Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara Kufungua Fursa Mafia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUFUNGUA FURSA MAFIA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuifungua wilaya ya Mafia kwa kujenga miundombinu bora ya barabara ili kuchochea fursa za kiuchumi, Utalii na Uwekezaji.

Bashungwa amesema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wananchi wa Kirongwe Wilayani Mafia katika ziara yake ya Kikazi ya kukagua hali ya miundombinu ya barabara pamoja na utendaji wa Kivuko cha MV Kilindoni kinachotoa huduma kati ya Nyamisati – Mafia.

Bashungwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kwa Wizara ya Ujenzi kuanza taratibu za kumpata Mkandarasi atakayejenga barabara ya Kilindoni – Rasmkumbi (km 52.28) kipande kilichobakia cha kilometa 50 kwa kiwango cha lami baada ya kukamilisha ujenzi wa kipande cha Kilindoni – Kigamboni (km 2.1)

“Kwa sababu ya jiografia ya Mafia, barabara ya Kilindoni – Rasmkumbi tukiijenga vipande vipande haitaleta tija na kutakuwa na gharama zaidi kutokana na namna ya kupata vifaa vya majenzi, hivyo ni lazima tulete Mkandarasi mmoja ili akiianza barabara hii abaki huku huku Mafia mpaka barabara hii ikamilike”, amefafanua Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amemuelekeza Meneja wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Pwani kuikarabati barabara ya kutoka Bungu hadi Nyamisati (km 40) kwa kiwango cha changarawe ili iweze kupitika wakati wa mvua na kiangazi.

“Kwa maboresho tunayoyafanya kwenye kivuko cha MV Kilindoni lazima utoaji huduma wa kivuko uendane na mwasiliano mazuri ya barabara”, amesisitiza Bashungwa.

Hatahivyo, Bashungwa ameahidi kusimamia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kivuko kingine ili kuleta tija kwa wananchi wa Mafia kupata huduma bora za usafiri na usafirishaji.

Naye, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ambaye pia nia Mbunge jimbo la Mafia Mhe. Omary Kipanga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kukiona kisiwa cha Mafia na kuleta fedha za miradi mbalimbali ambazo zimeboresha huduma kwa wananchi wake.

Vilevile, Kipanga amekipongeza Chama cha Mapinduzi kwa kusimamia utekelezaji wa ahadi zilizomo kwenye Ilani ya Chama ambapo hadi sasa zimeweza kutekelezwa kwa asilimia 95.
 

Attachments

  • UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KUFUNGUA FURSA MAFIA.mp4
    78.4 MB
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.16.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.16.jpeg
    300.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.17.jpeg
    191.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.18.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.18.jpeg
    366.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.18(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.18(1).jpeg
    399.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.19.jpeg
    577.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.20.jpeg
    341.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.21.jpeg
    278 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.22.jpeg
    545.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.23.jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.23.jpeg
    743.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.23(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-03-23 at 12.47.23(1).jpeg
    516.2 KB · Views: 4
Kunahitajika barabara ya kuunganisha wilaya za mkoa wa Pwani badala ya kutegemewa za Dar esalaam
 
Back
Top Bottom