Basi la MOA lazama baharini wakati linatoka kwenye kivuko cha MV Tanga

wakukurupuka1

JF-Expert Member
Feb 17, 2023
525
1,182
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Tanga kwenda kipumbwi limezama wakati likiwa ndani ya kivuko cha bweni kinachotumika kuvusha watu na magari katika mto mudu.

Hakuna madhara kwa abiria sababu wote walikua nje ya basi ilo.

===

Ufafanuzi zaidi
Basi la Kampuni ya MOA linalofanya safari zake kutoka Tanga kupitia Pangani na kuvuka kwenye kivuko hadi Kipumbwi limezama wakati linatoka ndani ya kivuko cha MV Tanga ambacho kilikuwa kimefika mwisho wa safari eneo la feri ya Kipumbwi kikitokea Pangani.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Zainab Abdallah ambaye amefika eneo la tukio amesema hakuna aliyepoteza maisha wala Majeruhi kwenye ajali hiyo kwakuwa Abiria walikuwa wameshuka na kukaa ndani ya kivuko kama ilivyo kanuni za vivuko siku zote ambapo kwenye Basi alibaki Dereva pekee yake ambaye hata hivyo aliwahi kuruka wakati Basi lilipofeli breki na kutumbukia majini.

Kwa sasa juhudi za kulitoa gari hilo ndani ya maji zinaendelea kufanyika.

View attachment 2697081
 
IMG_8103.jpeg
 
Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Tanga kwenda kipumbwi limezama wakati likiwa ndani ya kivuko cha bweni kinachotumika kuvusha watu na magari katika mto mudu.

Hakuna madhara kwa abiria sababu wote walikua nje ya basi ilo.

===

Ufafanuzi zaidi
Safi sana. Habari njema na nzuri hamna madhara kwa abiria.
 
wakukurupuka1 kuna ajali nyingi zinaendelea kutokea ila haujatujuza.
Tunaomba uendelee kutujuza habari za ajali maana wewe ndiye reporter mkuu wa ajali zote Tanganyika
 
Back
Top Bottom