Karibuni SUA Morogoro utalaam wote utapata free idara ya uzalishaji wanyama (DASP)Nisamehe sana,nilikuwa vijijini kwa muda mrefu kidogo kwa ajili ya mambo yetu haya ya kilimo. Miezi mitatu iliyopita niliweka sato 26 vifaranga,mpaka jana tumerecord sato mmoja kafa,kwa hiyo imenipa nguvu kwamba bwawa langu liko mahali sahihi kabisa kilichobaki ni maboresho,hasa aina ya chakula.
Mwezi juni nilipata Kambale 52,nimewaweka ktk visima vidogo,huku nasubiri bwawa jipya likae sawa,yaani lijijenge kupokea wageni. Kwa mwezi mzima sasa hakuna kambale aliyekufa. Nitakwenda Mbegani/ kunduchi nikachukue shule zaidi ili nifuge kwa wingi. Hapo nitapata mbegu ya kuuza. Mwaka jana kigogo mmoja alikosa mbegu ya kambale,tulitafuta sana bila mafanikio.
Pili,pale Kinguruila gerezani pana mbegu ya samaki inauzwa kwa bei nzuri sana,kifaranga kimoja Tsh 30/ sio 300 kama huku Mkuranga. Contact za mhusika nimepata,kwa aliye tayari aniambie nimpe.
Kwa ujumla ninafurahia kufaulu mtihani wa kwanza,yaani pilot trial niliyofanya.