Uhakiki wa Wanachama Chama Kipya Cha Siasa 1993

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,841
30,168
WANACHAMA WA CHAMA KIPYA CHA SIASA WAMEKUJA KUHAKIKIWA NA MSAJILI WA VYAMA ARNAUTOGLO HALL 1993

Asubuhi na mapema tulikuwa tumeshafika Ukumbi wa Arnautoglo tumekuja kuhakikiwa kwa ajili ya chama chetu kipya cha siasa.

Ukumbi huu una historia kubwa sana katika siasa za kudai uhuru wa Tanganyika na katika historia ya Julius Nyerere.

Tarehe 17 April 1953 kwenyw ukumbi huu ndipo Nyerere alikabidhiwa chama cha TAA baada ya ''kumshinda'' Abdul Sykes katika uchaguzi wa kugombea nafasi ya President wa TAA.

Wanachama kutoka sehemu tofauti za Dar-es-Salaam kuanzia Buguruni Kwa Mnyamani, Manzese Uzuri, Tandika, Temeke, Mbagala tumefika tumejikusanya nje ya ukumbi.

Maofisa wa Ofisi ya Msajili wamefika jua limepanda kidogo wametukuta tunawasubiri.

Niko pembeni na camera yangu naangalia yote yaliyoko pale.

Kwa mbali nikamuona Mzee Lumelezi anapita na shughuli zake.

Ukoo wa Lumelezi ni ukoo maarufu sana Dar-es-Salaam.

Mzee Lumelezi, Mzee Mavemba, Ally Sykes hawa wote mchezo mmoja na baba yangu na shule yao Al Jamiatul Islamiyya Muslim School Mwalimu Mkuu Sheikh Juma Mwindadi.

Nikamkimbilia kumwamkia.

Akaitikia salamu yangu lakini nikahisi kama vile anajiuliza hapa pana nini?

Sikusubiri aniulize nikamwambia, "Baba tumesajili chama cha siasa leo tunahakikiwa."

Siku hizo kuwa wewe si mwanachama wa CCM ilionekana kama usaliti vile.

Sasa mimi namtagazia hali ya hatari.

Niliona uso wa mzee wangu ukiporomoka kama vile kusema, "Mtoto ana kiranga huyu."

Mzee Lumelezi kainamisha kichwa chini hasemi kitu.

Tukaagana.

Lakini Mzee Lumelezi si mjinga kayaona yote kwa macho yake.

Kawaona waliotutangulia sisi na ndiyo wao na kashuhudia yote yaliyowafika.

Alikuwa kastaafu kazi City.
Hawakupata chochote TANU ilichowaahidi.

Watoto wao wamesoma sana darasa la la 12 lakini kawaida wanamaliza darasa la saba ndiyo mwisho wao.

Alikuwa kwa ule ukimya wake ananiambia, "Tumeshindwa sisi mtaweza nyie?"

Maofisa wa Msajili wa Vyama Vya Siasa walikuwa hawajaona watu sampuli yetu.

Kwanza tuliokuwa pale umasikini wetu ulionekana dhahir haukujificha.

Nguo zetu zilitutangaza vizuri sina haja ya kusema mengine ila moja.

Sote wanachama tuliokuja kuhakikiwa tulikuwa Waislam watupu.

Nimekuwekeeni picha mfaidi kwani picha inasema maneno 1000 na picha inaonyesha kile jicho kiliona.

Maofisa wa Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kutuangalia wakawa tayari wameshakasirika.

Nyuso zao wamezikunja hawana tabasamu.

Leo naangalia nyuma nacheka na nashangazwa na ule ujasiri wetu kuwa sisi masikini ya Mungu tunasajili chama kije kushindana na Chama Cha Mapinduzi, chama tajiri kilichokuwa na kila kitu achilia mbali kuwa kina serikali.

Kisa cha Daud na Jalut.

Jalut anajivuna kwa nguvu zake na uwezo wake wa kumuua kila aliyethubutu kukabiliananae kwenye uwanja wa mapambano.

Daud alipokuwa anakwenda kumkabili Jalut aliomba dua Allah amthibitishie miguu yake ardhini amkabili Jalut.

