The conceited
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 429
- 483
wakuu ni aina gani ya samaki ambao wako katika soko ukilinganisha na ufugaji wenyewe
Vifaranga hivyo vina bei kwa sababu kwanza uzalishaji wake unahitaji uangalizi wa juu, pia wanalelewa kwa muda mrefu mpaka kufikia umri wa kuweza mkulima kwenda kufuga.Mkuu mleta mada naomba kujua kwanini vifaranga vya kambare vinabei kubwa yaani 500?wakati sato ni 300?
Gharama ya monosex ni sh 300 kwa kifaranga. Wapo dealers wengi mfano Mzee Noni yupo vikindu (huyu mnapigiana gharama ya usafiri anakuletea hadi shambani); yupo mzee Eden yupo Chanika; yupo ruvu fish farm yupo ruvu bagamoyo. Hao wote wapo vizuri. Wapo wa mikoani lakin kwakuwa upo Dar basi pokea hao.Wakuu kwema humu? Nahitaji kujua gharama ya sasa ya vifaranga vya samaki monosex bei kwa kifaranga ni sh ngapi sasa? na reliable dealer anapatikana wapi? na chakula chao bei yake ni sh ngapi kwa sasa mimi napatikana DSM, mkuu bukoba boy msaada wako unahitajika kama unataarifa yoyote najua wewe ni mdau mkubwa kwenye sekta hii.
Mkuu samaki aina ya sato na kambale wanahitaji jotoridi kati ya 26-33 ili waweze kukua vizuri. Chini ya hapo kasi ya ukuaji inakuwa ya chini. Katika Mikoa tajwa unawza kufuga kwa msimu kwa samaki hao tajwa.je hali ya hewa ni ipi zuri kwa mfano iringa mufindi inafaa kwa samaki au kilimanjaro moshi hali ya hewa inafaa kwa ufugaji samakii? Naomba msaada wenu.
Fafanua mkuu sijakuelewa. Ila wengi wanafuga sato. Kambale kama unapatia soko lake nao wako vzrwakuu ni aina gani ya samaki ambao wako ktk soko ukilinganisha na ufugaji wenyewe
Morogoro tembelea kituo cha serikali pale Kingolwira. Gharama inategemea na aina ya udongo katika eneo lako. Mfano ukipata eneo lenye udongo wa mfinyanzi basi bwawa ni la kuchimba tu hivyo gharama ni ya excavator au vibarua tu.
- gharama kwa ujumla kama mimi nataka kufuga kulimo cha biashara . gharama average(general) zinakuwaje?
- na sehemu ninapoweza pata hao samaki wa kuanzia? nipo morogoro.
Maeneo ya rufiji kando ya maeneo ya mto yanafaa na yana udongo wa mfinyanzi.natamani sana kufuga samaki,je maeneo ya rufiji yanafaa?na upatikanaji wa maji vibali naazaje?na mtaji wa wastani sh ngapi ili uweze uza kwa faida angalau?
Mahesabu ya kwenye karatasi matamu sana! Ila bahati mbaya hayajawahi kumwacha MTU salama!Mkuu Million 40 Bora nikanunue Eicher Bus nikusanye laki mbili kila siku... kwa Mwaka Mmoja sikosi m100
Unaweza nisaidia contacts zao mkuu?? nasikia huwa wanatabia ukitaka monosex wanakuchanganyia hii changamoto unaweza epuka nayo vipi ndugu?Gharama ya monosex ni sh 300 kwa kifaranga. Wapo dealers wengi mfano Mzee Noni yupo vikindu (huyu mnapigiana gharama ya usafiri anakuletea hadi shambani); yupo mzee Eden yupo Chanika; yupo ruvu fish farm yupo ruvu bagamoyo. Hao wote wapo vizuri. Wapo wa mikoani lakin kwakuwa upo Dar basi pokea hao. Chakula wapo Farmers Centre Buguruni (1,800-2500/kg); Ruvu fish farm (3500/kg); Noni ( 2900/kg), Hills (4000/kg). Good news kuna kiwanda kinajengwa Moshi itakuwa chini ya hapo.
Njoo pmnenda wizara ya kilimo pale vetinary watakupa maelekezo.
Unafukua makaburi? Kumbuka ule msemo mali bila Daftari hupotea... So Biashara lazima uiandike mkuu... acha kujidanganya labda uwe na biashara ya kukata vimeoMahesabu ya kwenye karatasi matamu sana! Ila bahati mbaya hayajawahi kumwacha MTU salama!