Ujumbe kwa wanachuo na wahitimu wanaodharau wenye elimu za chini

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
MUHIMU: Kwa wale baadhi yao wenye tabia hii, sio wote, wapo wanaojiheshimu !

Elimu yangu niliishia form 4, ilinibidi nianze maisha ya kujitegemea kwa kujifunza useremala naoufanya hadi sasa (najikongoja wala siwezi kujisifia nimefanikiwa )

Katika miaka mingi nimeweza ku observe kwamba kua baadhi ya wanachuo na wahitimu hasa wale wenye chini ya miaka miwili baada ya kuhitimu huwa wana prejudice ya kujiona kwamba wapo level ya juu kwasababu tu wamo kwenye mazingira ya kuzisomea degree ama wanazo tayari.

Kwakweli naweza kumuheshimu sana mtu alie elimika maana kwake anajua kwamba hakuna mtu anaejua kila kitu na kila mtu ni mwalimu wa mwenzake na elimu ni chochote utachojifunza hasa chenye kuleta msaada kwako au kwa jamii, hata kama ni kujifunza ufundi cherehani kwake anajua ni elimu, Hawa walioelimika ni ngumu sana kudharau wengine

Tatizo linakuja kwa hawa wengine sasa wasomi wa vyeti, wanachosoma ni cha kwenye syllabus ya mtihani tu, huyu ni msomi na hajaelimika kwasababu hana kiu ya kuelimika kwa kujisomea hata vitabu vya ziada angalau hata biblia ama quran, rich dad poor dad, 40 laws of power, vitabu vya kuishi na watu kama mtu ulieelimika vya dane, n.k. na ninaposema hawa ni wasomi wala sikosei, wakishamaliza masomo yao wakapata vyeti hawaji kusoma chochote, wao wamemamliza hapo!! kwa cha kusoma ni kile cha kujibia mtihani tu hata kam ni kukaririri... Na ndio hawa sasa baadhi yao wapo ambao huwa wanadhani kuwa na cheti ni kuwa na akili za mtu alieelimika, mtu anakuwa very arrogant, sifa kama zote watu wajue ana gamba (cheti), hataki kupokea ushauri wa wale ambao hawajasoma, n.k.

Sitaki kuonekana na wivu ama chuki yoyote kwa wasomi wetu wenye tabia hizi lakini huku mtaani wapo baadhi yao (sio wote) wenye tabia hizo, bila ajira wanatia aibu kwa kumeza jeuri waliyokuwa nayo ya kujimwambafai kwamba wamesoma sana, bila ajira wengi wanachokwa kubebwa nyumbani kwao na inabidi waanze kujipambania na ndio hapo wanapomeza jeuri yao kwa kuanza kuomba ramani za kufanya shughuli za kawaida walizozi dharau kama kuuza kiosk, kuchoma mishkaki, n.k.

Mwisho wa post niseme tu kwamba, Elimu ni muhimu na hakuna anaejua kila kitu, Elimu zinategemeana

Kujifunza upishi ni elimu muhimu hii, bila hii elimu tutaishia kula mapera,

Kujifunza hesabu ni elimu muhimu, ukishindwa huwezi kutoa chenchi

kujifunza kuishi na watu ni elimu, bila hivyo hutaweza kuishi vizuri kwenye jamii hata uwe na phd ya hesabu

kujifunza useremala ni elimu bila hivyo watu watakaa kenye mawe badala ya viti,

kujifunza biblia / korani ni elimu muhimu pia, bila elimu hii watu hawezi jua dhambi na matendo mema.

kujifunza kiingereza ni muhimu, bila hii elimu bu kuoitwa na maudhui na taarifa nyingi muhimu.

Binafsi hata baada ya kufeli form 4 niliendelea kuelimika kwa kujifunza, useremala, kiingereza, coding, driving, bible, n.k. na bado naendelea kujifunza mengi hasa humu jamiiforums,
 
Watu mlioishia la Saba na form four huwa hamjiamin sjui Kwa nn ( mna inferiolity complex Sana ) , kazi kuwananga waliosoma , asa kama umefanikiwa si unyamaze sasa , waliosoma sio kuwa hawafanikiwi ni suala la mda tuu na wao wanakuwa kwenye mstari , mda mwingi wanalost kwenye masomo , so wanachelewa ku_regroup.....!!!
 
Jamii ina unyanyapaa sana. Mtu ukiwa na degree ukarudi mtaani kujifunza cherehani au kuuza genge utaona wanakucheka! Oooh na degree yake yote hiyo anauza genge looooh kumbe bora hata sisi ambao hatukusoma!!! Tena wanakuwa wanakucheka!
Ndo maana watu wanaogopa kujichanganya ila sio kwamba wanadharau kazi!
 
kabla yakuwalaumu wasomi laumu kwanza mfumo unaotengeneza hao wasomi.

tukiendelea kulaumu wasomi huku tukujua kabisa mfumo wa elimu unaotengeneza hao wasomi ndio unamatatizo na wote kwa nguvu yetu tupambane nao ukae sawa baadala ya kuendelea kulaumu wasomi ambao wengi wao ni waathirika tu.
 
Unaweza ukasoma sana pia utadhataulika kama Huna Hela. Mwenye Hela ndio anaongoza kwa dharau Hawa wasomi feki hebu tuwaache maana wasipojisikia kwa kisomo Chao basi Hawana Cha kujisifia wataonekana wapo wapo tu. .

Mie mwenyewe ukikaa vibaya nakuchana kwa sababu nyie ambao hamjaenda shule mnapenda ubishi sana. Juzi hapo nabishana na mtu kuhusu balance diet ananifundisha wakati hajui halafu hataki kujua anatak abak na ubishi wake...

Unakuta jitu halijui alafu linakwambia niache navyokua Mimi inauma sana elimu yangu Nampa Bure kabisa alafu halitaki ..
 
Hivi umenunua gari gani mkuu? Na unamiliki mali zenye thamani ya tzs ngapi?
nina gari ndio lakini hakuna kitu muhimu hapa duniani kumiliki kama akili na afya.

Usije changanya akili na uwezo wa kujibu mtihani wa darasani.
 
Back
Top Bottom