Ujumbe wa Masogange aliouandika ukurasa wa twitter

Ujumbe wa Masogange aliouandika ukurasa wa twitter

hii haiwezi kuniaminisha kuwa yuko huru,mkumbuke huyu mdada hata habari za kukamatwa kwake zilivotoka katika kurasa wake wa twter ilionekana niuongo alijionyesha akichat na mpenzi wake na akamuaminisha kuwa sio yeye aliye kamatwa..naami hizi habari na account zinatumiwa na jamaa zake wa hapa bongo kutuhadaa wabongo na kututuliza tusiamini hivyo.

Zikomo maningi
 
Awaahidi waTz kama hatarudia tena 7bu hata Mungu mwenyewe hapendi
 
Si nimesoma habari kwamba wamenyimwa dhamana mpaka Novemba tena? Hata akitoka lakini siri imeshafichuka na tumeshajua nyendo zake na ninadhani kwa hii itakuwa fundisho hatorudia tena kubeba sembe kupeleka nchi za nje labda sasa abadilishe biashara. Tena asithubutu kwenda china kule hawapindishi mambo hata kama wewe ni mtoto wa raisi wa dunia.
 
Sitashangaa siku akirejea home, Watanzania kadhaa, wakiongozwa na Waandishi wa Habari na Wapiga Picha za Matukio watakuwepo Airport kumpokea kama Shujaa wa Taifa! Atapewa shada la maua na kufunguliwa mlango wa gari na kuongozwa na msafara wa magari! Masaa machache na siku chache zinazofuata atafanya "interview" na Vituo vya TV na atapata prime time!

It makes me sick!

Umesahau mkuu ! Atapitia VIP
 
kwa utaratibu huu vita dhidi dawa za kulvya haiwez kuisha,na sijui ni mungu gani huyo wanaemtaja
 
Hivi wana shida gani hao wasichana hadi wajishughulishe na hiyo biashara haramu?

Hakuna shughuli ingine wanayoweza kufanya?

Mkuu zipi? kama ajira zimeota mbawa wafanyaje? Shughuli zingine zipi zitawaingizia mabilioni na wanataka kuishi high class life?
Lawama bado naiangushia serikali. Those are innocents, wamekosa baba wa kuwaelekeza nini cha kufanya. Familia ikikosa father figure inapoteza muelekeo always.
Taifa letu limekosa a father figure, ndiyo sababu vijana wetu wanaangamia.
 
Si nimesoma habari kwamba wamenyimwa dhamana mpaka Novemba tena? Hata akitoka lakini siri imeshafichuka na tumeshajua nyendo zake na ninadhani kwa hii itakuwa fundisho hatorudia tena kubeba sembe kupeleka nchi za nje labda sasa abadilishe biashara. Tena asithubutu kwenda china kule hawapindishi mambo hata kama wewe ni mtoto wa raisi wa dunia.

hii yaweza kuwa kweli,i also believe that.
 
Hili swala linaniaminisha kuwa wacheza na biashara ni watu wa kubwa mno kifuedha hapa nchini.
 
Vita hii ya Madawa ya kulevya Tanzania, haitafika popote...Waziri wa uchukuzi alijitahidi kuongea juu ya kupitishwa Madawa ya kulevya uwanja wa ndege Wa Julias Nyerere na kuchukua hatua kwa wahusika waliofanikisha kupitisha Mzigo wa dawa za kulevya uliokamatwa na wakina Masogange South Africa kwa kufukuzwa kazi na kushtakiwa lakini cha kushangaza Waziri wa Mambo ya ndani hakuongea wala kutoa taadhari na hatua za kuchukua dhidi ya Makundi haya yanayohusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho nimeamini biashara hii ni yaviongozi wakubwa serikalini wakiwamo Wanasiasa na familia zao.

akiachiwa itabidi mwakyembe awarudishe kazini wale wote aliowafukuza tena awalipe mishahara waliyoikosa na marupurupu na fidia ya usumbufu.
 
Si kweli bado yuko ndani.......

ataachiwa siku za karibuni, mpango uliosukwa ili waachiwe ulishajulikana kitambo, na pia ufahamu kuwa serikali ya south africa pia ni corrupt haipo perfect kama watanzania wengi wanavyofikiri.
 
Huyu mungu anasingiziwa mengi sana. Mhurumieni jamani.

Sembe muuze wenyewe kwa swagger zote halafu mkikamatwa hamwishi kumtaja mungu.

Dhana ya uwepo wa Mungu ni kwa ajili ya watenda maovu haijalishi aina ya uovu, kwa maana kusingekuwapo hayo maovu huo wema usingalitambulika mkuu, Pia Mungu yupo kwa ajili ya watenda maovu.... wamjue kisha wamfuate ndio maana huyu Agnes ameanza kwa kumtambua Mungu wake baada ya kutambua uovu wake....
 
IMG-20130918-WA0039.jpg


I hope this is NOT true. Yaani huyu demu kweli ana akili timamu? Kuua na kuharibu watoto wa watu kote miaka yote hii bado tu anaomba Mungu? Mungu kweli hutotenda mema kusikiliza maombi ya muuaji viumbe wako, it is NOT fair and this is where namuunga mkono Cosmas Chidumule kwenye wimbo wake wa "Rufaa Ya Kifo," ulioimbwa na Marijan Rajab kwani nami nakata rufaa ya muuaji kuachiliwa huru.
 
Back
Top Bottom