Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kwani hiyo ni safari ya kichama?
Yaani hadi msibani uende na sare za chama? Huu ni mwanzo wa kuleta utata, fikiria vyama vyote wafike wamevalia sare zao si tayari tutakuwa kama kipindi cha kampeni!

Yaani huu nao ni utumwa sasa.
 
Hapa wengi mnapiga siasa tu, na huenda hakuna hana mtu aliepoteza ndugu.
Hebu jiulizeni kwann hao wataalam walisema zoezi lisitiswe?
 
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
Mkuu umenena vyema
 
Tanzania Editors Forum Zanaki Street Plot No. 2285/7, Opp. CCM Office Mtendeni Branch
P.O.Box 75206 Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 22 123236 Mob: +255 715 339090, +255 713 488269
E-mail: tanzaniaeditorsforum2008@gmail.com
Septemba 23, 2018
Salamu za pole ajali ya MV Nyerere
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepokea kwa mshituko mkubwa, taarifa za
kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kinatoka Bugolora kwenda
Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza, Septemba 21, mwaka huu. Hadi sasa
taarifa zilizopo ni kuwa zaidi ya watu 200 wamepoteza maisha katika ajali hiyo.
Ajali hii inarejesha kumbukumbu mbaya kwa Watanzania kwani inawakumbusha
ajali za MV Bukoba (1996) katika Ziwa Victoria ambako watu zaidi ya 800 walipoteza
maisha, MV Spice Islander (2011) katika bahari ya Hindi, ambako zaidi ya watu 200,
walipoteza maisha, huku MV Skagit nayo ikizama kwenye bahari hiyo hiyo na
kupoteza maisha ya watu karibu 150 mwaka 2012.
TEF inatoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. John
Pombe Magufuli, familia za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki.
Tunafikiri wakati umefika wa Tanzania kuzuia kuendelea kushuhudia majanga kama
haya ambayo kwa hakika yanataka kugeuka kuwa utamaduni wa uendeshaji wa
vyombo vya majini nchini.
Tunaisihi Serikali, wananchi na wadau mbalimbali kuongeza elimu ya udhibiti wa
majanga, huku tukijenga utamaduni wa kuheshimu sheria, kanuni na taratibu
zilizowekwa kwa usalama wa abiria.
Tunaamini utafanyika uchunguzi wa kina na waliohusika na uzembe huu uliogharimu
maisha ya Watanzania watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Tunaomba katika kipindi hiki kigumu tuwe na utulivu, tuendeleze umoja na
mshikamano wa Watanzania, huku tukivisihi vyombo vya Dola vinavyofanya
uchunguzi kuharakisha uchunguzi na kuwatendea haki waliohusika kwa mujibu wa
sheria.
Tunaomba Mungu awape nafuu manusura waliojeruhiwa na pumziko la milele
Watanzania wenzetu waliopoteza maisha. Amina.
Deodatus Balile
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Balile asante kwa tamko hili
P
 
Ungekuwa wewe ungewalazimisha divers
Etwege naheahimu sana mawazo yako, lakini naomba ujue kitu kimoja, na kabla ya hapo hebu pitia clip ya waziri wa sheria alipoongelea askari na viapo vyao. Divers ni jeshi la uokozi, na wameapa kufa kama alivyosema waziri,hivi unataka tuwe na askari wanaoona mapambano yamekewa makali wanarudi nyumbani mpaka adui aondoke? Hoja ya divers kufa inatoka wapi hapa? Diver (askari) kufa kwa ajili ya kuokoa ndugu zake ni haki na ushujaa. Tuache kuhalalisha uzembe kwa sababu za kisiasa. Nadhani umenielewa.
Acha nikae kimya ni Majonzi.
 
Wakati Mungu anamuamrisha Nabii Nuhu ajenge boti kubwa lenye uwezo wa kubeeba viumbe na baadhii ya binadamu nadhani nuhu mwenyewe alijua mawazo ya munguni huwa hayana makosa,na kweli safari ilikuwa salama salimini.

