Bravo moderator!
Hata hivo usiwashangae sana hawa ndugu zetu, ndivo walivo...ndivo walivo...ndivo walivooooooooo...! Kumbuka, mfa maji hakosi kutapatapa! Japo mwisho wake ni bayana na anaujuwa, nao ni kifo baada ya kubugia maji mengi tena machafu!
Kwa mtindo huu usishangae ukiwasikia wasukuma nao wanakuja na mada kuwa, 'Kambalage ni msukuma' kwa vile alizaliwa na baba wa kisukuma wakati ule mama yake kambalage(Nyerere) alipoachika kwa mzee Burito(baba wa kufikia wa Nyerere) kwa kipindi cha miaka mitatu na akaenda kuishi kwa ndugu zake waliokuwa usukumani wilayani Magu kijiji cha Shigala katika jimbo la Busega kwa mheshimiwa Chegeni, wakati ule wa enzi za mkoloni! Ila kulingana na mila za wazanaki na wakurya ni kwamba, mwanamke akishaolewa na kutolewa mahali halafu akaachika, basi wale watoto wote atakaowazaa nje ya ndoa katika kile kipindi chote alichoachika, wote huwa ni 'watoto halali' wa yule 'mwanaume wa kwanza' (mzee Burito for this case)aliyetoa mahali.
Lakini yote hayo ni upuuzi tu kama huo wa akina KEVO na JMUSHI! Usikubali na wala usisumbuke hata kidogo kuumiza kichwa chako kufikiria huo upuuzi wao usiokuwa na tija yoyote kwa watanzania!
Hata kama Mbowe ni mtoto wa kambalage(Nyerere), so what?!
Hata kama kambalage(Nyerere) ni msukuma kwa vile baba yake mzazi ni msukuma, so what?!
NOTE: Habari hii ya baba msukuma wa Nyerere nimeipata toka kwa mke wangu ambaye ni msukuma wa Mwanza wilayani Magu.