu vitu vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii;

Kufeli kwa demokrasia
Kutokuwa na usawa, haki, na utawala wa kimabavu hupelekea ukatili dhidi ya tabaka la chini lisilo na sauti na mamlaka dhidi ya tabaka la juu ndani ya jamii, pia tabaka la chini linaweza kutumia njia haramu kukabiriana na tabaka tawala ndipo ukatili hukuwa na kuenea.

MWANAUME MZEE
Mzee huyu alitoa mawazo yafuatayo kuhusu vitu vinavyopelekea kukithiri kwa ukatili kati ya ndugu, wapenzi na watu wa karibu ndani ya jamii,

Umaskini
Umaskini na ugumu wa maisha vinachochea njia haramu za utafutaji pesa na mali, wanajamii wengi wanaoishi katika hali duni wamekuwa wenye wivu na mali za ndugu zao huku wengine wakidiriki hata kuua ili waweze kupata mali za ndugu zao.

Malezi mabovu kwa watoto
Familia nyingi zimekosa malezi bora kwa watoto wao kutokana na ubize wa majukumu mbalimbali , hivyo wazazi wanakosa muda wakutosha kujua mienendo ya watoto wao na mwishoe kukosa maaadili na kukuwa katika tabia zisizo kubalika ndani ya jamii kama ukatili.


ZIFUATAZO NI NJIA ZA KUPUNGUZA NA KUTOKOMEZA UKATILI KATI YA NDUGU, WAPENZI NA WATU WA KARIBU NDANI YA JAMII

Ngazi ya familia


Malezi bora katika familiya na kudumisha upendo miongoni mwa wanajamii
Famila ni sehemu muhimu inayoweza kudhibiti tabia ya za watu tangu wanapoanza kukua na kuwajenga kimaadili sambamba na kudumisha undugu na upendo baina ya wanafamilia na wanajamii kiujumla husaidia kudumisha amani na kupunguza ukatili ndani ya jamii.

Ngazi ya Serikali
Utungaji na usimamiaji wa sheria na sera za kukemea ukatili
Serikali inajukumu la kutunga sheria na kutoa elimu juu ya sheria na sera mbalimbali dhidi ya ukatili ndani ya jamii, njia mbali mbali zaweza kutumika kama njia za semina, harambee na kampeni mbalimbali za kupinga ukatili pamoja na utoaji adhabu kwa wale wanao vunja sheria elekezi.

Ngazi ya Dini
Utoaji wa ushauri nasaha kwa wanajamii
Viongozi wa dini wanakazi ya kutoa ushauri nasaha kwa wanajamii waendelee kuishi kwa misingi ya kidini na imani na kufata matendo mema kama maandiko matakatifu yanavyo tuagiza ili kuondokana na ukatili baina ya wanajamii.


Hitimisho
Kila mwanajamii anajukumu la kudumisha amani, upendo na umoja kwa kushirikiana na serikali katika kupambana dhidi ya ukatili ndani ya jamii kwa maendeleo ya taifa letu
 
Back
Top Bottom