Uingereza waanza kujilaumu na kushuku kuwa BREXIT ndio mwanzo wa mdororo wa uchumi wake

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,327
24,209
Waziri wa Fedha Uingereza, Chancellor Jeremy Hunt, ameanza kukubali kile waingereza wengi walikuwa wakishuku lakini moyoni wakikikataa, kuwa kujiondoa Umoja wa Ulaya unawapiga kiuchumi kwa sana.

Waziri wa Fedha Uingereza sasa amekaririwa akikubali kuwa kati ya nchi zenye uchumi imara Ulaya, Uingereza peke yake ndio ina mdororo wa uchumi uliopitiliza.

Sababu kubwa ni kuendelea kukosa masoko ambayo zamani yalikuwa yake kabla ya kujitoa Umoja wa Ulaya, BREXIT.

Tukumbuke, Obama aliwahi kuionya Uingereza kuwa itakuwa na uchumi wa mwisho katika Ulaya.

Huu ni muendelezo wa mawazo ya waingereza wengi wanaoamini sasa kujitenga na Ulaya hakukuwa sahihi.
 
Wakati mwingine mamlaka ya nchi, utakiwi kuwasikiliza sana watu wa kipato kidogo. Maana wao wanawaza leo badala ya leo na Kesho. Maisha yanategemeana sana, waingereza hawana kujitegemea hata asilimia 50 ukiilinganisha na USA, ambayo ina asilimia zaidi ya 50 ya kujitegemea ndio maana wanakuwa na uwezo wa kuiadabisha nchi yoyote duniani. Sasa waingereza izi Sera za demokrasia kuwasikiliza sana watu wa kipato kidogo ndio inawaletea shida sana. Mtu asiyekuwa na uhakika wa maisha, akiambiwa ugumu wa maisha unaletwa na wageni, Kesho unawakuta barabarani wanaandamana hatuwataki wageni. Wakiondoka wageni izo kazi hawataki kuzifanya, mfano mzuri hata apa Tanzania, uwezi kuta mtu mwenye elimu anafanya KAZI ya kufagia barabara au anauza bar, lakini mtu kutoka vijijini na sehemu ya mbali na apo alipozaliwa anafanya na anapata icho kidogo na maisha yake yanaenda pia. Ilo ni somo, England kayakanyaga
 
Waziri wa Fedha Uingereza, Jeremy Hunt, ameanza kukubali kile waingereza wengi walikuwa wakishuku lakini moyoni wakikikataa, kuwa kujiondoa Umoja wa Ulaya unawapiga kiuchumi kwa sana.

Waziri wa Fedha Uingereza sasa amekaririwa akikubali kuwa kati ya nchi zenye uchumi imara Ulaya, Uingereza peke yake ndio ina mdororo wa uchumi uliopitiliza.

Sababu kubwa ni kuendelea kukosa masoko ambayo zamani yalikuwa yake kabla ya kujitoa Umoja wa Ulaya, BREXIT.

Tukumbuke, Obama aliwahi kuionya Uingereza kuwa itakuwa na uchumi wa mwisho katika Ulaya.
Hawakuona hasara aliyoleta Jiwe kwa Tanzania kwa kugombana Mara kwa Mara na Kenya?
 
UK walirejea matumizi ya Pound yao na wakaachana na EURO mazima..

Hata hivyo Jamaa walikuwa mguu nje mguu ndani toka EU imeundwa, hawakuwahi kukubali kuachana na Pound moja kwa moja kama walivyofanya wenzao wengine..
Bado imekula kwao.
Sasa Pound na Dollar karibu zinalingana.
Leo £1=1,17$ miaka 30 iliyopita 1£ ilikua around 2,5$.
Hali si shwari huko UK.
 
Miaka 44 iliyopita shilingi ya Tanzania na ya Kenya zilikuwa ngoma droo sasa leo tuambie tofauti ikoje, shilingi 1 ya Kenya ni sawasawa na shilingi 20 za Tanzania.

Tuliharibu uchumi wetu kwa kupigana vita vya kijinga ili Nyerere amrudishe rafiki yake Obote madarakani pamoja na sera za hovyo za kijamaa.
 
