Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Kudos Maranya; afterall what is in a name?! Mimi nilisoma A level Mkwawa zama hizo na mtu akiitwa MSAKANJIA MKATAKONA lakini jina hilo la kiaina halikumzuia kupiga principals zake 3 na kuendelea na chuo kikuu! Masalia Shonza na genge lake anamfahamu JENERALI ULIMWENGU?! pen name yake haijamkosesha utu wala heshima ndani ya taifa letu
Chapa kazi John Suguta; Masalia wanalia machozi ya samaki ambayo huwa hayaonekani mpaka azame ziwani!!
 
Mwita Makabila na majina ya ukoo yako chadema tu?Jana tu nimefafanua jambo hili bado unanukuu. Madelu sio jina halisi la baba bali ni jina linalotambulisha kuwa ana ndevu nyingi. Alifunga ndevu sana akiwa kijana akawa wanamwita madevu kinyiramba madelu. Lameck ni jina la mganga nililopewa siku ya kwanza nilipopelekwa clinic baada ya kuzaliwa nyumbani mwigulu ama mgulo ndio majina ya babu niliyopewa tangia nazaliwa mchanga.Nenda waulize vizee mgulo/ mwigulu utajua. Hivi tangu lini jina limekuwa tatizo? Mbona mobutu seseseko aliyabadili yote ? Nitakwenda kuapa niachane na Yote haya nijiite nitakavyo na sheria inaruhusu kujiita Muhamad Yesu
 
Hayo majina officially ni issue kubwa sana hasa kwa upande wa signatory na nyaraka mtu mmoja hauwezi ukawa na majina sita ili iweje sasa? Mimi sio mwanasiasa and i hate politics.
 
Niliposoma tu ile makala ya utetezi ya Bi Juliana Shoza huku nikijua ni msomi wa chuo kikuu nilihisi haraka sana ile kitu ya majina tofauti ya John Heche imepikwa, kama ilikua na ukweli wowote, mwandishi au mtoa shutuma akiwa ni msomi, nilitegemea angeonesha pia wapi huyu bwana ali Cook hayo majina, hadi mwisho wa makala yake sikuona then nikajua aidha hana ushahidi au kafanya makusudi kuposha jamii au alifanya vile ili John Heche mwenyewe aje ajibu na waanze kukosoa kwakusema ni wapi tulipokutumuhu kwamba unatumia jina la mtu? Bahati mbaya mtego wake umeferi vibaya tena, RIP kisiasa bi Juliana.
 
Mwita Makabila na majina ya ukoo yako chadema tu?Jana tu nimefafanua jambo hili bado unanukuu. Madelu sio jina halisi la baba bali ni jina linalotambulisha kuwa ana ndevu nyingi. Alifunga ndevu sana akiwa kijana akawa wanamwita madevu kinyiramba madelu. Lameck ni jina la mganga nililopewa siku ya kwanza nilipopelekwa clinic baada ya kuzaliwa nyumbani mwigulu ama mgulo ndio majina ya babu niliyopewa tangia nazaliwa mchanga.Nenda waulize vizee mgulo/ mwigulu utajua. Hivi tangu lini jina limekuwa tatizo? Mbona mobutu seseseko aliyabadili yote ? Nitakwenda kuapa niachane na Yote haya nijiite nitakavyo na sheria inaruhusu kujiita Muhamad Yesu

Ndugu Mwigulu Nchemba huna sababu ya kupanic kiasi hicho.
Katika maelezo yangu sijasema hayo ni majina ya Chadema bali nimezungumzia majina ya kikurya sijui kama unaelewa hapo. Wakurya wapo Chadema, wapo ccm, wapo tlp na kwingineko. Na pia nimezungumzia kwamba na makabila mengine yanaweza kuwa na utaratibu kama wetu, kwahiyo nimejikita kuongelea kabila langu na sijaongelea wanyiramba ama wanyaturu.

Lakini pia unafahamu kuna thread hapa JF inayozungumzia utata wa jina lako na mimi niliwahi kukusihi uitafute na kuitolea ufafanuzi lakini sikuwahi kukuona ukifanya hivyo, sasa hapo ujilaumu mwenyewe kwakuwa umepata platform ya kuweka kumbukumbu sawa sawa lakini kwa makusudi ama kutojua/kutojali umeacha kuitumia.

Kwa mfano wako wa mobutu ndio unasadifu majina ya John Heche Suguta unaweza kumuita Wegesa Heche Suguta, na hiyo haijawahi kuwa tatizo hadin pale ccm mlipoanzisha siasa za ,majitaka dhidi ya majina ya watu ndipo sasa wananchi nao wameanza kuwahoji na kuona kama ni hoja ya msingi.
 
Last edited by a moderator:
Mwita Makabila na majina ya ukoo yako chadema tu?Jana tu nimefafanua jambo hili bado unanukuu. Madelu sio jina halisi la baba bali ni jina linalotambulisha kuwa ana ndevu nyingi. Alifunga ndevu sana akiwa kijana akawa wanamwita madevu kinyiramba madelu. Lameck ni jina la mganga nililopewa siku ya kwanza nilipopelekwa clinic baada ya kuzaliwa nyumbani mwigulu ama mgulo ndio majina ya babu niliyopewa tangia nazaliwa mchanga.Nenda waulize vizee mgulo/ mwigulu utajua. Hivi tangu lini jina limekuwa tatizo? Mbona mobutu seseseko aliyabadili yote ? Nitakwenda kuapa niachane na Yote haya nijiite nitakavyo na sheria inaruhusu kujiita Muhamad Yesu
halafu unajiita first class degree holder,.katubu kwa dhambi ya kusafiria jina la mtu mwingine,ndio maana hatuendelei kwa kuwa na watu waliofoji mtihani kama wewe..
 
