Uganda yatangaza Visa vipya 31 vya COVID19, visa 16 ni Watanzania

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,210
2,000
Uganda imetangaza Wagonjwa 31 wapya wa #COVID19 waliopatikana baada ya sampuli 1,116 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253

Wagonjwa 23 ni kutoka mipakani ambapo sampuli 896 zilichukuliwa na 8 ni waliopimwa wakiwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali kuwa na #CoronaVirus

Wizara ya Afya Nchini humo imesema katika ya wagonjwa 23 waliopatikana mipakani, 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na wanne ni Wakenya. Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao

Aidha, Wizara imebainisha kuwa hadi kufikia sasa jumla ya Wagonjwa 69 wamepona
 

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
4,991
2,000
Uganda ajifunze kukaa kimya

Kila Nchi ina taratibu zake, mzee mseven ajifunze kwa Kenyatta
 

batmanwafez

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
498
1,000
Huu ugonjwa sasa unasambazwa na madereva wa malori....kwanini serikali isifanye hata jitihada kuwapima hawa madereva.

Tumeshawaelewa nia ya kutokutangaza maambukizi....kazi tunawaachia majirani kutuumbua tu kila siku.
 

encyclopaedia Tanzaree

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
470
500
Huu ugonjwa sasa unasambazwa na madereva wa malori....kwanini serikali isifanye hata jitihada kuwapima hawa madereva.
Tumeshawaelewa nia ya kutokutangaza maambukizi....kazi tunawaachia majirani kutuumbua tu kila siku.
Juzi hapo walikuwepo madereva wa malori kama 800 Wanapimwa mabibo,au una maanisha kupimwaje?
 

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
6,147
2,000
Uganda ajifunze kukaa kimya

Kila Nchi ina taratibu zake, mzee mseven ajifunze kwa Kenyatta
Utaratibu wa Uganda kutangaza majibu yote hadharani. Kila nchi na utaratibu wake.

Mmesahau! 1.5 trillion zilitafunwa na majizi CCM
 

Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
4,991
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom