Elimu ya juu inakuzwa sana kuliko uhalisia kwenye biashara. Elimu ya form 4 inatosha sana kwenye biashara za Tanzania

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Kwanza kabisa huwa nawashangaa wanaopiga kelele kuhusu mtu asome mpaka chuo ili aweze kufanya biashara wakati wanachuo hao wapo bize kutafuta ajira na wakizipata wanaridhika na mishahara.

Na hata wasomi wanaofanya biashara wengi wao wanafanya biashara hizi hizi wanazofanya watu walioshia darasa la saba na form 4.

Ni nadra sana kuwakuta wafanya biashara wanaotumia elimu zao kwenye biashara, Tuna wahitimu wengi sana wa vyuo vya IT lakini hadi leo bidhaa za IT hapa Tanzania ni chache sana, Tuna wahitimu wengi wa Engineering lakini hadi leo makampuni yanayouza hata gesi za kuchomelea ni ya Wahindi, n.k.

Wenye masters na wenye elimu za form 4 Wengi tunakutana maporini kuchana mbao, kuagiza na kuuza bidhaa masokoni, kujuzana machimbo, n.k.
 
Back
Top Bottom