Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Kimenuka NHC, Wizara yamweka kitimoto NMK na timu yake

Asubuhi ya tarehe 2April, 2013 siku ya Jumanne, Bwana NKM amekutana na joto ya jiwe pale ambapo watendaji wakuu wa wizara ya ardhi ambapo wizara inawajibika, walipomtaka yeye na team yake watoe maelezo kuhusiana na kuanguka kwa jengo! Maswali yaliyokosa majibu ni kama ifuatavyo:

1. Kwamba wizara ambayo NHC inawajibika kwake imesikitishwa na kuanguka kwa jengo ambalo NHC wana ubia na kwamba hawakutarajia uchapakazi “unaosifiwa” wa NKM angefanya uzembe wa kiwango kile.

2. Kwamba NHC kwa sababu ndiye mmiliki wa hati ambapo jengo limejengwa, wao ndio walio-apply for building permit, sasa je, waliomba permit ya ghorofa 10 au 16?

3. Kwamba iwe walipewa ya ghorofa 10 au 16, je, wao kama si tu wamiliki wa 25% bali baada ya muda ilitakiwa wamiliki 50% ili iwe 50/50, kwa nini hawakutimiza wajibu wao kama strategic partners?

4. Kwamba inakuwaje NHC ina team ya wataalamu then they just let it go, dancing the tune of the developer?

5. Kwamba hili haliitaji mkataba ukoje, provided walikuwa strategic JV partner, wana la kujibu katika kushiriki kupoteza maisha ya watanzania 36.

Mchapakazi NKM na team yake wamekosa majibu na hivyo kuambiwa aondoke akaandae majibu ya kutosha!

MY TAKE:
Mimi simkubali NKM, na sitamkubali, mbali ya kwamba kuna watu kama Pasco wanamkubali sana, huwaambii kitu.
Kwanza ni mchakato uliotumika kumpata ambao ni kama alipewa tu hiyo nafasi bila ya kumfanyia ushindani ili apatikane na kulinda maslahi ya waliomuweka. Mtakumbuka interview ya kwanza ya PWC ilipigwa chini, ukafanyika uchakachuaji, mzigo ukaamishiwa Ernst &Young, ili kijana apate nafasi!

Baaada ya kuingia NHC, amelifanya shirika kama kampuni ya simu za mkononi ama SUMATRA!
Katika management team yake aliamua kujaza washikaji (Fellow bankers) na watu wake wengine wa karibu huku akiondoa wataalamu waliosomea uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na technical issues za NHC.

Ndio maana nimesema NHC si shirika tu kama kampuni ya simu kwamba alimradi fulani ana degree au MBA can fit in! Haina tofauti na TANESCO ama TANROADS, bora hata ingekuwa SUMATRA! Hebu jiulize NKM ndo angekuwa pale TANESCO au TANROADS halafu akatimua wote technical expects, akaweka his winning team (failing team so to say), hayo mashirika yangekuwaje? Ndo tunayoyaona hapo NHC. Wataalamu wote wa kumshauri kawatupa mikoani.

NKM amejitahidi sana kucheza na media ili kuweka mambo yake sawa! Nyote mnafahamu Yule bwana wa Maisha ni Nyumba ambaye inasemekana yupo kwenye payroll ya NHC.

Watanzania wengi tunapenda kufuata mkumbo na kusifia tu bila kuwa na facts! Mnaosema NKM kalibadilisha shirika, kivipi? Mradi wa Medeli Dodoma umekuwa ni white elephant! Ubungo NHC nao inakula kwake big time, baada ya wengi kulipia downpayments na kuamua warudishiwe pesa zao! Kwa nini? Wengi walikurupuka, ila baada ya kwenda benki(wengi walikuwa wananunua kwa mkopo) na kupigiwa mahesabu ya mkopo, achilia mbali VAT, nyumba zilishoot almost three times asking price! Am afraid the same is going to happen kwa projects za Kigamboni na nyinginezo!

Kuhusu ongoing NHC projects, I can bet na watu kama Pasco kwamba they are going to be white elephant big time!!!

KWA NINI?

NHC kama shirika la umma, linahitaji kufuata taratibu zote za manunuzi kama inavyotakiwa na PPRA! Sasa nyote mnajua katika utaratibu wa tender system, huwezi shindana na wawekezaji privates kama akina FIDA ambao hawana PPRA na materials wanafuata wenyewe na ku-save a lot! Lakini leo hii NKM anajenga apartments Upanga ati ashindane na wale wawekezaji wengine (private developers? Wapi na wapi? Kwanza wengi wao wana certificate of incentives inayowapa nafuu ya kodi ama kutolipa kodi kabisa! Kibaya zaidi NHC wao bei zao wanauza as per prevailing market rate, kibaya zaidi wanacharge VAT! Nani atanunua za NHC kwa black market iliyopo na imperfections zilizopo katika biashara ya nyumba hapa bongo! Kwa nini nisinunue from other developers?

Narudia, tusitofautishe NHC na TANROADS au TANESCO! Shirika linahitaji wataalamu, na si tu kisa mtu anajua kujipendekeza na kuwa na downloaded presentation hiyo hiyo tu mkamwona kichwa na kumpatia shirika! Hii sio SUMATRA au shirika la bima! Linahitaji technical know how ya product to be traded by a corporation concerned, si technical know who! Nilitegema management team iwe na professionals katika Real Estate pia, achilia mbali watendaji wa chini! Kibaya zaidi hata team yake inapwaya! Huwezi kujaza bankers pale NHC! Ingekuwa TANROADS hayo madaraja yangekatika kila siku au TANESCO ndo ingekufa kabisa, sasa NHC ndo tunayaona leo!!

Mwisho, nimeangalia kiingereza cha mkurugenzi mkuu alipojibu hoja humu JF, dah! Ni kweli kiingereza si lugha yetu, lakini kwa NKM na mbwembwe zake najua pale ka-edit sana kabla yaku-post lakini, wapi!

It is high time uweke mikoba chini mkuu, you don’t belong where you are! Your smartness can only be shown now!

Najua wengi mtaniita nina chuki binafsi kama livyo kawaida kwa wengi baada ya kuchanganua kwanza kilichoandikwa wakajenga hoja!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wizara-yamweka-kitimoto-nmk-na-timu-yake.html
​

i should declare kwamba simfahamu Mchechu hata kidogo zaidi ya kumsikia, kumsoma na kumuona kwenye media. AbasMzeEgyptian, hata kama una point lakini post yako imekaa ki chuki zaidi, umeshindwa kabisa kuficha hatredness yako kwa Mchechu (NKM kama unavyomwita). Hivi wewe hauna mapungufu?? Are you that much an angel, so to say?? Zinaonekana ni fitna za watu waliozoea kufanya kazi za umma zaidi, sishangai pia kwanini vijana wengi wanapata shida kuzoea mazingira ya ufanyaji kazi serikalini au ofisi za umma ... mtu akijituma au kutimiza wajibu wake ni kama anakaribisha balaa ... fitna, masengenyo, chuki na majungu are orders of the day. Mangapi makubwa yametokea kwenye nchi yetu na ni nani aliyejiuzulu?? Ungepaza sauti this much wakati wa vimeo vya mabomu Gongo la Mboto + Mbagala, EPA, meremeta, radar etc ... then ningekuona ni mtu wa maana sana. Kwa mtu aliyepitia private firms kujiuzulu its not an issue and its not the end of life, sitoshangaa pia kama Mchechu ata tender resignation yake kuachana na watu kama nyie mnaokalia majungu tu na kusubiri uone wapi mtu usiyempenda anakosea ... opportunities are always there! Chuki zako ni bure! Kila la kheri!
 
Last edited by a moderator:
Ngoma ikivuma sana hupasuka; walisema wahenga; Nehemia Kyando Mchechu ni bogus; na kuanguka kwa jengo hilo Indira gandhi street is an eye opener; shughuli za NHC zichunguzwe kwa undani kabisa, Majengo mengi mapya mapya ya NHC viwango vya vya ujenzi na usimamizi leave a lot to be desired! mengi yanavuja na hayana estate officers wa kuyaangalia kwa usafi, huduma za maji na umeme na ulinzi. wamecommission wakala bogus kama NKM wa usafi, katika baadhi ya majengo huwezi kuingia msalani kulivyo kuchafu. A case in point ni jengo lililopo Arusha roud about ya florida kuelekea mianzini ambalo ni maskani ya shirika la utangazaji tanzania TBC

Nehemia Kyando Mchechu na timu yake wawajibishwe kinidhamu na kisheria
 
Wakati mwingine head hunting hufanyika pia... for a good reason na siyo lazima ufisadi...

I have participated in recruitment processes... wakati mwingine kazi inatangazwa.. wanaoomba unakuta ni watu wa viwango vya chini mno... hata ukiwashindanisha wenyewe kwa wenyewe utaishia kupata mtu asiye stahili.In such circumstance u may be forced to resort to head hunting.

Nehemia as I know him is a material for the position.... tunaweza kulaumu na kusema mengi lakini anabakia THE CEO FOR NHC for the time being..tukubali na tumpe nafasi jamani. It could have been you or me..ila haikuwa.

Nakuunga mkono kwani hata kama procedure zilirukwa lakini tunaye Mtu muafaka kwa NHC. Tunajua shirika la Nyumba halijawahi kuwa na ufanisi mkubwa kama uliotokea baada ya kumwajiri Mchechu. tatizo letu tunakariri procedures kwamba ndo zinatupa the right person. Ukweli ni kwamba some time procedure zinafuatwa na tunakosa right person then hapo ndo utashi na right judgement inatakiwa kutumika kufanya head hunting. inawezekana hata wanaolalamika wasingeweza fanya reformation kubwa kama ilivyofanywa na Mchechu bali wengi wao nyumba zao wamenyang'anywa kwa kutolipa kodi au kubomolewa kwa kupisha ujenzo wa kisasa.
 
Mtu mwingine aliyepata uteuzi wa bwerere bila sifa za kutosha ni Bw. Eliudi Betri Sanga, mkurugenzi mkuu wa LAPF. Huyu pia aliteuliwa kinyamela kufuatia mbinu chafu zilizofanywa na mzee Luhanjo akiwa bado ni Katibu Mkuu Kiongozi pale Ikulu. Matokeo yake Sanga amegeuza LAPF kama NGO yake, ukitofautiana naye kidogo tu, au akikuhisi ni tishio kwake anakufanyia hila akufukuze kazi. Watu wengi wamefukuzwa LAPF bila kosa lolote. Jamaa pia amefanya ufisadi wa kutisha, ghafla ana hela za kufa mtu, amenunua, majumba ya kifahari, magari ya kifahari, anamiliki shule kubwa ya kifahari, mashamba makubwa nk. Anatishia watu, ukinichezea nitakufukuza halafu nitahonga mahakamani usirudi.

Naye huyu anapaswa amulikwe na kuchukuliwa hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na kufilisiwa.
 
Mmh hii kali sasa, kweli we dare to talk openly.,ngoja wanahabari waikamate hii na kuishikia bango tuone kitakachoendelea.

Tanzania hakuna wana habari wako akina Pasco wa JF ambao wao nii bahasha na kumpepea Lowasa . Atakaye andika bila kuhongwa habari hakika Tanzania hayupo wao wanasoma hapa na kuishia mitini .
 
Aisee kweli Dunia haiishi majungu na fitna pole mtoa post
 
yule jamaa ni jembe ! habu tukumbuke jinsi shirika lilivyo kuwa linadorora huko nyume, na sasa hivi kuna hatua waliyo fikia! binafsi yangu hata kama walimchomeka anafaa nafasi ile. habu kumuka walivyo vutana bi TIBAIJUKA , binafsi nimependa approach yao jointy partnership, wanita wawekezaji waendeleze maeneo wasio na uwezo wa kuyaendeleza na wanagawana kipato, angalia maswala ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu na kushirikiana na mabenki kukopesha raia...... hizi ndizo standard za kimataifa. big up nchechu............. watu wanamajungu mjini hapa
 
Mwacheni mchechu apige kazi, watanzania hatupendi kuona jambo likifanikiwa, yaani kazi yetu ni kuharibu tu.mwacheni mchechu apige kazi
 
Kama Nehemia ana uwezo na amefanikiwa huko ni big up kwake

Kama uteuzi walicheza hizo rafu kwa kutumia mwanya wa uzoefu wake huko alikopita kwa ajili ya malengo la kulihujumu taifa,napinga kwa nguvu zote huo uteuzi

Huu mwaka inabidi tuwe makini sana,kimsingi hatukustahili hata kuibembeleza hii serikali iliyoingia madarakani kwa njia ya KAGODA.

Inawezekana yaliyosemwa miaka minne iliyopita sasa yanadhihiri.
 
Jamani. Anayemfahamu Nehemia privately nimpe Jina la huyu anayemchafua mitandaoni
 
Mi najuaga CEO wa mashirika yote ya serikali hua ni presential appointment sasa haya mambo ya usahili sijui nini yanatokea wapi? Performance ya Nehemiah pia jamani tuweni wakweli, jamaa kaibadiri sana NHC.
 
Msechu natumaini yuko vizuri ingawa simjui kiundani...ila akileta ufisadi..afungwe tu.
 
Kwanini Nehemia azungumzwi sana tunasahau histori ya shirika lilikuwa limekwisha kabisa sidhani kama tutakuwa wakweli tusipokuwa tayari kuona mchango wa Nehemia kwa shirika au lazima wachambuzi wa wa mambo watakuwa tayari kukumbuka wapi tumetoka? Tusimwandike kwa chuki binafsi tuwe wakweli kwenye nafsi zetu huyu kijana ni big up sana, tuache chuki binafsi tuongozwe na utajiri wa shirika na mchango wake aliutoa kwa shirika hilo
 
Mheshimiwa Raisi Dkt John.P.Magufuli angalia ufisadi huu wa maafisa wa umma kujilipa mamilioni ya kununulia thamani za majumbani(Furnitures)
 
Mheshimiwa Raisi Dkt John.P.Magufuli angalia ufisadi huu wa maafisa wa umma kujilipa mamilioni ya kununulia thamani za majumbani(Furnitures)

Hata kama kapatikana kifisadi je Shirika la nyumba alivyoingia lilikuwaje na je sasa hivi Shirika limepiga hatua kiasi gani wacheni unafki usio kuwa na mantiki
 
Back
Top Bottom