Ujumbe wa Masogange aliouandika ukurasa wa twitter

Ujumbe wa Masogange aliouandika ukurasa wa twitter

Vita hii ya Madawa ya kulevya Tanzania, haitafika popote...Waziri wa uchukuzi alijitahidi kuongea juu ya kupitishwa Madawa ya kulevya uwanja wa ndege Wa Julias Nyerere na kuchukua hatua kwa wahusika waliofanikisha kupitisha Mzigo wa dawa za kulevya uliokamatwa na wakina Masogange South Africa kwa kufukuzwa kazi na kushtakiwa lakini cha kushangaza Waziri wa Mambo ya ndani hakuongea wala kutoa taadhari na hatua za kuchukua dhidi ya Makundi haya yanayohusika na biashara ya Madawa ya kulevya kitu ambacho nimeamini biashara hii ni yaviongozi wakubwa serikalini wakiwamo Wanasiasa na familia zao.
 
Sitashangaa siku akirejea home, Watanzania kadhaa, wakiongozwa na Waandishi wa Habari na Wapiga Picha za Matukio watakuwepo Airport kumpokea kama Shujaa wa Taifa! Atapewa shada la maua na kufunguliwa mlango wa gari na kuongozwa na msafara wa magari! Masaa machache na siku chache zinazofuata atafanya "interview" na Vituo vya TV na atapata prime time!

It makes me sick!
 
Akirudi wampe nabendera yanchi basi' si balozi wao!! Amewawakilisha vema...
Poor tz..
 
Uyo mungu aliemsaidia kusafirisha ngada ndo uyo uyo wa mbinguni, majanga!
 
Hivi wana shida gani hao wasichana hadi wajishughulishe na hiyo biashara haramu?

Hakuna shughuli ingine wanayoweza kufanya?
 
Hapo ndo utajua mungu story tu.

Mungu ana sense ya justice iliyo lower than polisi wa Mrema?

Mimi wala sijashangaa kama anamshukuru mungu kwa kusikiliza na kujibu maombi yake. Dunia hii ina miungu wengi sana na huyo anayemshukuru ni mmoja wao.

Ningeshangazwa sana kama angesema anamshukuru Mungu kwakuwa siamini kwamba Mungu anaweza kushirikishwa kaatika biashara ya kusafirisha sembe.
 
Huyu mungu anasingiziwa mengi sana. Mhurumieni jamani.

Sembe muuze wenyewe kwa swagger zote halafu mkikamatwa hamwishi kumtaja mungu.

Oooops, Does He exist?!!!! Weird darwinic fallacy.
 
Mungu humsikiliza kila kiumbe wake. Hopely umelia sana na kasikia kilio chako. Njoo kwangu sasa tuanzishe familia mama. Wewe mzuuri sana ila uachane na Mama Rwakatale atakuangamiza next time.
 
Halafu huyo "mungu" aliyekuwa naye wakati wote na kumsaidia ili afanikishe deal la madawa ya kulevy ni hovyo kabisa.

Mkuu uko sahihi kabisa hilo linaitwa li shetani kabisaaaaaaaaaa lifanyabishara likuu la madawa ya kulevya
 
Jamani mbona yuko sawa kumshukuru mungu wake na sio Mungu....

Kumbukeni kuna "Mungu" na mungu....

Ndio maana na kwenye kutoa shukran nyingine kasisitiza kwa kidhungu "god" na sio "God"

Hivyo basi tusishangae yeye kumshukuru mungu / god......

baelezee baelewe.. Watu hawajui kuwa shetani naye ni mungu
 
Kweli Mungu ni wa ajabu,ona kama wauza madawa nao wanaoharibu watoto wa watu,nao wanaomba mungu waachiwe huru na wanaachiwa regardless wame cause damage ya kiasi gani,mmh kazi kweli kweli.

Si huyo Mungu unayedhania kuwa unamjua aliyemsaidia. Kuna miungu wengi tu, Ukibahatika ukasoma Biblia, fungua kitabu cha 2 Wakorintho 4 : 4, unasema; mungu wa dunia hii aliwapofusha mioyo. Si kwamba mwandishi alikosea kumwandika huyo mungu kwa herufi ndogo. Huyu naye ni mungu. Huenda ndiye mtu wako alimwomba. Mali ya 6.8 billion! Ogopa. Ukianza kuzihesabu kwa mkono utazeeka halafu utasahau ulianza lini. Sa asitokee mungu kumsaidia? Hiyo ni zaidi ya bajeti ya baadhi ya wizara hapa.
Usiogope, Mungu wa kweli hatawaacha hao wanaowaharibu watoto wetu wakwepe kila siku. We have a living God whom we fear. He will do something one day. Utasema ni ndoto zangu lakini nitaishi nizione sikitokea kweli.
 
Uwe na dini usiwe na dini, Miungu ipo mingi wengine tunamuabudu Mungu katika jina la Yesu Kristo wa Nazareti, wengine Mungu katika jina la Mtume Muhamad wengine Mungu katika jina la nyoka, Ngo'mbe, jiwe, moto na kadhalika. Kwa hiyo kila mtu anasaidiwa na Mungu wake. Ila mimi naamini na kuona kwa macho kwamba Mungu wangu ana nguvu kuliko wote.

Mimi sina dini wala siamini katika mungu.

Kama sitaki kufungwa kwa kesi ya madawa ya kulevya, sijiingizi katika kubeba madawa ya kulevya. Wala sitahitaji kumuomba mungu ili anitoe kwenye kesi ya madawa ya kulevya, kwani matendo yangu ni zaidi ya sala ya kumuomba mungu anitoe kwenye kesi ya madawa ya kulevya.

Action speaks louder than words, your very actions are your prayers. Wengine wanaomba wapate kesi kwa matendo, wakishikwa haweshi kuomba waachiwe.

Mungu hayupo, shetani hayupo. Waswahili wanasema "Ibilisi wa mtu ni mtu".Na mimi naongeza "Mungu wa mtu ni mtu".
 
Kwan kuna twitter new version???????uwiiiiiiiiiiiiiii

Sijui party ya kumpongeza ni wapi mana ndo mambo yetu wabongo
 
Mimi wala sijashangaa kama anamshukuru mungu kwa kusikiliza na kujibu maombi yake. Dunia hii ina miungu wengi sana na huyo anayemshukuru ni mmoja wao.

Ningeshangazwa sana kama angesema anamshukuru Mungu kwakuwa siamini kwamba Mungu anaweza kushirikishwa kaatika biashara ya kusafirisha sembe.

Mungu alituma Mwanae kwa wenye dhambi, hivyo basi, kama alimwita Mungu ambaye anamwana Yesu na kumwomba Msamaha, what better will you get than freedom?

Biblia inasema kuwa Yesu alikuja kwa wenye dhambi na si wasio na dhambi. 1 Timothy 1: 15Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi.

Huu ndio ushuhuda tosha kuwa, Yesu ni juu ya SHERIA.
 
Back
Top Bottom