Mjadala kuhusu Jukwaa la Kodi na Uwekezaji 2024, Ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2024:

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mjadala unaofanyika kwenye Jukwaa la Kodi na Uwekezaji 2024, Ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam, Februari 28, 2024:


MDAU: KUNA UTAMADUNI WA TRA KUTOA BENKI FEDHA ZA WATEJA WAO WENYE MIGOGORO YA KIKODI BILA USHIRIKISHWAJI

Mdau ameshauri mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kuachana utaratibu wa kuchungulia akauti za wateja wao kutokana na sababu mbalimbali za migogoro ya kikodi.

Amesema kuwa kumekuwepo na utaratibu ambao amedai kuwa maafisa wa TRA wamekuwa wakichungulia akauti za wafanyabiashara kuzizuia akauti zao na hata kutoa pesa zilizopo kwenye akauti hizo bila ushirikishwaji.

Mdau huyo, Innocent Mlimakifi ambaye ni mfanyabiashara kutoka mkoani Iringa akichangia mjadala kwenye 'Jukwaa la Kodi na uwekezaji 2024' linaloendelea kwenye ukumbi mikutano wa JNCC leo February 28, 2024 amehoji kama uhalali wa TRA kufanya hivyo unatokana na sheria au taratibu zipi?

Akitoa mfano wa kisa cha aina hiyo amesema kuwa kuna mfanyabiashara mkoani Iringa alikuwa anadaiwa milioni 60 lakini TRA waliingia kwenye akauti yake wakakuta kuna zaidi ya milioni 600 na kwamba fedha zote walizitoa na kuzipeleka hazina, ambapo amedai kuwa mtu huyo mpaka sasa hajapata fedha hizo.

Ambapo ameshauri kuwa kama kuna jambo ambalo linahusisha masuala ya migogoro ya kikodi ni muhimu kuzingatia sheria katika kutafuta utatuzi kuliko kuchukua uamuzi wa kukimbilia kufunga akaunti au kutoa pesa kwenye akaunti jambo ambalo amedai kuwa sio utaratibu rafiki kwa sababu sio shirikishi na hauzingatii haki za mteja.

"Kuwepo na Sheria ambayo inalinda akaunti ya mfanyabiashara au mteja mwenye migogoro na mamlaka ya mapato TRA."ameshauri mfanyabiashara huyo

Kauli mbiu kwenye jukwaa hilo ni "Maboresho ya sera katika uwekezaji, ukusanyaji wa mapato ya ndani na ukuaji wa uchumi jumuishi."

Dkt. KIDA, AANIKA FURSA KWA WABUNIFU WACHANGA
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, ametoa wito kwa Wabunifu wachanga kuchangamkia fursa inayotolewa na Ofisi yake kupitia program ya Funguo.

Dkt. Kida ametaja fursa hiyo aliposhiriki Mdahalo kwenye Jukwaa la Kodi na Uwekezaji linaloendelea Jijini Dar es Salaam.

“Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, kupitia kitengo cha Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji kwa ufadhili wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) tunaendesha tunaprogram ya uwezeshaji (Funguo Programme) ambayo mtekelezaji ni UNDP. Amesema Dkt. Kida

Dkt. Kida amesema kupitia program ya FUNGUO zaidi ya Euro milioni (5), zilitengwa kuwawezesha wabunifu wachanga, na hivyo amewaalika wabunifu hao, kuchangamkia fursa hiyo kupitia taasisi za TIRDO, COSTECH na SIDO na UNDP.

Snapinsta.app_430063024_1470687820548430_1193824736731604999_n_1080.jpg
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Elijah Mwandumbya, akitoa mada kuhusu Mwenendo wa Uchumi duniani na Athari zake kwa Uchumi wa Tanzania, katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji 2024, ambalo limebeba kauli mbiu ya “Maboresho ya Sera katika Uwekezaji, Ukusanyaji wa Mapato ya ndani na ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, linalofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mada hiyo iliongozwa na kujadiliwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo , Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Remidius Ruhinduka na kwa njia ya mtandao ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Mhe. Mbelwa Kairuki na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza.
Snapinsta.app_430355282_958238275373945_553992131240291718_n_1080.jpg


Snapinsta.app_430103437_298871053212238_1555404062398715433_n_1080.jpg
 
Yaan kuna mtu jinsi anavyoanza kuchangia tu unajua huyu ni ludewa aama iringa😀😀😀😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom