Timu ya uongozi wa CCM yenye wajumbe sita inayoongozwa na Kanali mstaafu Ngemela Lubinga na Ndg. Humphrey Polepole ambao ni wakuu wa idara za CCM Makao Makuu na katibu wa UVCCM Taifa Mwl Raymond Stephen Mwangwala, tayari imewasili na kuweka kambi mkoani Mwanza wilaya ya Ukerewe katika kisiwa cha Ukara ili kuhakikisha mambo yote yanayoendelea kusimamiwa na Serikali yanakwenda vizuri ikiwa ni pamoja na kuhakikisha majeruhi wanapatiwa matibabu ya haraka pamoja na wale wote ambao wamepoteza maisha kuhakikisha kuna kuwepo na utaratibu mzuri wa kuwasitiri na kuwahifadhi.
#WapumzikeKwaAmani #PoleTanzania
#WapumzikeKwaAmani #PoleTanzania