Hivi mpaka leo bado tuna hangover ya vita ya Kagera. Inahitaji miaka mingapi kubadili uchumi wa nchi?. Nadhani adui mkubwa wa uchumi wetu ni Ufisaidi na kutokujali:
1. Huduma mbovu ya maji
2. Umeme kukatikakatika
3. Kuachilua rasilimali zetu kuchukuliwa kiholela
Na mengine mengi.
Ukweli hatujapata viongozi wenye maono. Tuache kumsingizia Nyerere. Tuache udhaifu
 
Kila kitu kina hapo mwanzo, sasa unafikiri uchumi wetu ulianzaje kuharibika pamoja na ukweli kwamba ccm imechangia sana na kwa kiasi kikubwa kutofufuka kwa uchumi.
 
Wakati mwingine mamlaka ya nchi, utakiwi kuwasikiliza sana watu wa kipato kidogo. Maana wao wanawaza leo badala ya leo na Kesho. Maisha yanategemeana sana, waingereza hawana kujitegemea hata asilimia 50 ukiilinganisha na USA, ambayo ina asilimia zaidi ya 50 ya kujitegemea ndio maana wanakuwa na uwezo wa kuiadabisha nchi yoyote duniani. Sasa waingereza izi Sera za demokrasia kuwasikiliza sana watu wa kipato kidogo ndio inawaletea shida sana. Mtu asiyekuwa na uhakika wa maisha, akiambiwa ugumu wa maisha unaletwa na wageni, Kesho unawakuta barabarani wanaandamana hatuwataki wageni. Wakiondoka wageni izo kazi hawataki kuzifanya, mfano mzuri hata apa Tanzania, uwezi kuta mtu mwenye elimu anafanya KAZI ya kufagia barabara au anauza bar, lakini mtu kutoka vijijini na sehemu ya mbali na apo alipozaliwa anafanya na anapata icho kidogo na maisha yake yanaenda pia. Ilo ni somo, England kayakanyaga
Tatizo la Uingereza sio watu wa kipato cha chini. Ni tatizo la bourgeois class and the aristocratic elites. Kwanza;
i) Ndio waliong'ang'ania kuendelea na mfumo wa kizamani wa kiutawala wa kifalme
ii) Ndio waliong'ang'ania kubaki na pesa yao ya Pound Sterling wakati wenzao wakiamua kutumia Euro.
iii) Na ndio waliong'ang'ania kutoka kwenye Umoja wa Ulaya wakiohofia kumezwa na Ujerumani.

Kwa maelezo hayo utaona ya kwamba watu wa kipato kidogo hawawezi ku influence mambo hayo.
 
Kila kitu kina hapo mwanzo, sasa unafikiri uchumi wetu ulianzaje kuharibika pamoja na ukweli kwamba ccm imechangia sana na kwa kiasi kikubwa kutofufuka kwa uchumi.
Ni kweli tuache kumsingizia Nyerere.. Mpaka around 2002 chumi hizi mbili za Kenya na Tanzania zilikuwa zinalingana..

Uchumi wa Kenya ulianza kutuacha baada ya Kibaki kupewa nchi na kufanya reforms kubwa, tangia hapo Kenya akaanza kutuacha gizani ambako mpaka sasa bado tupo.
 
Waingereza wa Tandale,mnauchambua zaidi uchumi wa UK kulko uchumi wa nchi yao umekumbwa na nin??na nin kifanyke
 
Ni kweli tuache kumsingizia Nyerere.. Mpaka around 2002 chumi hizi mbili za Kenya na Tanzania zilikuwa zinalingana..

Uchumi wa Kenya ulianza kutuacha baada ya Kibaki kupewa nchi na kufanya reforms kubwa, tangia hapo Kenya akaanza kutuacha gizani ambako mpaka sasa bado tupo.
Sio kweli labda mwaka 1978 ulikuwa hujazaliwa au ulikuwa mtoto mdogo sana. Uchumi wa Tanzania ulianza kuyumba baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977 lkn baada ya vita 1979 ndio ukafa kabisa hadi leo.
 
Tatizo la Uingereza sio watu wa kipato cha chini. Ni tatizo la bourgeois class and the aristocratic elites. Kwanza;
i) Ndio waliong'ang'ania kuendelea na mfumo wa kizamani wa kiutawala wa kifalme
ii) Ndio waliong'ang'ania kubaki na pesa yao ya Pound Sterling wakati wenzao wakiamua kutumia Euro.
iii) Na ndio waliong'ang'ania kutoka kwenye Umoja wa Ulaya wakiohofia kumezwa na Ujerumani.

Kwa maelezo hayo utaona ya kwamba watu wa kipato kidogo hawawezi ku influence mambo hayo.
watu wa chini na wasio na elimu wengi ndiyo waliunga mkono Brexit.
 
Back
Top Bottom