Uingereza yapaswa kuachana na mawazo ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
1684498062713.png

Waziri wa Biashara wa Uingereza Dominic Johnson hivi karibuni alifanya ziara mjini Hong Kong, China, akiwa na lengo la “kuihimiza Uingereza kupata uwekezaji na biashara zaidi”. Hata hivyo, bado hakuacha kufuatilia mambo ya ndani ya Hong Kong, na kudhihirisha kuwa ni vigumu kwa Uingereza kuacha mawazo ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”.

Hivi sasa Uingereza ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya uchumi wake. Mwezi Januari, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilitabiri kuwa uchumi wa Uingereza utashuka kwa asilimia 0.6 mwaka huu, huku Shirika la Goldman Sachs likitabiri kuwa, utapungua kwa asilimia 1.2. Uchumi wa Uingereza unakabiliwa na changamoto mbalimbali zisizoweza kusuluhishwa kirahisi, zikiwemo upungufu wa nishati, mfumuko wa bei, na ukosefu wa uwezo wa kuboresha maisha ya watu. Hii pia ni moja ya sababu kuu zilizoifanya Uingereza kutuma afisa wake wa juu kwenye Hong Kong kuomba ushirikiano.

Johnson alitoa ajenda yake mjini Hong Kong kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, na pia alichapisha makala katika Gazeti la South China Morning Post, akisema anatumai kuimarisha uhusiano wa uwekezaji kati ya Uingereza na Hong Kong wenye thamani ya Paudi bilioni 94 za Kiingereza. Johnsona anafahamu vizuri kwamba Hong Kong ni moja ya vitovu vya kimataifa vya fedha, na kuna nafasi kubwa ya ushirikiano na mkoa huo katika nyanja za fedha, miundombinu, na uhifadhi wa mazingira. Ushirikiano na China unaweza kupunguza mzozo wa kiuchumi nchini Uingereza na kuleta fursa nzuri ya maendeleo, kwani China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Uingereza barani Asia, na Uingereza ni nchi ya pili inayovutia uwekezaji wa China barani Ulaya. Mwaka 2021, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Uingereza ilikuwa dola bilioni 112.6 za Kimarekani.

Hata hivyo mwanasiasa huyu wa Uingereza ambaye alikuja China kutafuta ushirikiano, hakuacha mawazo yake ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”, na kwa mara nyingine tena, aliingilia kati mambo ya ndani ya China. Wakati wa ziara yake mkoani Hong Kong, alisema Uingereza haitakwepa kile kinachoitwa “wajibu wake wa kihistoria” kwa Hong Kong, haitafumbia macho "ukiukwaji wa uhuru" mkoani humo, na kuitaka China kutekeleza “haki za binadamu”.

Hong Kong ina historia ndefu ya kuteseka na utawala wa kikoloni wa Uingereza. Mnamo mwaka 1841, Waingereza walianzisha Vita vya Afyuni dhidi ya China, na kukalia Hong Kong, na kuitawala kwa zaidi ya miaka 150. Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, kutokana na kubadilika kwa nguvu ya kitaifa, Uingereza ililazimika kukubaliana na China kurejesha mamlaka ya utawala wa Hong Kong kwa China mwaka 1997. Hata hivyo, baada ya Hong Kong kurudi kwa China, Uingereza imeshindwa kubadilisha mawazo yake ya kuwa “Bwana wa Kikoloni”, na kuingilia kati mambo ya Hong Kong mara kwa mara.

Kama nchi kubwa zaidi ya zamani ya Kikoloni duniani, Uingereza iliwahi kutawala nchi nyingi karibu katika mabara yote isipokuwa Antaktika. Wakoloni wa Uingereza walipora mali, kutesa watu na kuwaua kikatili wale waliojaribu kuwapinga katika nchi hizo. Sasa ukoloni umeondolewa kwa miaka mingi, lakini badala ya kuomba msamaha kutokana na vitendo viovu vya kikoloni, Uingereza bado inachukulia historia ya ukoloni kama ni fahari yake, na kutaka kuendelea kuwa na ushawishi katika nchi na sehemu ilizotawala kikoloni.

Katika suala la ushirikiano na China, Uingereza inapaswa kuwa na busara ya kujua inachohitaji kufanya, na kuacha kabisa ndoto ya kuendelea kuingilia mambo ya ndani ya China, huku ikitarajia kuzidisha ushirikiano na China.
 
Maelezo mengi lakini yote ni nonsense!

Umesema Hong Kong ina historia ya kiteseka ikiwa chini ya uingereza, duh!! hivi ww unaona watu hatujui vinavyoendelea huko Hong Kong?

Tangu CCP imetia mguu wake Hong Kong na kuanza kuingilia mifumo ya kiuongozi ikiwemo kubadilisha sheria ya kutaka watuhumiwa waweze kwenda kuadhibiwa main land Hong Kong imekuwa hakufai tena.

Yale maandamano makubwa yaliyofanyikaga Hong Kong mwaka 2019, 2020 yalionesha ni kwa jinsi gani wachina wengi hawaipendi selikari isiyo ya uhuru na ya kidemokrasia. Na wanatamani uhuru wao ule waliokuwa nao awali.

Mmeiharibu kabisa siasa nzuri na mfumo Bora wa kidemokrasia wa Hong Kong, mmeingilia na kuvuruga uchumi wa Hong Kong hadi Imepelekea watu kuhama Hong Kong na kuamia nchi za west. Hong Kong tangu ianze kuwa chini ya CCP sio salama tena

Unadai uchumi wa uingereza unayumba, huku ukisahau kielezea jinsi uchumi wenu wa main land China ulivyo kwa sasa. Mnahaha kuzibembeleza nchi za west kuendelea kuwekeza China mkidhani wao hawajitambui, kila siku viongozi wenu wanaimba no de coupling from China because wanajua fika hali za wachina wengi zitakakvyokuwa after de coupling.

Uchumi wa China ni mkubwa lakini ni unafaidisha elites ambao wengi ni wanachama wa CCP, vitu kama Ardhi sio Mali ya umma na ndio maana China malalamiko kwenye local governments watu kuporwa Ardhi zao na selikari ni mengi sana, taasisi na makampuni ya selikari vyote vina sekretari wa CCP maana yake no one is owning anything mfumo wa kikandamizaji usiofaa.

European union wanajadili jinsi ya kuanza kuachana na China, de coupling ikifanyika kwa sehemu kubwa hali za wachina wengi zitakuwa mbaya sana kuliko sasa.

Umedai uingireza inataka kuzidisha ushirikiano na China wakati hivi majuzi tu UK walitaka kuvifungia na kuacha kuvipa fund vyuo vyote vya Confucius vyilivyoko uingereza kwa kusambaza propaganda za CCP ikaanza kuhaha na kutoa vitisho.,

USA imacha kuipa fund Wuhan institute of virology ya China, taasisi nyingi za China zinategemea fund za west na kwasasa zinaanza kufutwa, uone ni kwa jinsi gani decoupling inavyoendelea na itakavyowacost.

ujerumani imerejea kuangalia makubaliano yaliyoingiwa awali juu ya hisa za bandari ya humburg port zinazotakiwa na china na kuzishusha mpaka 24.9% kutoka 35% na hapo bado hawajafikia makubaliano rasmi.

Yaani kila taifa la ulaya saivi linapunguza mahusiano yake ya awali na China.

China imekuwa ya hovyo sana na haina tena freedom of speech wala haiheshimu tena human rights.
 
Hong Kong imekuwa chini ya Uingereza lini na kwa nini Hong kong ilikuwa chini ya Uingereza wakati ni sehemu ya China ?
 
Tangu CCP imetia mguu wake Hong Kong na kuanza kuingilia mifumo ya kiuongozi ikiwemo kubadilisha sheria ya kutaka watuhumiwa waweze kwenda kuadhibiwa main land Hong Kong imekuwa hakufai tena.

