Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lawa muokozi wa Afrika katika masuala ya sayansi na teknolojia

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1703037558728.png


1703037570585.png


Tangu katika kipindi cha katikati ya miaka ya 1990, China imetambulisha tena sera yake ya Afrika, ikiongeza msaada wake wa maendeleo, na kuyataka makampuni ya China kwenda nje na kuzidisha miradi ya miundombinu. Hata hivyo, sera kabambe ya mambo ya nje ya rais Xi Jinping na pendekezo lake muhimu la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (BRI) vimefanya umuhimu wa China barani Afrika uonekane waziwazi na kujilikana na hata watu wa kawaida. Kwa maneno mengine, BRI imezidi kuinua hadhi ya China na kuwa mshirika anayeaminiwa zaidi na nchi za Afrika.

Ushirikiano kwenye sekta ya sayansi kati ya China na Afrika, unaendelea kuwa moja ya maeneo muhimu ya ushirikiano kati ya pande mbili ambao unaleta mabadiliko makubwa barani Afrika. Kupitia pendekezo hili la Ukanda Mmoja, Njia Moja, China imeshiriki kwa moyo wote katika masuala ya uvumbuzi wa kisayansi na nchi za Afrika kwa kufuata mipango yake mikuu ikiwemo mawasiliano ya kisayansi baina ya watu, kuanzisha maabara za pamoja za utafiti, ushirikiano wa maeneo ya teknolojia na mabadiliko ya teknolojia.

Zamani nchi nyingi za Afrika zilikuwa zikiona kwenye televisheni ama kusikia redioni tu kuhusu teknolojia zinazovumbuliwa katika nchi za nje ama nchi zilizoendelea, lakini kwa sasa teknolojia hizi zimekuwa si jambo geni tena kwa nchi za Afrika, maana nchi nyingi zimekuwa zikishirikishwa kwa njia moja ama nyingine kupitia miradi mbalimbali ya BRI inayotekelezwa na China barani Afrika.

Katika bara zima la Afrika kulikuwa na mataifa machache yanayotumia uwezo wa teknolojia ya satelaiti. Lakini baada ya kuanzishwa ushirikiano huu, ukafanya idadi ya nchi za Afrika zinazomiliki satellite ziendelee kuongezeka, ambapo sehemu kubwa ya satellite za nchi hizi zimetengenezwa na kurushwa kwa ushirikiano na China.

Kwa sasa Misri inaongoza kwa kuwa na satelaiti tisa katika obiti, ikifuatiwa na Afrika Kusini (nane), Algeria (saba), na Nigeria (sita). Na nyingine ni pamoja na Morocco, Ghana, Kenya, Rwanda, Angola, Sudan, Ethiopia na Mauritius nazo pia zimejiunga katika kurusha satellite zao anga za juu.

Teknolojia ya anga za juu ni jambo moja tu, lakini tukigeukia upande wa TEHAMA inaonekana kwamba Afrika sasa inakwenda sambamba na nchi za mabara mengine na imepiga hatua kubwa sana. Kampuni ya Huawei ya China ambayo inafahamika kwa ukubwa wake kwenye teknolojia imekuwa mshirika mkubwa wa miradi ya teknolojia ya China barani Afrika, ikisaidia nchi hizi katika kupanua Mkonga wa Taifa wa Mwasiliano, na kurahisisha huduma ya mawasiliano ya internet.

Mingoni mwa nchi zinazojivunia uwepo wa Huawei katika Afrika ni Tanzania. Huawei imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kukuza ubora wa elimu ya TEHAMA ambayo inaongeza ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania, kupitia programu yake ya “Seeds for the Future”. Mipango mkubwa ya Huawei ni kuiwezesha Tanzania kukabiliana na mahitaji ya teknolojia kidijitali ambayo yanabadilika mara kwa mara. Aidha ni hivi karibuni tu Shirika la simu Tanzania (TTCL) lilisaini mkataba na kampuni hii ya Huawei kwa ajili ya kupanua Mkonga wa Taifa wa Mwasiliano (NICTBB) hadi kufika katika wilaya 23 nchini humo.

Eneo jingine ambalo nchi za Afrika zinanufaika na Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja kwenye masuala ya sayansi ni uchumi wa kidijitali. Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Bw. Zhang Xiangchen amesema, katika miaka ya hivi karibuni, licha ya kufufuka polepole kwa uchumi wa dunia, nchi nyingi zaidi za Afrika zimetumia uchumi wa kidijitali kama chachu nyingine ya kukuza maendeleo.

Baadhi ya tafiti ukiwemo uliofanywa na taasisi ya ushirikiano wa kidijitali (DCO) zinaonesha kuwa uchumi wa kidijitali utachangia asilimia 30 ya pato la duniani huku ukiongeza ajira milioni 30 zaidi. Kwa barani Afrika uchumi wa kidijitali unatarajiwa kufikia thamani ya dola bilioni 712 ifikapo mwaka 2050. Na hivi sasa Pato la Afrika ni dola 3.1 trilioni na dijitali inachangia bilioni 200.

BRI imesaidia sekta mbalimbali za Afrika katika ukuaji huo wa kidijitali zikiwemo sekta ya kilimo ambayo inatumia teknlojia za kisasa kutoka China, viwanda, usafirishaji, masoko mitandaoni na kutumia suluhu za kidijitali katika nyanja zote za kiuchumi ikiwemo akili bandia. Kwa maana hiyo ari waliyonayo Waafrika ya kushirikiana na kutafuta suluhu za kiuvumbuzi na China, bila shaka itawasukuma na kuweza kupata mafanikio ya kushangaza katika safari yake ya kutafuta maendeleo ya bara.
 
Back
Top Bottom