Mliopo Dar es Salaam kuna kitu kinapita maeneo yenu angani

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,765
21,239
Kuna kitu sijui naweza kusema ni nini, maana si ndege kwa muonekano wa taa ulivyokuwa mrefu, ila nimeshindwa kuelewa kwa sababu ya giza.

Angani.png


Kimetokea uelekeo wa Bagamoyo kwenda kigamboni, mliopo huko hadi mbagara mnaweza kutujuza au anayeweza kuelewa ni kitu cha aina gani.

Kwenye komenti No. #7 kuna picha mdau wa Arusha Capt Tamar aliwahi kupiga picha, vinatembea kwa mstari kama wale ndege weupe wanaoluka pamoja kwa mstari wakihama wanaopatikana dead lake njia ya Loliondo.

Nawasilisha.

UPDATES:
Baada ya wadau hapa JF kutoa majibu ilikuwa ni kitu gani nimejaribu kufuatilia na kuwasilina na ofisi ya uhusiano ya Space X na wao wakanipa ushirikiano mzuri kuhusiana na hizo kitu.

Kwamba ni kundi la satelaiti bandia zinazofanya kazi pamoja kama mfumo mmoja angalia picha mjongeo hapo chini.


GPS24goldenSML.gif


Hii ni tofauti na setilaiti moja, tunaweza kusema ni kundi nyota ambayo inaweza kutoa utandawazi (globalization) wa kudumu wa kimataifa au kwenye ulimwengu wetu huu.

Hii ni kwamba wakati wowote kila mahali kwenye Dunia angalau setilaiti moja inaweza kuonekana na hizi zinazosaidiana na zile zilizopo anga za juu kuunganisha kwenye vituo vya ardhini vinavyosambaza mawasiliano kimataifa.

Pia soma > Ufafanuzi wa tukio lilotokea jioni ya leo kwenye Anga la Tanzania, Teknolojia inazidi kukuwa, Watanzania tunaachwa nyuma tunabaki kushangaa
 
Ni satelaiti za kampuni ya internet ya starkink inayomilikiwa na Elon Musk.

Internet hii inapatikana hata uwe bondeni, milimani, porini, kijijini, n.k. Internet haina kikomo utatumia unavyotaka (Unlimited)

Elon Musk aliwahi kuja Tanzania kuomba vibali ili alete ofisi zake watanzania tunufaike na hii huduma lakini waziri wetu wa teknolokia Nnape Nnauye alituangusha

Internet hii imesambaa nchi nyingi, Nchi jirani zinazofaidi huduma hii ni Kenya, Rwanda, Malawi, Zambia na Msumbiji. Sisi tutabaki kushangaa na kukodolea macho hizo satelaiti.

Kuna takribani satelaiti elf 5 za starlink zinazunguka juu ya anga hapa duniani, hakuna haja ya mnara ukiwa na starlink, popote duniani utapata intenet, wenzetu wanafaidi teknolojia za kisasa.

1708966292568.png



1708968051321.png
 
Ni kama nyota zinazoongozana kwa mstari mnyoofu, zikiachana kwa nafasi ndogo, zinaonekana zikiwa mbili mbili zilizokaribiana zinaacha nafasi kidogo kisha zinafuata nyingine mbili na kuendelea,tazama picha chini,sijawahi kuona kitu cha namna hii maishani.View attachment 2917366
vitu kama hivi havipati wachangiaji. ngoja iwekwe ngono na siasa uchwara za machawa....watachangia weeeeeeeeeeeeeee mpaka kinyaa!
 
Back
Top Bottom