I'm just dissapointed kwamba some people wamekwenda nje ya topic na kuanza kupigana vijembe na kejeli. Inaudhi sana pale unapofuatilia thread halafu unakuta post za ajabu ajabu za watu kutupiana maneno badala ya kuchangia thread au kuipinga.
Kwa wale ambao Zitto "kawakuna" na kuanza kuquestion credibility ya opposition parties leaders, pia nao mtazamo wao ni finyu. Kama alivyowahi kuandika kiongozi mmoja wa upinzani ambaye pia ni member humu, watu wengi hatuthubutu hata kuweka our real identities in this forum. Tunapenda kuchangia na kuipinga serikali na mambo mengine kibao, lakini tukitumia fake names. Sasa, jiulize wapinzani hapa nchini wanacourage kiasi gani ya kwenda kusimama pale viwanja vya Jangwani na viwanja vingine hapa nchini na kutaja majina ya mafisadi na mambo mengi lukuki ya kuikosoa serikali. Wangapi tunaweza hilo? If we can not even reveal our true identities humu kwenye forum, tunaweza kuwenda Jangwani na kuongea kuhusu Lukaza, Lowassa etc? Lets just be fair to leaders of our opposition parties. Wanafanyakazi katika hali ambayo mazingira yanaruhusu. Huwezi kutoa mifano ya Obama kule USA unataka kulinganisha na Mbowe hapa bongo. Level ya democracy na civic education katika hizi nchi mbili ni tofauti sana. Mazingira ya nchi yetu yanapelekea wao kufanya kazi kama wanavyofanya. Lets all give them credits to that.
Kama you think they dont deserve any credits, then anzisha chama chako cha upinzani, uje na sera za Obama then tutakupa kura mpaka ikulu.