Sasa ngoja uyasikie ya SUMATRA hawa jamaa walipopewa mamlaka ya kudhibiti chombo hicho chicho ndio unasikia vilio kila teo ni kwa nini chombo kilichopendekezwa kubeba kizazi cha watu wema ambacho katika maoni yangu ndio chombo salama muliko vyote SUMATRA wazembee kiasi hicho.

Kama SUMATRA wangelipewa jukumu la SAFINA si wangemgomea NUHU kwamba "Mzee hapandi mnyama yoyote hapa tunaijaza hii boti na mapipa ya mvinyo kwanza halafu ndio hivyo vinyama vya mwitu vitakuja juu yake"
religion-bird-woodpecker-ark-noah-noahs_ark-sea0817_low.jpg

SUMATRA WANGEPEWA KAZI YA KUISIMAMIA SAFINA MAMBO YANGEKUWA HIVI.
 
Copy and Paste

Tarehe 25 March 2016, huko Watchet, West Beach, Laguna, California.

COASTGUARDS, boti za uokoaji (lifeboats) mbili, paramedics (watoa huduma ya kwanza) pamoja na chopa (helicopter) zilihusika katika usiku wa kuvutia, kwa zaidi ya masaa sita wakati wa kuokoa baharia mmoja ambaye MASHUA yake ilipigwa na mawimbi mazito na kukosa uelekeo na kuzama.
Baharia huyu mzoefu sana, umri wa kati alikuwa akiendesha chombo hicho kutoka Penarth kwenda Watchet usiku wa Jumamosi tarehe 25/03/2016 kwenye mashua yake ya rangi ya blue 25ft fin-keeled, wakati 'injini' ilipogoma kufanya kazi.
Shuhuda wa tukio akatoa taarifa kwa haraka, baada ya kuona mashua ikipigwa na upepo wa Kaskazini Mashariki (North~easterly wind) kupelekwa kwenye miamba kutoka kwenye ukanda wa West Street Beach.

Shuhuda wa tukio hilo anaitwa Jeff Bourne, akatoa taarifa kwa LAPD (Los Angeles Police Department) wao wakafika na chopa, paramedics, na lifeboats mbili kwa ajili ya 'kuokoa mtu mmoja' walitumia saa sita kumtafuta, kumpata na kumuokoa (kama inavyoonekana pichani).
Tarehe 20 September 2018, Bugolora, Ukerewe, Mwanza, Tanzania.

Kivuko cha Mv.Nyerere chenye kufanya safari zake Bugorora hadi Ukara, kupitia Ziwa Victoria, kinazama majira ya saa 10 jioni just mita 100 tu kabla ya kufika ufukweni. Boti za wavuvi zinajaribu kuokoa watu kwa njia za jadi. Wavuvi hawana nyenzo wala hawana skills za uokoaji lakini wanajitahidi kuokoa watu karibu 40 wakiwa hai.
Kwa zaidi ya masaa matatu serikali haijachukua hatua yoyote zaidi ya kuangalia wavuvi wanavyozamia kuokoa manusura. Hakuna helcopter, hakuna boti za uokoaji, hakuna vikosi maalumu vya uokoaji, hakuna life jackets, hakuna paramedics, hakuna lifeboats. Kitu pekee kilichokuwepo ni mashangingi ya mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya, ambao wamesimama kando ya ziwa wakiangalia wavuvi wanavyohangaika kuokoa waliozama.

Saa 2 usiku Mkuu wa mkoa wa Mwanza anazuia zoezi la uokoaji lisiendelee kwa sababu "GIZA" limetanda. Yani alishindwa kabisa kufikiri kuhusu kuleta 'chopa' imulike eneo la tukio uokoaji uendelee? Labda tungeokoa watu wengi zaidi.
Kwamba hata kufikiri kuhusu kutafuta msaada wa haraka wa kununua spotlights zenye watts 1500~2000 ilishindikana? Au hata kuongeza Jenereta la KV 7 ili 'uokoaji' uendelee alishindwa? Kwamba kwa uwezo wake wa kufikiri aliona heri watu waendelee kufa aje kuokota maiti asubuhi, kuliko kutafuta alternative ya mwanga usiku? Hizi ndio akili za viongozi wetu? Na bado yupo ofisini hadi sasa?