Chama chetu kilinyimwa usajili.
Lakini huo haukuwa mwisho wetu.

Tuliyokuja kufanya si tu yalimstaajabisha Mzee Lumelezi bali hata sisi wenyewe.

Nimeweka na picha ya mkutano kwanza wa TANU Ukumbi wa Ghandhi Hindu Mandal mwaka wa 1955.

Fananisha picha hii na picha yetu.

334694252_1614180729102052_5833874265695232266_n.jpg

334709390_1352858755287545_2739443264799295865_n.jpg

330781784_621910456438604_3313645283185321560_n.jpg

334702773_146974518262849_5958340362266701242_n.jpg

331795436_147118884905105_1199791197814951944_n.jpg
 
Tatizo focus ya 1950s na 1993 zilionekana tofauti. Mlifanikiwa badae au ndio ilishindikana kabisa mzee wetu?
 
Tatizo focus ya 1950s na 1993 zilionekana tofauti. Mlifanikiwa badae au ndio ilishindikana kabisa mzee wetu?
Sheiza,
Yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana.
Hali ya siasa Tanzania imebadilika sana.

Angalia uchaguzi Zanzibar chaguzi sita CCM Zanzibar haijawahi kushinda.
Tanganyika uchaguzi wa 2020 hapakuwa na uchaguzi.

Jiulize hali hizi zimesababishwa na nini?
Magomeni Mapipa ninapoishi serikali ya mtaa yote ilikuwa chini ya upinzani.

2020 wagombea wote wa upinzani yalikatwa majina yao.

CCM wakagombea peke yao.
"Wakashinda" viti vyote.

Huwa nikipita ofisi ya serikali ya mtaa nawatania wale vijana wa CCM nawaita, "Viti maalum."

Wao hubakia kucheka.
Wanaujua ukweli.

Zingatia pia kuwa eneo hili wanaishi watu gani.
 
Sasa mzee chama cha siasa kinakuaje na waisalam watupu kwani mlikua manaenda kufungua taasisi nyingine ya kiislam?

Anyway nikupongeze kwa ujasiri wenu pia kuikataa ccm mana msingi wa mattizo ya nchi hii ni hicho chama kilichogeuka kuwa kikundi cha walaghai na mafisadi.
 
Jiwe...
Ilikuwa kama wazee wetu walivyounda African Association 1929 wakajikuta wako wenyewe akina Kleist , Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima...

TANU 1954 ni hivyo pia Mshume Kiyate, Jumbe Tambaza, Mwinjuma Mwinyikambi...
 
Hicho chama ndiyo kile cha AMNUT! Wakati mwingine mkisajili chama cha siasa, mjitahidi kugusa makundi yote katika jamii inayo wazunguka.
 
Muonekano wa chama chenu ulikuwa Kama Baraza la idd, mlichoshindwa kufanya 1993 ACT walikifanikisha baadae
 
Muonekano wa chama chenu ulikuwa Kama Baraza la idd, mlichoshindwa kufanya 1993 ACT walikifanikisha baadae
Msaga...
Mimi nimekwenda mbali zaidi.
Nimeingia kwenye Maktaba yangu ya picha nikaIpata picha ya mkutano wa TANU 1955.

Picha ile ya 1955 ikawa imefanana na picha hiyo ya 1993 kwa kila kitu.
 
Hicho chama ndiyo kile cha AMNUT! Wakati mwingine mkisajili chama cha siasa, mjitahidi kugusa makundi yote katika jamii inayo wazunguka.
Tate...
Huwezi kufananisha AMNUT na vyama hivi.

AMNUT ili uwe mwanachama lazima kwanza uwe Muislam.

Sheria ya wakati ule iliruhusu vyama kama hivi.

Vyama hivi vya sasa Waislam wenyewe bila ya ubaguzi waliona wawe na chama cha siasa ambacho kitasimamia haki sawa.

Hapa ndipo ulipo umuhimu wa maneno yako ya nakundi yote katika jamii.

Hakuna maslahi ya makundi yote Tanzania toka hapo wazee wetu walipoanza kupambana na ukoloni.

Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbele lakini hawakubagua ingawa Uislam ulikuwa na nguvu kubwa katika TANU hadi uhuru unapatikana 1961.

Wakati wa kurejeshwa kwa vyama vingi Waislam wakijitazama hawako popote.

Nini kilitokea?
Jibu lipo hapa.

Waliokuwa ndani ya CCM walikuwa wamefanikuwa pakubwa kiasi hadi kufuta historia ya TANU.

HIli alipata kulionya Sheikh Suleiman Takadir mwaka wa 1958 katika kisa maarufu lakini hakuna anaetaka kifahamike.

Waislam wakajikuta wako nje ya fursa zote za nchi na walioshika fursa hawakuta kugawana.fursa hizo na wengine.

Katika hali hii chama chochote chenye kuungwa mkono na Waislam kiliwajaza hofu kubwa.
 
Kwenye nchi yenye dini mchanganyiko kama hii chama cha siasa kinachoegemea upande wa dini moja kinapaswa kuwa haramu

Yoga,
Muhimu lazima sheria izuie hilo kwani litasababisha mgawanyiko mkubwa sana endapo litaachiwa.

Angalia historia ya TANU.

Viongozi wa TAA walipokuwa sasa wanatafuta kiongozi wa kumkabidhi kuongoza harakati za kudai uhuru baada ya kuunda TANU suala la dini lilipewa kipaumbele.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950 na President wa TAA Dr. Vedasto Kyaruzi alikuwa kaondolewa Dar-es-Salaam na serikali kwa nia ya kuidhoofisha TAA.

Abdul Sykes akawa Act. President na Secretary hadi 1953.

Waingereza wakijua kuwa nia ya TAA ni kugeuzwa kiwe chama cha siasa kamili Tanganyika idai uhuru wake.

Abdul Sykes hakuitaka nafasi ya TAA President kisha waunde TANU.

Hakuitaka nafasi ile kwa kuwa alijua nafasi ya President wa TANU ilihitaji Mkristo ili kuondoa fikra ya kuwa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika ni jambo linalosukumwa na Waislam peke yao.

Wakati ule Waislam ndiyo walikuwa mstari wa mbele katika TAA.

Ingekuwa wepesi kwa Waingereza kuwashawishi Wakristo kuunda chama chao ili wasimezwe na Waislam.

Haya yalikuwapo India ambako kulikuwa na Congress Party ya Ghandhi na All-India Congress League ya Mohamed Ali Jinnah.

Yaliyowafika Wahindi viongozi wa TAA waliyajua na hawakutaka yawafike Watanganyika.

Nafasi ya President wa TAA ikawa anatafutwa Mkristo wa kuijaza.

Chaguo la Abdul Sykes alikuwa Chief David Kidaha Makwaia wa Siha.

Hamza Mwapachu yeye alipendelea Julius Nyerere ndiye apewe nafasi ile 1953 na 1954 waunde TANU wadai uhuru.

Hivi ndivyo viongozi wa TAA walivyoweza kuiepusha Tanganyika na migogoro ya kidini katika vyama vya siasa.

TANU ilipoundwa mwaka wa 1954 ingawa Uislam ulikuwa na nguvu katika chama hiyo haikuwa sababu ya asiyekuwa Muislam kubaguliwa.

Matatizo yalikuja baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
 
Msajili aliona mbali... kingekuwa chama cha kipumbavu sana kuwahi kutokea kwenye uso wa Tanzania. Ninawapongeza sana maafisa waliokataa kusajili hicho chama cha kidini.
 
Msajili aliona mbali... kingekuwa chama cha kipumbavu sana kuwahi kutokea kwenye uso wa Tanzania. Ninawapongeza sana maafisa waliokataa kusajili hicho chama cha kidini.
Mama...
Umefanya haraka kutoa uamuzi kuwa chama cha kipumbavu.

Naomba urejee tena kusoma kwa utaratibu naamini utagundua kwa nini ilitokea vile.

Jiulize kwa nini African Association ilipoundwa 1929 waasisi 6 walikuwa Waislam na 3 Wakristo.

