Asante Mkuu kwa mchanganuo huu, Je wewe umeshaanza kufuga au unaelezea nadharia? Katika uwekezaji au biashara yeyote kuna changamoto zake, kwa hiyo usijekuingia katika uwekezaji au biashara kwa mahesabu haya; mambo yakienda tofauti unaweza kukata tamaa.
Unaweza kuona ufugaji wa kuku wa kienyeji ni rahisi, lakini siyo rahisi kama wengi wamavyofikiria (kwa uzoefu wangu). Nami nilikuwa na mahesabu kama haya nikanunua kuku zaidi ya 35, lakini zilianza changamoto za magonjwa na walibaki wachache sana. Unaweza kusema tumia dawa. Kwa sasa kuku wa kienyeji nimeweka kwa ajili ya matumizi binafsi lakini kwa biashara niliamua kufuga kuku wa nyama (broiler). Nimetoa comment kutokana na uzoefu niliopata lakini wengine wanaweza kuwa na uzoefu wa tofauti na michango zaidi inaweza kutolewa.