Hivi huko ziwani Askari wa maliasili wanatumia boats gani kwenye ulinzi dhidi ya wavuvi haramu? Kwanini hizo boti hazikuitwa kusaidia uokoaji?
Kweli jeshi la polisi hakuna chopa? Kamandi ya JWTZ huko Lake zone pia haikuwa na helcopter? Mwanza nzima hakuna huduma ya rescue inayotumia chopa? Kwamba tulikosa Mwanga kabisa wa kumulika eneo la tukio? The best option tukaona ni kuhairisha zoezi, tukalale, tuamke asubuhi tuje kuokota maiti? Seriously?
Fidel Castro wakati wa jaribio la mapinduzi ya kumuondoa Dikteta Fulgencio Batista madarakani, mmoja kati ya wapiganaji wenzake alizama kwenye maji, safari ya kwenda Sierra Maestra ilihairishwa ili 'mpiganaji' huyo atafutwe na apatikane.
Mwandishi wa vitabu, Muingereza George Orwell alipata kusema "All human beings are equal but some are more equal than others" kwa tafsiri isiyo rasmi Orwell alimaanisha; Binadamu wote ni sawa lakini kuna ambao ni sawa zaidi kuliko wengine"
Hebu jiulize huko kwenye kivuko kungelikuwa na mtoto wa Rais, Waziri Mkuu, au IGP je huyo mkuu wa mkoa angetoa amri ya kusitisha zoezi la uokoaji kwa sababu ya giza? Au lets assume mtoto wake mwenyewe angekuwa huko, je angeruhusu watu kwenda kulala ili asubuhi aje kuokota maiti ya mwanae? Amin, amin nawaambia mtoto wa Mongela angekuwepo kwenye kivuko asingekubali kwenda kulala aje kuokota maiti ya mwanae asubuhi. He could fight to infinity because he believe to be more equal than others. Hivi ndivyo viongozi wetu walivyojengwa.

Hii inatufundisha nini? Marekani na nchi zilizoendelea uhai wa mtu mmoja ni muhimu kuliko jambo lolote. Wanathamini utu wa kila mtu bila kujalisha ni kiongozi au sio kiongozi, ni maarufu au sio maarufu, ni mzee au kijana. Kwao utu kwanza. Ndio maana wapo tayari kukesha ndani ya maji kutafuta mtu mmoja aliyepotea baharini na kumuokoa akiwa hai, bila kujalisha wametumia gharama kiasi gani.

Lakini hapa Tanzania thamani ya mtu inategemea yeye ni nani? ni wa chama gani? ana undugu na kiongozi gani? Hujawahi kuona watu wanabaguliwa kwa sababu ya chama? Hujawahi kuona watu wananyimwa fursa fulani kwa sababu hawana ndugu zao ambao ni viongozi? Hivi ndivyo jamii yetu ilivyojengwa. Ndio maana Mongela alipoona hakuna kiongozi yeyote kwenye hicho kivuko, wala hakuna mtoto wa Rais, PM, waziri au viongozi wengine wakubwa akaamua waokoaji waende kulala, watakuja kuokota maiti asubuhi.
Lakini asingepata usingizi kama kungekuwa na mtoto wa kiongozi mkubwa kwenye hicho kivuko. Wala asingethubutu kusimamisha zoezi la uokoaji. Angepambana zipatikane helicopter za kumulika hata kama ni za kukodi. Angepambana kupata boti za uokoaji, angepambana kupata life jackets za kuwarushia manusura. He could do anything save lives. Hapa sasa ndipo utamuelewa George Orwell aliposema "All human beings are equal but some are more equal than others"
Miaka 22 baada ya Mv.Bukoba tumejifunza nini?
CREDIT. Ninja

Citation

FB_IMG_15376917214067900.jpeg
 
Back
Top Bottom