Ebu tupr hesabu wale Twiga,Tembo jumla yao ilikuwa ngapi. Meno ya tembo iliyokamatwa Hongkong ni nani alihusika. Achana na haya ya Shoza tuangalie yale yanayoumiza wananchi waliowengi. Hivi wale wenye account uswizi ni akina nani na ni wa chama gani. Huyu mzee wa rada ivi ni kada wa cdm. Na zile pesa alizoweka south africa huyu aliyekuwa sijui mkuu wa majeshi je yamerudishwa?
hahahahahahah!!!!! Mi huwa mnifuraisha sana mnavyojibu hoja zinazoelekezwa kwenu!!!!!Sasa unaniuliza hayo maswili mimi kama nani? Mimi sio raisi, mimi sio waziri wala katibu wa wizara yeyote am just a a local Tanzanian citizen and a student of one of the university in tz, hebu acheni kujibu hoja kitoto kwamba wewe umenisema na mimi nakusema, kama kijana mpenda demokrasia na siasa za hoja kujibiwa kwa hoja nlitaka kujua majibu yenu ya hoja za Shonza si kuelezea majina wakati Shonza hajahoji majina! Japo bado Heche yupo wrong kutumia unofficial name katka official document bila kuapa mahakaman japo majina aliyoyatumia ni yake!Sasa kwani hapo kutakuwa na tofauti gan kati yake na wasanii wa sanaa?! Maana wasanii wa sanaa ndo huwa wanatumia majina yoyote wanayojisikia na jamii haiwahoji.Narudia tena hebu jibuni hoja za Shonza kwa kutuelezea vifungu anavyolalamikia kuwa vimekiukwa bila kusahau kutoa sababu kwanini yeye (Shonza) aliadhibiwa na Mamuya akaachwa wakat wote hawakuattend kikao?
 
Majina WEGESA SUGUTA aliyotumia Juliana Shonza katika taarifa yake kwa vyombo habari akimaanisha ni jina la John Heche limeanza kuleta mjadara katika mitandao ya kijamii. Wapo wanaohisi kuwa yawezekana akaingia katika kashfa ya majina kama Mwiguru Nchemba (Lameck Mkumbo), Philipo Mulugo (Amimu Agustino), Khamis Kigwangala (Nassoro Bagaire) etc.
Yaezekana kipo kitu kilichojificha nyuma ya jina hili, lakini naomba nitoe uzoefu wangu katika masuala ya mjina kwa watu wa kanda ya ziwa hasa kwa Mkoa wa Mara na wilaya ya Ukewe.
Katika maeneo niliotaja hapo juu ni nadra sana kukuta mtu ana jina moja. Kwa mfano mimi nilipozaliwa Mama yangu aliniita MAJULA, anasema hili ni jina la ulezi yaani la kulelea, kisha nikapewa jina MABELE, hili ni jina la kurithi. Mabele alikua babu yake na baba. Nilivyobatizwa nikaitwa MARTIN. Pia jina langu lingine ni MKAIMA, mtoto yeyote wa kiume kwenye ukoo wetu huitwa jina hili. Mara nyingi ukiitwa jina hili basi umeheshimika sana au mtu emefurahi kukuona.
BABA yangu alipozaliwa aliitwa MALIMA, hili ni jina la uliezi, Alivyobatizwa akaitwa SELESTIN. Pia alipewa jina la kurithi MABELE. Kijijini kwetu baba yangu anafahamika kwa jina la utani la NYANGAJO. Na mimi kijijini kwetu nafahamika sana kwa jina langu la urithi la MABELE. Wale niliokua nao huku mjini wananifahamu kwa jina la MAJULA. Mzee wangu kazini alikua anatumia Selestin Malima Masyenene (Masyenene ni jina la baba yake, yaani babu yangu)
Kwa hiyo ukikutana na mtu akakwambia mimi naitwa MABELE NYANGAJO au MAJULA MALIMA au MAJULA MASYENENE unaweza kuzani Martin M Malima (Martin Majula Malima) nimeiba.
Sina nia ya kumtetea Heche, lakini uwezekano wa yote kuwa majina yake ni mkubwa. Ila yeye (Heche) ndio anaweza kujisemea. Mimi nimetoa uzoefu tu wa watu wa Msoma na Ukerewe.
 
Mkuu Martin Majula Malima hii issue tayari nimeitolea ufafanuzi wa kina kabisa jana, tafuta thread hiyo utaona clarification iliyojitosheleza.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kimbunga heri ya mwaka mpya. Ulikuwa umejificha wapi mkuu hatujaonana tangu mwaka umeanza.
Sasa mkuu unataka kuniambia hii post hujaiona, hujaisoma ama hukuielewa?

Ndugu yangu Chasha ahsante sana kwa ufafanuzi wa hoja. Tuko pamoja sana Poti, kidogo kidogo hadi watatuelewa tu.

Mku Mwita nipo imara na mwaka huu nimeuona kwa mapenzi yake Jalal. Mkuu hiyo post nilikuwa sijaisoma. Kwa maana hiyo ni kwamba Heche alipewa jina la Wegesa kwa sababu maalum; labda kumuenzi bibi yake kama ambavyo ukoo wenu unamuenzi Mogesi?
 
Hii imeeleweka tena vizuri tu, ambaye hajaelewa atakuwa tu kaamua kutoelewa ili kendeleza ligi isiyokuwa na ubingwa.
 
Back
Top Bottom