Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,913
- 6,516
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake wa Chama cha Wakulima (AAFP) Taifa, Shani Ally Kitumbua, amemkosoa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche kutokana na kauli yake ya kukiita AAFP kuwa "chama cha mfukoni" na kudai kuwa kina watu wachache.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 5, 2026 katika Makao Makuu ya AAFP mkoani Dar es Salaam, Shani amesema kauli hiyo inakidhalilisha chama hicho na wanachama wake.
Amesema AAFP ni chama halali kilichosajiliwa, kilishiriki uchaguzi mkuu na kinastahili kuheshimiwa kama vyama vingine vya siasa. Aidha, amesema chama hicho kilikubali kushiriki kikao kilichoandaliwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa viongozi wa vyama vya siasa kwa hiari, kwa lengo la kuchangia maridhiano na kuimarisha amani nchini.
Soma Pia: Heche: Ni kweli hakuna upinzani, CHADEMA ni chama kikuu cha siasa nchini
"Mazungumzo ya aina yoyote yakiacha CHADEMA nje, hakuna mazungumzo hapo. Tusidanganyane, unachukua chama kinaitwa AAFP, chama chenye watu wawili unachukua AAFP, chama ambacho hata mke wa mwenyekiti wake ni mwanachama wa CHADEMA. Chama cha mfukoni 'briefcase', ukiacha CHADEMA nje umeacha robo tatu ya wananchi wa nchi hii”, alisikika Heche.