Kwa nini masheikh takriban wote walikuwa TANU na kwa nini Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe zaidi ya 200+ wote walikuwa Waislam.

TANU hakikuwa chama cha kipumbavu.

Mazingira ya ukoloni ndiyo yaliyosababisha Waislam wajikusanye chini ya AA na ikawa hivyo hadi kuundwa kwa TANU.

Kwa nini viongozi wa kanisa hawakuiunga TANU mkono na kwa nini walikuwa mbali sana na Nyerere.

Juu ya haya Waislam hawakuacha kuhangaika kutaka kuwa na chama ambacho kitawasikiliza.

Kwa nini unadhani imekuwa hivi?

Viangalie vyama vilivyopo na angalia mwelekeo.

Kipo utakachogundua.
Fungua macho yako.

Waislam walikuwa wanakosa nini ndani ya CCM chama kilichotokana na TANU chama walichokijenga wao?
 
Mama...
Umefanya haraka kutoa uamuzi kuwa chama cha kipumbavu.

Naomba urejee tena kusoma kwa utaratibu naamini utagundua kwa nini ilitokea vile.

Jiulize kwa nini African Association ilipoundwa 1929 waasisi 6 walikuwa Waislam na 3 Wakristo.

Kwa nini masheikh takriban wote walikuwa TANU na kwa nini Baraza la Wazee wa TANU lililokuwa na wajumbe zaidi ya 200+ wote walikuwa Waislam.

TANU hakikuwa chama cha kipumbavu.

Mazingira ndiyo yaliyosababisha Waislam wajikusanye chini ya AA na ikawa hivyo hadi kuundwa kwa TANU.

Kwa nini viongozi wa kanisa hawakuiunga TANU mkono na kwa nini walikuwa mbali sana na Nyerere.

Juu ya haya Waislam hawakuacha kuhangaika kutaka kuwa na chama ambacho kitawasikiliza.

Kwa nini unadhani imekuwa hivi?
Viangalie vyama vilivyopo na angalia mwelekeo.

Kipo utakachogundua.
Fungus macho yako.
Mzee Mohamed kubali tu kwamba hizo fikra zako za kidini haziwezi fanikiwa hapa Tanzania. Unapoteza muda wako. Hizo harakati ungezifanyia kwenye nchi zz kiislamu ungekuwa mbali sana.
 
Mzee Mohamed kubali tu kwamba hizo fikra zako za kidini haziwezi fanikiwa hapa Tanzania. Unapoteza muda wako. Hizo harakati ungezifanyia kwenye nchi zz kiislamu ungekuwa mbali sana.
Mama...
Fikra zangu si za kidini.

Huu ni uchambuzi ambao mtu yeyote huru anaweza kuwa nao.

Hivi ni vibaya kuuliza kwa nini Bunge na Serikali imehodhiwa na watu wa imani moja?

Au ni vibaya kuuliza mbona historia ya kweli ya uhuru ilifutwa hatuwasomi wazalendo waliopigania uhuru?

Sijui kama hizi ni harakati wala sijui unaposema ningekuwa mbali unakusudia nini.

Unakusudia hapa Tanzania kwetu niko nyuma?
Labda nikufahamishe.

Hapa JF nimepokea Certificate of Appreciation kwa uandishi wangu.

Waislam wa Tanzania wamenipa nishani mara mbili pia kwa uandishi wangu na kwa kusahihisha historia ya uhuru.

Naamini unakijua kitabu changu: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (London 1998).

Hivi karibuni hapa JF walikuwa wanapiga kura kuchagua mwandishi bora kwq kila jukwaa.

Wapiga kura 14 kwa mfululizo walinichagua mimi.

Baada ya hivyo ikasimamishwa na wapiga kura walikuwa wakisema sina mshindani.

Huenda hufahamu ni vipi mimi nimejua sana historia hii kuwapita watu wengi.

Babu zangu ndiyo walianzisha harakati hizi za kudai uhuru 1929 na najua historia yao.

Si kwa kuisoma vitabuni bali kwa kuwa harakati hizi zilikuwa ndani ya familia na ndani ya nyumba zetu.
 
Back
Top Bottom