#COVID19 Uganda yatangaza Visa vipya 31 vya COVID19, visa 16 ni Watanzania

Wizara ya afya Uganda imetangaza Visa vipya 31 vya Covid 19 baada ya sampuli 1,116 kupimwa na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253, wagonjwa 23 ni kutoka mipakani kati yao 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na 4 Wakenya, wote wamekabidhiwa katika nchi zao. Kwanza TV on Twitter
Watasituka badae sana

Kuwa wanapoteza muda kwenye ugonjwa wa mafua mtu anaugua na kupona mwenyewe then anaugua rena

Wanazidi kupoteza pesa za bure

Kuna wahuni wananufaika na hio fursa mpaka raisi wao asituke its too late
 
Huu ugonjwa sasa unasambazwa na madereva wa malori....kwanini serikali isifanye hata jitihada kuwapima hawa madereva.
Tumeshawaelewa nia ya kutokutangaza maambukizi....kazi tunawaachia majirani kutuumbua tu kila siku.
Kuna mtu alishatoa wazo kama hilo. Ila mpaka sasa naona serikal hailifanyii kazi. Sijui wameridhika na hali
 
Uganda imetangaza Wagonjwa 31 wapya wa #COVID19 waliopatikana baada ya sampuli 1,116 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253

Wagonjwa 23 ni kutoka mipakani ambapo sampuli 896 zilichukuliwa na 8 ni waliopimwa wakiwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali kuwa na #CoronaVirus

Wizara ya Afya nchini humo imesema katika ya wagonjwa 23 waliopatikana mipakani, 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na wanne ni Wakenya. Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao

Aidha, Wizara imebainisha kuwa hadi kufikia sasa jumla ya Wagonjwa 69 wamepona
Huku tuna ambiwa yamepungu jamani!
 
Juzi hapo walikuwepo madereva wa malori kama 800 Wanapimwa mabibo,au una maanisha kupimwaje?

Wakapime mipakani. Dereva akipimwa Mabibo inaweza kumchukua siku hadi tatu kabla hajafika Mutukura. Hapo katikati anaweza kuambukizwa! Tujitahidi kuthibitisha kwa nchi jirani kuwa madereva wetu ni salama. Mpakani!!
 
Wakapime mipakani. Dereva akipimwa Mabibo inaweza kumchukua siku hadi tatu kabla hajafika Mutukura. Hapo katikati anaweza kuambukizwa! Tujitahidi kuthibitisha kwa nchi jirani kuwa madereva wetu ni salama. Mpakani!!
Kwani kuna shida gani kama kwenye gari kunakuwa na watu wasiozidi 2?
Cha muhimu ni kupimwa na kutembea kwa tahadhari,haijalishi amepimiwa wapi.
Siungi mkono serikali kufanya chochote ili kiwaridhisha hao wakenya na waganda wako.
Hizi propaganda zina mwisho wake
 
Back
Top Bottom