Elimu siyo vyeti!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Nijuavyo, kuna namna mbili za kujifunza:
~ Informational learning!

~ Transformational learning!

INFORMATIONAL LEARNING huhusisha kufundishwa. Ndiyo mfumo unaotumika shuleni.

Lakini TRANSFORMATIONAL LEARNING hutokea kwa jitihada binafsi za mtu. Mara nyingi, matokeo ya maarifa yapatikanayo kwa njia ya transformational learning yana matokeo chanya zaidi kuliko ya informational learning.

Kuna watu ambao hawajasoma katika taasisi za Elimu ya Juu lakini wana uwezo wa kufundisha hata Vyuo Vikuu. Kuna watu ambao hawana vyeti kutoka taasisi za Elimu ya Juu lakini kutokana na uelewa wao, hawawezi kusimangwa na wasomi kwamba hawana Elimu.

Mark Zuckerberg, Anthony Robbins, Bill Gates, Michael Dell, n.k., ingawa hawakuhitimu Vyuo Vikuu, lakini hawajisikii wanyonge wanapokuwa na wasomi wa Vyuo Vikuu.

Hata hapa Tanzania, kuna baadhi ya watu ambao pamoja na kutokuwa na degree za Vyuo Vikuu, matokeo ya kazi zao zimezidi za baadhi ya maprofesa.

Chukulia mfano, Freeman Mbowe. Kama si mshabiki wa kisiasa, utakubaliana nami kuwa ni kati ya Watanzania wenye "akili".

Inasemekana hajasoma Chuo(ingawa sina uhakika), lakini hata kama ndivyo, ni kipi ambacho ameshindwa kukifanya kwa sababu ya kutokuwa na cheti cha Chuo Kikuu?

~ Ni mmoja wa wanasiasa maarufu nchini

~ Ni mfanyabiashara mwenye mafanikio

~ Nasikia pia ni Mwenyekiti mwenza kwingineko huko ...(sijui kama ni Afrika au duniani kote), nafikiri, wa vyama vya kidemokrasia.

~ Si mropokaji. Yupo makini sana katika kuongea

~ Ni jasiri

Elimu si cheti. Bora uwe na Elimu bila cheti kuliko cheti bila maarifa.
 
Back
Top Bottom