[h=2]Kimenuka NHC, Wizara yamweka kitimoto NMK na timu yake[/h]
Asubuhi ya tarehe 2April, 2013 siku ya Jumanne, Bwana NKM amekutana na joto ya jiwe pale ambapo watendaji wakuu wa wizara ya ardhi ambapo wizara inawajibika, walipomtaka yeye na team yake watoe maelezo kuhusiana na kuanguka kwa jengo! Maswali yaliyokosa majibu ni kama ifuatavyo:
1. Kwamba wizara ambayo NHC inawajibika kwake imesikitishwa na kuanguka kwa jengo ambalo NHC wana ubia na kwamba hawakutarajia uchapakazi "unaosifiwa" wa NKM angefanya uzembe wa kiwango kile.
2. Kwamba NHC kwa sababu ndiye mmiliki wa hati ambapo jengo limejengwa, wao ndio walio-apply for building permit, sasa je, waliomba permit ya ghorofa 10 au 16?
3. Kwamba iwe walipewa ya ghorofa 10 au 16, je, wao kama si tu wamiliki wa 25% bali baada ya muda ilitakiwa wamiliki 50% ili iwe 50/50, kwa nini hawakutimiza wajibu wao kama strategic partners?
4. Kwamba inakuwaje NHC ina team ya wataalamu then they just let it go, dancing the tune of the developer?
5. Kwamba hili haliitaji mkataba ukoje, provided walikuwa strategic JV partner, wana la kujibu katika kushiriki kupoteza maisha ya watanzania 36.
Mchapakazi NKM na team yake wamekosa majibu na hivyo kuambiwa aondoke akaandae majibu ya kutosha!
MY TAKE:
Mimi simkubali NKM, na sitamkubali, mbali ya kwamba kuna watu kama Pasco wanamkubali sana, huwaambii kitu.
Kwanza ni mchakato uliotumika kumpata ambao ni kama alipewa tu hiyo nafasi bila ya kumfanyia ushindani ili apatikane na kulinda maslahi ya waliomuweka. Mtakumbuka interview ya kwanza ya PWC ilipigwa chini, ukafanyika uchakachuaji, mzigo ukaamishiwa Ernst &Young, ili kijana apate nafasi!
Baaada ya kuingia NHC, amelifanya shirika kama kampuni ya simu za mkononi ama SUMATRA!
Katika management team yake aliamua kujaza washikaji (Fellow bankers) na watu wake wengine wa karibu huku akiondoa wataalamu waliosomea uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na technical issues za NHC.
Ndio maana nimesema NHC si shirika tu kama kampuni ya simu kwamba alimradi fulani ana degree au MBA can fit in! Haina tofauti na TANESCO ama TANROADS, bora hata ingekuwa SUMATRA! Hebu jiulize NKM ndo angekuwa pale TANESCO au TANROADS halafu akatimua wote technical expects, akaweka his winning team (failing team so to say), hayo mashirika yangekuwaje? Ndo tunayoyaona hapo NHC. Wataalamu wote wa kumshauri kawatupa mikoani.
NKM amejitahidi sana kucheza na media ili kuweka mambo yake sawa! Nyote mnafahamu Yule bwana wa Maisha ni Nyumba ambaye inasemekana yupo kwenye payroll ya NHC.
Watanzania wengi tunapenda kufuata mkumbo na kusifia tu bila kuwa na facts! Mnaosema NKM kalibadilisha shirika, kivipi? Mradi wa Medeli Dodoma umekuwa ni white elephant! Ubungo NHC nao inakula kwake big time, baada ya wengi kulipia downpayments na kuamua warudishiwe pesa zao! Kwa nini? Wengi walikurupuka, ila baada ya kwenda benki(wengi walikuwa wananunua kwa mkopo) na kupigiwa mahesabu ya mkopo, achilia mbali VAT, nyumba zilishoot almost three times asking price! Am afraid the same is going to happen kwa projects za Kigamboni na nyinginezo!
Kuhusu ongoing NHC projects, I can bet na watu kama
Pasco kwamba they are going to be white elephant big time!!!
KWA NINI?
NHC kama shirika la umma, linahitaji kufuata taratibu zote za manunuzi kama inavyotakiwa na PPRA! Sasa nyote mnajua katika utaratibu wa tender system, huwezi shindana na wawekezaji privates kama akina FIDA ambao hawana PPRA na materials wanafuata wenyewe na ku-save a lot! Lakini leo hii NKM anajenga apartments Upanga ati ashindane na wale wawekezaji wengine (private developers? Wapi na wapi? Kwanza wengi wao wana certificate of incentives inayowapa nafuu ya kodi ama kutolipa kodi kabisa! Kibaya zaidi NHC wao bei zao wanauza as per prevailing market rate, kibaya zaidi wanacharge VAT! Nani atanunua za NHC kwa black market iliyopo na imperfections zilizopo katika biashara ya nyumba hapa bongo! Kwa nini nisinunue from other developers?
Narudia, tusitofautishe NHC na TANROADS au TANESCO! Shirika linahitaji wataalamu, na si tu kisa mtu anajua kujipendekeza na kuwa na downloaded presentation hiyo hiyo tu mkamwona kichwa na kumpatia shirika! Hii sio SUMATRA au shirika la bima! Linahitaji technical know how ya product to be traded by a corporation concerned, si technical know who! Nilitegema management team iwe na professionals katika Real Estate pia, achilia mbali watendaji wa chini! Kibaya zaidi hata team yake inapwaya! Huwezi kujaza bankers pale NHC! Ingekuwa TANROADS hayo madaraja yangekatika kila siku au TANESCO ndo ingekufa kabisa, sasa NHC ndo tunayaona leo!!
Mwisho, nimeangalia kiingereza cha mkurugenzi mkuu alipojibu hoja humu JF, dah! Ni kweli kiingereza si lugha yetu, lakini kwa NKM na mbwembwe zake najua pale ka-edit sana kabla yaku-post lakini, wapi!
It is high time uweke mikoba chini mkuu, you don't belong where you are! Your smartness can only be shown now!
Najua wengi mtaniita nina chuki binafsi kama livyo kawaida kwa wengi baada ya kuchanganua kwanza kilichoandikwa wakajenga hoja!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wizara-yamweka-kitimoto-nmk-na-timu-yake.html