Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,080
Siku ya leo jioni kumekuwa na taharuki baada ya watu kuona vitu vilivyopita angani mithiri ya nyota zinazoongozana katika mstari mmoja, wapo waliodhani ni nyota, wapo waliodhani ni vimondo, mpaka waliodhani ni miujiza.
Pia soma > Mliopo Dar es Salaam kuna kitu kinapita maeneo yenu angani
Ukweli ni kwamba hizi zilikuwa ni satelaiti za kampuni ya internet ya starkink inayomilikiwa na Elon Musk.
Internet hii inapatikana hata uwe bondeni, milimani, porini, kijijini, n.k. Internet haina kikomo utatumia unavyotaka (Unlimited), Kuna takribani satelaiti elf 5 za starlink zinazunguka juu ya anga la dunia kuhakikisha internet inapatikana sehemu zote duniani,
Tanzania tulikua moja ya nchi za mwanzo kabisa kuhusishwa na hii internet lakini mpaka leo vibali vinashughulikiwa, Tangu mwaka jana mwezi wa pili Waziri wa Teknolojia, Nnape Nauye amekuwa akisema starlink hawajakamilisha vibali,. >> source <<
Internet hii imepewa vibali nchi nyingi, Nchi jirani zinazofaidi huduma hii ni Kenya, Rwanda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Kwa sasa sisi tutabaki kushangaa hizo satelaiti angani lakini wanaozitumia ni majirani,