Wizara ya Afya ya Tanzania inapanga kuvunja Programu za Kitaifa za kupambana na UKIWWI, TB, Malaria na Chanjo

JICHO LA KARIBU

New Member
May 4, 2023
1
0
Wizara ya Afya chini ya Uongozi wa Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu inaandaa Mpango wa kuzivunjilia mbali Programu za Kitaifa za Kupambana na magonjwa ya UKIMWI,MALARIA,CHANJO,MAGONJWA YASIOPEWA KIPAUMBELE na Kifua Kikuu na majukumu na shughuli za Msingi za hizo Programu kuhamishiwa katika Idara na Vitengo vingine ndani ya Wizara ya Wizara ya afya .

Hali hiyo imekuja baada ya kuona Programu zimeweza kufanikiwa ipasavyo kupambana na maambukizi ya UKIMWI,KIFUA KIKUU, UKOMA,Malaria na kufikia malengo ya CHANJO hali inayosabibisha Programu hizo kuonekana hazifanyi kazi yoyote yenye tija katika Wizara ya Afya.

Ikumbukwe Program hizi ndio zimewezesha na kufanikisha ipasavyo TANZANIA KUWEZA kupambana na magonjwa ya UKIMWI, MALARIA,SURUA,POLIO,MABUSHA,MATENDE, USUBI, KIFUA KIKUU NA UKOMA hali ambayo imeifanya Jamii kuyaona magonjwa hayo ya kawaida sana. Mfano kwasasa Watanzania hawaogopi sana UKIMWI KULIKO KISUKARI kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Programu za UKIMWI NA Kifua kikuu. Kwasasa wananchi pia hawana hofu na Ugonjwa wa Malaria kutokana kazi nzuri inayofanywa na Mpango wa Taifa wa Malaria.

Programu zimefanya kazi nzuri zinatakiwa kupewa MAUWA yake kabla hazijavinjwa na Mganga Mkuu wa Serikali DR NAGU.

LEO kutokana na utendaji mzuri wa Programu hakuna Mtoto anayekosa Chanjo, Mgonjwa aneyekosa ARV,Dawa za Kifua Kikuu na Dawa za Malaria na elimu ya magonjwa hayo imefika kila Mahali. Programu zipewe Mauwa yake mapema kabla ya Intervention MPYA za CMO za kwenda kuharibu msingi ambao ulikuwepo wa Programu maarufu kama Mipango ya Taifa ya kupambana na kudhibiti, UKIMWI,MALARIA, KIFUA KIKUU NA CHANJO.

Kama Nchi Tulifurahia kuona Programu hizi zimeheshimiwa na kuanzishiwa Idara Maalumu ya Programu kwa ajili ya kufast track mambo/kazi na shughuli ziweze kutokea KWA HARAKA. Kwa hili tunatoa MAUWA na Pongezi kubwa sana kwa Mh Waziri Ummy Mwalimu kwa Idea hiyo ya Programu zote kuwekwa katika Idara ya Programu kwa kuleta ufanisi mzuri. Utekelezaji wa mawazo ya Mh Waziri wa Afya Ummy umeingia DOA baada tu ya kuteuliwa kwa Dr Nagu kuwa Mganga Mkuu wa Serikali kwani Mganga Mkuu wa Serikali maono yake katika hizi Programu ni negative negative negative hana ushirikiano na Programu zote na Mpango wake ni kuzivunja kabisa na kukaidi maelekezo ya Waziri wake.

Kwasasa utekelezaji wa majukumu ya Programu toka Dr Nagu aingie Wizarani umekwama hakuna shughuli zinazotekelezwa, Viongozi na watumishi katika Programu wapo harassed, vibali vya kazi havitolewi yaani Programu zinakwamishwa ipasavyo kutekeleza majukumu yake.

Mytake; mfumo huu wa Mganga Mkuu wa Serikali wa kukwamisha utekelezaji wa majukumu ya Programu kwa wakati unaweza kuleta athari kubwa kwa Nchi katika siku za mbele hasa katika upatikanaji wa bidhaa za afya e.g dawa na vitendanishi, watumishi waliojengewa uwezo wa kutibu na kuhudumia wagonjwa, elimu ya umma kuhusiana na magonjwa kupungua katika jamii na Wafadhili WAKUBWA hususan Global Fund,GAVI na PEPFAR/CDC kusitisha ufadhili wao baada ya kuona majukumu ya program hayatekelezwi kwa msingi unaosimamiwa na Programu.