Yale maandamano makubwa yaliyofanyikaga Hong Kong mwaka 2019, 2020 yalionesha ni kwa jinsi gani wachina wengi hawaipendi selikari isiyo ya uhuru na ya kidemokrasia. Na wanatamani uhuru wao ule waliokuwa nao awali.
Kabla ya 1997 ni lini HKSAR ilikuwa huru na ya kidemokrasia ?
 
Hii kauli yako inaonesha ukweli kabisa China main land hakuna demokrasia, freedom of speech na respect of human rights.

Nchi yenye watu Billion 1.4 inafanyiwa maamuzi na watu wasiozidi elfu 3
 
Naona una tunga nawe swali lako. baki na swali nililo uliza
Majibu ya swali lako yapo ndani ya majibu ya swali nililokuuliza.

Maandamano ya mwaka 2019/2020 ya Hong Kong yalikuwa yanapinga selikari ya main land China kuimpose sheria na taratibu zake Hong Kong ambazo waHong Kong walijua fika zitakandamiza uhuru wao na Demokrasia Yao.

Mfano mdogo ni juzi tu mchekeshaji wa mainland china Li Haoshi na kampuni yake wamepigwa fine ya $ 1 million na kampuni yake kutakuwa kusitisha show zake zote kisa tu aliitaja PLA kwenye comed yake..

Wachina wengi wanaiona hiyo kama ukandamizaji wa freedom of speech. Mambo kama haya Hong Kong na Taiwan hayapo na ndomana hawaipendi kabisa selikari inayoongozwa na chama cha kidikteta cha CCP.

China with autocratic leadership inaelekea kuwa nchi ya kidikteta very soon na watakaoathirika ni nyinyi wachina wenyewe.
 
Majibu ya swali lako yapo ndani ya majibu ya swali nililokuuliza.

Maandamano ya mwaka 2019/2020 ya Hong Kong yalikuwa yanapinga selikari ya main land China kuimpose sheria na taratibu zake Hong Kong ambazo waHong Kong walijua fika zitakandamiza uhuru wao na Demokrasia Yao.

Mfano mdogo ni juzi tu mchekeshaji wa mainland china Li Haoshi na kampuni yake wamepigwa fine ya $ 1 million na kampuni yake kutakuwa kusitisha show zake zote kisa tu aliitaja PLA kwenye comed yake..

Wachina wengi wanaiona hiyo kama ukandamizaji wa freedom of speech. Mambo kama haya Hong Kong na Taiwan hayapo na ndomana hawaipendi kabisa selikari inayoongozwa na chama cha kidikteta cha CCP.
Maneno mengi bure kabisa, mpaka sasa hujajibu maswali hayo mawili niliyo uliza. vitu usivyo na uelewa navyo achana navyo.
 
We jamaa VP, si nimekujibu hapo, unauliza vitu ambavyo vipo wazi kabisa,

Hong Kong ilikuwa huru na ya kidemokrasia since ilipokabidhiwa kwa selikari ya China na uingereza, walikuwa wanafanya uchaguzi na viongozi walikuwa wanachaguliwa na wananchi, tangia CCP iingilie imepunguza zaidi ya robo tatu ya viti vya wawakilishi wa wananchi na kuachia sehemu ndogo tu ichaguliwe na wananchi sehemu kubwa ya viongozi wanapigishwa na baraza la viongozi na sio wananchi... hii kama sio suppression of democracy ni nn?

Upuuzi huo huo mnataka muupeleke Taiwan halafu manataka watu wawaangalie tu.
 
Hong Kong ilikuwa huru na ya kidemokrasia since ilipokabidhiwa kwa selikari ya China na uingereza, walikuwa wanafanya uchaguzi na viongozi walikuwa wanachaguliwa na wananchi, tangia CCP iingilie imepunguza zaidi ya robo tatu ya viti vya wawakilishi wa wananchi na kuachia sehemu ndogo tu ichaguliwe na wananchi sehemu kubwa ya viongozi wanapigishwa na baraza la viongozi na sio wananchi... hii kama sio suppression of democracy ni nn?
Kama unafahamu HKSAR ilikuwa huru na ya kidemokrasia baada ya kukabidhiwa China sasa hayo maneno yako mengi ya kuikalipia CPC na serikali ya China iliyo ifanya HKSAR kuwa huru na democratic yana faida gani na maana gani.

Au hufahamu HKSAR wakati inakabidhiwa China, China ilikuwa Chini ya serikali na chama gani ?!.
 
Maelezo mengi lakini yote ni nonsense!

Umesema Hong Kong ina historia ya kiteseka ikiwa chini ya uingereza, duh!! hivi ww unaona watu hatujui vinavyoendelea huko Hong Kong?

Tangu CCP imetia mguu wake Hong Kong na kuanza kuingilia mifumo ya kiuongozi ikiwemo kubadilisha sheria ya kutaka watuhumiwa waweze kwenda kuadhibiwa main land Hong Kong imekuwa hakufai tena.

Yale maandamano makubwa yaliyofanyikaga Hong Kong mwaka 2019, 2020 yalionesha ni kwa jinsi gani wachina wengi hawaipendi selikari isiyo ya uhuru na ya kidemokrasia. Na wanatamani uhuru wao ule waliokuwa nao awali.

Mmeiharibu kabisa siasa nzuri na mfumo Bora wa kidemokrasia wa Hong Kong, mmeingilia na kuvuruga uchumi wa Hong Kong hadi Imepelekea watu kuhama Hong Kong na kuamia nchi za west. Hong Kong tangu ianze kuwa chini ya CCP sio salama tena

Unadai uchumi wa uingereza unayumba, huku ukisahau kielezea jinsi uchumi wenu wa main land China ulivyo kwa sasa. Mnahaha kuzibembeleza nchi za west kuendelea kuwekeza China mkidhani wao hawajitambui, kila siku viongozi wenu wanaimba no de coupling from China because wanajua fika hali za wachina wengi zitakakvyokuwa after de coupling.

Uchumi wa China ni mkubwa lakini ni unafaidisha elites ambao wengi ni wanachama wa CCP, vitu kama Ardhi sio Mali ya umma na ndio maana China malalamiko kwenye local governments watu kuporwa Ardhi zao na selikari ni mengi sana, taasisi na makampuni ya selikari vyote vina sekretari wa CCP maana yake no one is owning anything mfumo wa kikandamizaji usiofaa.

European union wanajadili jinsi ya kuanza kuachana na China, de coupling ikifanyika kwa sehemu kubwa hali za wachina wengi zitakuwa mbaya sana kuliko sasa.

Umedai uingireza inataka kuzidisha ushirikiano na China wakati hivi majuzi tu UK walitaka kuvifungia na kuacha kuvipa fund vyuo vyote vya Confucius vyilivyoko uingereza kwa kusambaza propaganda za CCP ikaanza kuhaha na kutoa vitisho.,

USA imacha kuipa fund Wuhan institute of virology ya China, taasisi nyingi za China zinategemea fund za west na kwasasa zinaanza kufutwa, uone ni kwa jinsi gani decoupling inavyoendelea na itakavyowacost.

ujerumani imerejea kuangalia makubaliano yaliyoingiwa awali juu ya hisa za bandari ya humburg port zinazotakiwa na china na kuzishusha mpaka 24.9% kutoka 35% na hapo bado hawajafikia makubaliano rasmi.

Yaani kila taifa la ulaya saivi linapunguza mahusiano yake ya awali na China.

China imekuwa ya hovyo sana na haina tena freedom of speech wala haiheshimu tena human rights.
Decoupling maana yake nini!!
 
Wakati inakabidhiwa makubaliano yalikuwa yanasemaje?
 
Hupendi tu China, Haina demkrasia yes,lakini western wanakimbilia Kila siku kutaka kuwekeza na wamewekeza hasa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom