Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Ufisadi kwenye uteuzi wa Nehemia Mchechu?

Waberoya,

NHC si shirika la umma tena, si kwa masilahi ya umma wala Taifa, ni kwa masilahi ya Wateule wachache!

Imagine kuwa wewe ni mjumbe wa NEC unakwenda NHC kuomba nyumba, halafu Masanilo Mkulima naye anakuja kuomba kununua nyumba.

NHC kwa kutumia fedha za wananchi imejenga nyumba hii kwa kutumia Dola Elfu kumi ($10,000.00), wanakuuzia nyumba wewe Wabeyora kwa kuwa unafahamika na ni mkubwa kwa Dola elfu kumi na tano ($15,000.00), tena mbaya zaidi kwa kuwa una mamlaka na uzito wa kisisasa na kichama, wanakuuzia hata nyumba tano, kutegemea na mfuko wako na uzito wako.

Masanilo anaambiwa "hatuna nyumba tena, lakini kamwone Waberoya anauza nyumba tuliyomuuzia". Masanilo anakwenda kwa Waberoya anamwambia naipenda nyumba hii naomba kuinunua, Wabeyora anatoa bei, anadai nyumba ile ni Dola laki moja ($100,000.00) na tayari zile nyumba nyingine tano kaziweka kwa bei hiyohiyo na zile nyumba nyingine jirani zimenunuliwa na kina Nyani, Rev. Kiranga na GT nao ni wajumbe wa NEC, sijui Wabunge au ni ndugu wa Rais na Waziri fulani. Kila mmoja wao ana nyumba si chini ya tano ambazo wamezinunua kwa hiyo dola $10,000.00 na wanaziuza kwa dola $100,000.00.

Sasa ni lini NHC iwe shirika la kumjengea nyumba Muuguzi au Njagu?

Mfano wa pili, sakata la kujenga hizi nyumba bora na nafuu, Serikali inadai Manzese na Tandika watu wamejijengea holela, wanavunjiwa nyumba na kupewa fidia kiduchu. Serikali inaipa NHC 60% ya ardhi ya bomoa bomoa ijenge na sehemu iliyobakia wanapewa kina Sailesh Vithlani.

NHC wanajenga nyumba kwa dola $10,000.00 ambazo ni kodi ya mwananchi, na kumuuzia Mama Chiligati kwa dola $ !5,000.00 na yeye Mama Chiligati anaiuza ka Ubalozi wa Kuwait kwa dola $150,000.00!

Ni shirika la nyumba la Taifa hilo ambalo tumeridhia Wizara Mama na Rais waliongoze.

Kama mazao yao yatawanufaisha wengine, kwa nini Watanzania wasinufaike kama umma na wanufaike watu mmoja mmoja?
Linchi limeoza hili kwa ufisadi ...
 
JF ni habari nyingine aisee. Ushauri wangu: tuwe makini sana na maisha yetu ya kila siku especially hii mitandao. Tusijidanganye eti ni upepo utapita. At some point you will be caught!
 
Kwa kuanza tuu napenda niwafahamishe kuwa namfahamu BINAFSI huyu NEHEMIA hivyo sina kinyongo wala matatizo naye if anything nilimfahamisha what to expect alipopewa taarifa ya uteuzi huu miez kadhaa iliyopita.

By definition UFISADI pamoja na kuibia serikali ..tunaweza kusema ni kurudisha maendeleo nyuma na kuwa na upendeleo wa dhahiri kwenye ajira serikalini including NHC!

Nadhani mnakumbuka takriban miezi sita iliyopita nilileta thread ya uteuzi wa DG mpya wa NHC na nikaelezea jinsi uhuni ulivyokuwa umefanywa ili kukidhi profile ya baadhi ya watu. Uhuni huu haukufanywa na mwingine bali IKULU ambako walitoa maagizo kuwa tangazo la awali la nafasi hii iliyotolewa gazetini ibadilishwe...in short tangazo la nafasi ya hii la mwanzo lilitaka mtu mwenye qualifications kem kem baadae tangazo la pili lililotoka likawa limepunzuza sifa za anayetakiwa ...bila maelezo yoyote ile.


Ukweli wa uteuzi huu wa nehemia ni kama ufuatavyo:

1.Nehemia HAKUOMBA kazi hii kama ambayo sheria ilitaka afanye

2. Nehemia hakuitwa kwenye USAILI kama ambavyo sheria ilitaka ifuatwe

3. Nehemia kapata kwa sababu ya presha na ufisadi wa hali ya juu uliyofanywa na Katibu Mkuu wa Ikulu bwana LUHANJO

4. Ambao waliomba na wakaitwa kwenye usaili hawajaandikiwa barua ni sababu zipi walikosa halafu kazi akapewa ambaye hakuomba hiyo kazi in the first place.


Sasa in the wake of haya ya kumsifia Nehemia na mengineyo tusisahau kuwa kuna uteuzi kama huu unaweza kuja kufanywa na rais na nadhani ni muhimu watu wasilalamike kuhusu FAIRNESS kama ambavyo hawalalamiki kuhusu procedures zilizotumika kumpata huyu Bwana NEHEMIA....isije ikawa Mkuki Kwa Nguruwe...

If anything hata kama Luhanjo alikuwa anamtaka kijana wake what was so difficult or worong UTARATIBU ukafuatwa?
Mchechu ,mchechu, hamna kazi za kufanya,you're so busy kumdiscus mwanaume mwenzenu
 
Waberoya,

NHC si shirika la umma tena, si kwa masilahi ya umma wala Taifa, ni kwa masilahi ya Wateule wachache!

Imagine kuwa wewe ni mjumbe wa NEC unakwenda NHC kuomba nyumba, halafu Masanilo Mkulima naye anakuja kuomba kununua nyumba.

NHC kwa kutumia fedha za wananchi imejenga nyumba hii kwa kutumia Dola Elfu kumi ($10,000.00), wanakuuzia nyumba wewe Wabeyora kwa kuwa unafahamika na ni mkubwa kwa Dola elfu kumi na tano ($15,000.00), tena mbaya zaidi kwa kuwa una mamlaka na uzito wa kisisasa na kichama, wanakuuzia hata nyumba tano, kutegemea na mfuko wako na uzito wako.

Masanilo anaambiwa "hatuna nyumba tena, lakini kamwone Waberoya anauza nyumba tuliyomuuzia". Masanilo anakwenda kwa Waberoya anamwambia naipenda nyumba hii naomba kuinunua, Wabeyora anatoa bei, anadai nyumba ile ni Dola laki moja ($100,000.00) na tayari zile nyumba nyingine tano kaziweka kwa bei hiyohiyo na zile nyumba nyingine jirani zimenunuliwa na kina Nyani, Rev. Kiranga na GT nao ni wajumbe wa NEC, sijui Wabunge au ni ndugu wa Rais na Waziri fulani. Kila mmoja wao ana nyumba si chini ya tano ambazo wamezinunua kwa hiyo dola $10,000.00 na wanaziuza kwa dola $100,000.00.

Sasa ni lini NHC iwe shirika la kumjengea nyumba Muuguzi au Njagu?

Mfano wa pili, sakata la kujenga hizi nyumba bora na nafuu, Serikali inadai Manzese na Tandika watu wamejijengea holela, wanavunjiwa nyumba na kupewa fidia kiduchu. Serikali inaipa NHC 60% ya ardhi ya bomoa bomoa ijenge na sehemu iliyobakia wanapewa kina Sailesh Vithlani.

NHC wanajenga nyumba kwa dola $10,000.00 ambazo ni kodi ya mwananchi, na kumuuzia Mama Chiligati kwa dola $ !5,000.00 na yeye Mama Chiligati anaiuza ka Ubalozi wa Kuwait kwa dola $150,000.00!

Ni shirika la nyumba la Taifa hilo ambalo tumeridhia Wizara Mama na Rais waliongoze.

Kama mazao yao yatawanufaisha wengine, kwa nini Watanzania wasinufaike kama umma na wanufaike watu mmoja mmoja?

kitambo sana
 
inaonekana hujasoma thread kuanzia mwanzo, leave head hunting kwenye private sectors not public sectors!, hivi mbona mnapenda kumix kuwa upatikanaji wa wafanyakazi Zain uwe sawa na serikalini? that is public sector!

Whether Nehemia is a right guy or wrong guy hapa haituhusu, swala ni kuwa process (democratic process haikufuatwa) na kwenye public sector wakianza hivi ni hatari, hupo mkuu? acha hadithi za google earth , marekani, kigamboni wapi wapi.. hapa hazipo, don't waste time to talk things like tha,hit to the point. If Nehemia is a right guy is he the best guy? how can you find the best guys in the population of 40 Million?

Can you actually confirm to me that Nehemia is a best and only guy in that position? if not the best how do you get one?? mnataka nchi hii walio kwenye class fulani basi wawe wao na vizazi vyao? hawa wengine nani atawaona au kuwaangalia? mbona wakubwa mnaleta utani na kuwa na double standard kwenye vitu vinavyokinzana na maisha ya 'equal chance-equal opportunity' kwa kila mtanzania

Mwingine unayemfahamu ni Yackoub Kidulla wa NSSF? katika watanzania millioni 40 unawafahamu hawa wawili tu? so nani anafaa TTCL, TRL, Tanesco? nani. Hivi ndugu yangu wengine huwa mnawaza nini wakati mnabonya keyboard zenu? sasa kwa standard yako nani zaidi kati ya Kidulla na Nehemia? na umetumia criteria gani? huoni kuwa unajikaanga mwenyewe? have you forgotten success ya kampuni ni team work? thast why in interview we need one and only one person awe evaluated!!

Ridhiwan Kikwete sio damu mpya?, J. Makamba sio damu mpya? sasa leo hii JK aseme anamweka mtoto wake NHC kwa sababu ni damu mpya inaingia akilini? swala ni uwezo wa mtu whether ni damu mpya au ya zamani ( kama ipo) tukishaweka criteria za uwezo , tunaanza mchakato ambao ni wa wazi, unajulikana , fair, na equal opportunity!

Rudia tena kusoma post zako huone kama zina reflect maisha ya kawaida ya mtanzania, maisha ya wale vijana au raia wanaotafuta kazi usiku na mchana huku wakiwa na uwezo mkubwa kabisa ila wamekosa nafasi, acha kulewa maisha ya kisasa na net pay hizo mkawasahau watanzania jamani, acheni kuleta utani kwenye issue za social classes, post zako hizi zitabaki kukusuta miaka yote ijayo, kuwa katika watu wanaosema social classes ziwepo, walio juu waendelee kuwa juu, walio chini waendelee kuwa chini! wewe humo!aibu hii!

Umezungumzia middle classes? hivi unajua middle class tanzania wanaanzia mshahara gani? hakuna tofauti kubwa ya classes Tz, ila nyie ndio mnataka kuzileta sasa kwa method zenu za vitabuni za kutafuta wafanyakazi kwa head hunting!, NHC should and must be a corporation for all people!

NHC ilipo na inakoenda ni shirika la kitajiri, hiyo middle class unayoisema, manesi, polisi, waalimu hawamo! kwako wewe middle class inaanzia wanaopata net kuanzia laki nane, na ndio wanaoweza kuafford hizo nyumba tena kwa mkopo! Nimejenga nyumba za NHC mbweni (kama mhandisi trainee), I know exactly what I am talking about.

Nehemia ( ambaye hana kosa hapa) ataenda kufullfill nia na mipango ya elite classes, na wale wooote watakaokuwa na uwezo wa kujikomba kwa hao jamaa ili uweze kupata nyumba. NHC mkuu usifananishe na maendeleo ya marekani. NHC should by any how waige South Africa wamefanyaje kwa watu wasio na uwezo kabisa, vijijini na mijini! NHC should not only be in cities/town! otherwise wabadilishe jina na objective!!

Funguka mawazo yawe ya kizalendo zaidi na sio kuzungumza mambo ya vijiweni na kuleta hadithi za watoto wa Msaki na Msasani humu, we need your input, na sio hadithi hizo ambazo huwezi kuzisema popote pale,huwezi ukasema haya mbele ya vijana wanaokaa chini madarasani au wanaohangaika kutafuta ajira kila siku.

Sipandi pantoni kwenda huko, labda uniambe hizo nyumba za Kigamboni nani anaweza kununua? Usiongee kwa confidence buddy, we can even describe hiyo miradi ya Kigamboni kuliko ujuavyo na kukueleza kila kitu in and out , haikuwa kwa manufaa ya umma na haipo. Kama kwako wewe kila kinachong'aa ni dhahabu ni khatari

To me and my stand is sioni ubaya wowote wa Nehemia (Unless tuhuma za EPA akiwa CBA ziwe confirmed) nina dispute process zilizotumika ambazo naona kabisa it is against public interest, it is against human right, it is against democracy, this method is menat for elite people, please leave this to public sectors, head hunting id forbidden in the society that we claim we are equal!

as for NHC should be operated kama South african, for all people kuanzia akina Mengi na maprofessor mpaka Matonya... hii ya sasa ina alarm nyingi sana kuwa linatayarishwa na kama tulivyoliona kwa ajili ya matajiri tu.

Sidhani kama inahitaji debate kubwa , liko wazi kuwa process hazikufuatwa zinavyotakiwa, we have seen the very same kwenye issue ajira nyingine nyingi tu 'nji' hii

miaka 7 baadae! bado NHC haiko kwa ajili ya maskini
 
Pole mchechu. Nakukumbuka ktk ishu ile ya kuwalazimisha wapangaji kulipia huduma za usafi, umeme, walinzi na maji ya kitanzania kwa US Dollar hadi leo hii. Hongera kwa ku side na wabia.
 
Mimi nawaomba sana hao wachunguzi wa Mchechu wasiache kupita kwa wapangaji waliomo ndani ya Golden Plaza Dar, kujisikilizia wenyewe jinsi matumizi ya dollar yanavyolipia wadada wa usafi, walinzi na umeme wa common areas. Chini ya shinikizo la Mchechu. Tena anakwambia kabisaa hutaki nitakufukuza utoke ktk nyumba.
 
This was JF,enzi hizo hizi bundle za bure hazipo, lilikuwa ni jukwaa la aina yake, ulikuwa ukiingia hutoki bila elimu ya maana, huwa natenga nusu saa kila wiki kusoma threads za enzi hizo.
 
for you to be unbiased weka tangazo la kwanza then weka la pili kuonmesha au kujustify hayo unayosema kuwa tangazo la pili qualifikation zilipunguzwa
Unaweza pia ukayatafuta hayo matangazo ili kuthibitisha hisia
 
Back
Top Bottom