Jicho la Pili la Wizara ya Afya linamuomba Mh Waziri wa Afya asimamie kauli yake aliyoitoa ya kuziundia Programu Idara yake ili ziweze kutekeleza kwa kasi ya HARAKA MAJUKUMU YAKE. UAMUZI WA MH WAZIRI UMMY MWALIMU TUNASHUKURU ULIANZA KUTEKELEZWA NA ALIYEKUWA KATIBU MKUU PROF MAKUBI kuanzisha idara ya programu iliyojumuisha programu zote isipokuwa program mbili au tatu za wizara zilikuwa bado hazijajumuishwa katika idara hiyo. Matarajio ya jicho la karibu la Wizara ya Afya ilikuwa kuona Programu zote zilipo Wizara ya Afya zinawekwa katika idara moja lakini Baada ya kuchaguliwa kwa Mganga Mkuu wa Serikali uamuzi huo umeanza kuwekewa vikwazo vingi na Mganga Mkuu na Wakurugenzi wengine wa Idara na Vitengo wa Wizara ya afya kwa kutotambua maamuzi ya Waziri na hoja yao KUU ni kugawana majukumu/shughuli na RASILIMALI zilizopo kwenye Programu kwenda katika idara zingine NA KUZIVUNJILIA MBALI PROGRAMU ZOTE . Chondechonde Mh Waziri kuelekea kusomwa kwa bajeti tunaomba Mganga Mkuu asiingilie majukumu ya Programu azipe uhuru Programu wa kupanga na kutekeleza sio kila kitu kinachopita kwake ni kukwamisha tu

Jicho la Pili la Wizara ya Afya linaomba Mh Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wapitie upya majukumu ya Mganga Mkuu wa Serikali ni yapi kwanini hivi sasa Mganga Mkuu wa Seriakali amegeuka kuwa Mhasibu wa Fedha, Muidhinisha malipo, mtoa vibali vya matumizi ya mafuta na mambo kede wa kede ambayo yeye sio Core business yake. Ukifatilia Mganga Mkuu wa Serikali hatekelezi majukumu yake ya Msingi na badala yake anatekeleza majukumu ya katibu Mkuu na Afisa Mipango

Jicho la Pili la wizara linavyoandika hivi sasa limeshaona baadhi ya majukumu na kazi ya Programu zimeshaanza kugawanywa katika Idara zingine

Mwisho tupo tayari kwa Programu za Wizara ya Afya kuvunjwa kutokana na maono ya Dr Nagu kwani ndio mwelekeo wake wa sasa wa kuzivunja program zote lakini kabla hajafanya hivyo tunashauri ufanyike utafiti kama Programu zinahitajika au hazihitajiki

Mwisho Pamoja na changamoto za Watumishi katika Programu hizo unatakiwa kuwekwa mkakati wa kuziimarisha kwani zimefanya makubwa katika Nchi yetu katika kudhibiti majanga. Hiki kinachoendelea hapo wizarani sana kinaweza kurudisha magonjwa yote ya mlipuko ambayo program zilishamudu kupambana nayo Mganga Mkuu na Wakurugenzi wake wasione wivu kwa rasilimali nyingi program zinazopata hadi kufikia hatua ya kuwapora rasilimali hizo bali hizo rasilimali zipo kwa ajili ya majukumu na Core Business ya program
 
Vimeumana. Wizarani mpo busy ila output zenu hazinaga tija. Umejazana maafisa wengi ambao hawahitajiki Kwa muundo na majukumu ya wizara yanayotakiwa.

MoH ikipata kiongozi mzuri anapasa kufanya tathimini ya mfumo na muundo wa wizara. Tathimini hiyo itaonyesha kama Kuna tija ya kuendelea na program hizo au lah.

Mleta mada ulivyo elezea sio kwamba majukumu yaliyokua yakitekelezwa na program yatasimamishwa Bali ni muundo wa kiutendaji na uratibu ndo utakaobadirika (operationalization).

Najua vita hiyo ni kubwa coz inaenda kugusa maslahi ya watu ambao maisha yao yanahitaji activities za program.

But all in sisi wananchi tunataka ufanisi na tija. Msifanye mabadiriko ili kukomoa watu Bali msingi wa mabadiriko iwe ni kuongezeka ufanisi na tija Kwa program.

Viongozi wa wizara mjue majukumu yenu , mjikite katika masuala ya kisera, uratibu na kutoa miongozo na kutafuta rasilimali pesa . Mambo ya kiutendaji yashusheni Kwa wataalamu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom