Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Ufafanuzi: Majina John Heche Vs Wegesa Suguta

Maskini Juliana hana pa kushika mh" yote hii kisa u first lady jamani!!!!!!
 
Wakurya wana kawaida ya kurudia saana darasa la saba hadi anapofaulu kwenda sekondari ya serikali. Nilidhani ndio yaliyomkumba John Heche a.k.a Julius Malema wa CHADEMA.
 
nilisoma na john heche kwa majina haya ya john charles heche.nashangaa kuona hapa kuwa eti alisomea majina mengine hapana wagesa suguta atakuwa ni
mtu mwingine
 
nilisoma na john heche kwa majina haya ya john charles heche.nashangaa kuona hapa kuwa eti alisomea majina mengine hapana wagesa suguta atakuwa ni
mtu mwingine

Tatizo watu humu wanatumia Tumbo kiuwaza, Mara John Heche sio jina lake na la kwake ni Wegesa,. sasa hao ndugu zake na wao wameiba majina? so ukoo mzima wameiba majina
 
Kamanda umetoa ufafanuzi mzuri na wa kueleweka.

Masalia wana kazi. Wakishatumika na mafisadi mwisho wake ni kutupwa chooni kama toilet paper
 
Ngoja niingie facebook nimtafute huyo Juliana Shonza ni test Zali. Haaa!
 
Mi nilishawambia, mfa maji huwa haachi...................atataka kushika kila kitu, Oh mara Slaa, mara Mbowe mara Heche oh mara Suguta wapi wewe? Aje tena sasa kanakurupuka tu cjui kaliamka kakasahau kuoga na kuanza kuandika hovyo kama kamo ndotoni. Sasa mmekubali kwamba Mbowe hakukosea aliyesema Kashonza kana hoja za kitoto na Dr. Mkumbo aliyesema hakajabalee kisiasa. Kaje tena sasaivi kakirusha kofi sisi tunapiga ngumi, karirusha ngumi tunarusha bomu, tuone sasa.
 
Ndugu wanaJF,

Nimelazimika kuanzisha thread hii kwa lengo moja tu la kutoa ufafanuzi juu ya upotoshwaji wa jina la mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema unaofanywa na kundi la masalia kwa sababu maalum.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.

Bila shaka ameamua kufanya hivyo kama muendelezo wa tuhuma walizozianzisha kundi la masalia kwa kutumia ID yao ya kundi ya Tuntemeke kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Hili kundi la PM7 linataka kumuonyesha John Heche kwamba naye amegushi jina kama walivyo baadhi ya viongozi wakubwa huko ccm (wafadhili wao). Mathalani imetajwa mara kadhaa kwamba miongoni mwa watu wanaotumia majina ya kugushi huko ccm ni pamoja na Naibu katibu mkuu bara Bw. Mwigulu Nchemba (Lameck Madelu?) na Dr. HKigwangalla (Saidi Bagaile?) ambao wanadaiwa kutumia majina ya bandia.

Sasa nirudi kwenye hoja ya msingi. Kawaida sisi wakurya hata kama umezaliwa mjini ama katika mazingira ya mbali na nyumbani/kijijini lazima unapewa jina la kikurya, kwahiyo kwa wakurya wengi wanakuwa na majina mawili ama matatu lakini yote yakiwa ya mtu mmoja.

Kwa mfano mwalimu Nyerere, majina yake ni Julius Kambarage Nyerere(Julius jina la kikristo). Kuna mwanae Charles Makongoro Nyerere (Charles jina la kikristo), kuna Dr. James Mnanka Wanyancha-mwenyekiti wa Road Fund (James jina la kikristo), Marehemu Jenerali Ernest Mwita Kyaro (Ernest jina la kikristo), Jenerali mstaafu George Marwa Waitara (George jina la kikristo. Nadhani kwa kutaja hao wachache mnaweza kuona scenario ya majina ya kikurya, naamini kuna makabila mengine yenye utamaduni kama wa kwetu.

Sasa nije kwa John Heche Suguta:
Jina lake la kikurya ni Wegesa na baba yake mzazi anaitwa Heche Suguta. Wegesa Heche Suguta jina lake la kikristo ni John, ndipo sasa unapata John Heche Suguta. Jina la kikristo la baba yake John Heche (Heche Suguta) ni Charles, ndipo sasa unapata Charles Heche Suguta.

Katika vyeti vyake vya shule John Heche anatumia jina la Wegesa Charles Suguta (Wegesa Suguta). Aliandikishwa shule kwa jina la Kikurya na akaendelea kulitumia katika harakati zake zote za kishule. Ndugu zake na John Heche ni pamoja na Bw.Manchare Heche Suguta (Mwanasheria NEMC), Chacha Heche Suguta (M/Kiti Bavicha Tarime) na Mome Heche Suguta (Tarime) kwa kutaja wachache ambao angalau wanafahamika na watu wengi.

Nimalizie kwa kuwajulisha masalia kwamba kama mnadhani mnaweza kumchafua Bw. John Heche kwa staili ya majina basi nawashauri msahau kwakuwa watu wote waliokua nae toka utotoni Tarime, shuleni alikosoma sekondari ya Bulima (O level), Musoma Alliance (A level), Bunda TTC na hatimaye SAUT Mwanza wanamfahamu sana John Heche kwa majina yote mawili.

John Heche aligombea na kushinda kiti cha udiwani Tarime mjini mwaka 2008 katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Chacha Wangwe, kwa kumshinda mbabe wa Tarime Bw. Peter Zakaria. Wakati huo alikuwa mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu augustino (SAUT) Mwanza. Kama angelikuwa anatumia majina ya bandia ama majina ya mtu mwingine bila shaka hilo lisingejificha wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baada ya kusema hayo nadhani nime-clear doubts zilizokuwa zimeanza kujitokeza kwa baadhi ya watu hapa JF.

Nawatakia jioni njema.

Kinachosumbua Chadema ni uelewa mdogo tu, Mfano; Shonza hakusema kuwa John H. ametumia jina la mtu mwingine bali alikuwa analiweka jina la Wegesa Suguti kwenye mabano kama kuonyesha anajua majina yake yote. Lakini nashangaa wanaChadema wanakuja kusema amekurupuka, je majina aliyoyaandika hayamhusu John Henche?. Mimi nilifikiri wangekuja na agender ya kukuataa jina la Wegesa Suguti ndo Juliana Shonza angeonekana kakurupuka. Hii ni sawa na kuulizwa jina la Chama chenu unajibu Siasa badala ya Chadema. Shuleni hasa kuanzi Msingi hadi O-Level huwa Mwanafunzi anashauliwa asome maswali yote kwa umakini ndipo aanze kujibu kwanza anayoyaweza, maana yake ni nini unaweza kukuta umeambiwa usijibu swali lolote wewe ukaona Mwalimu amekutungia maswali rahisi ukajikuja kujibu kumbe umekosa na kuanza kumraumu Mwalimu kwa kukukosesha na wakati umepata. Tunashukru umetoa ufafanuzi wa jina la John na Wegesa, je hao unaowaita masalia walihoji hayo majina au wewe ndo umekurupuka?.
 
Wahi lumumba muda huu.
 
Ukirudia darasa la saba ukabadili jina
Ukifika fomu wani unatakiwa kuomba kubadili jina utumie lako la zamani

Ukisahau kufanya hivyo, Shonza anasema hadharani
Kongosho Kumbe hujaielewa thread yangu na ufafanuzi wote nilioutoa. John Heche Suguta ndiye huyo huyo Wegesa Heche Suguta, hakuna issue ya kurudia shule.
 
Last edited by a moderator:
Kinachosumbua Chadema ni uelewa mdogo tu, Mfano; Shonza hakusema kuwa John H. ametumia jina la mtu mwingine bali alikuwa analiweka jina la Wegesa Suguti kwenye mabano kama kuonyesha anajua majina yake yote. Lakini nashangaa wanaChadema wanakuja kusema amekurupuka, je majina aliyoyaandika hayamhusu John Henche?. Mimi nilifikiri wangekuja na agender ya kukuataa jina la Wegesa Suguti ndo Juliana Shonza angeonekana kakurupuka. Hii ni sawa na kuulizwa jina la Chama chenu unajibu Siasa badala ya Chadema. Shuleni hasa kuanzi Msingi hadi O-Level huwa Mwanafunzi anashauliwa asome maswali yote kwa umakini ndipo aanze kujibu kwanza anayoyaweza, maana yake ni nini unaweza kukuta umeambiwa usijibu swali lolote wewe ukaona Mwalimu amekutungia maswali rahisi ukajikuja kujibu kumbe umekosa na kuanza kumraumu Mwalimu kwa kukukosesha na wakati umepata. Tunashukru umetoa ufafanuzi wa jina la John na Wegesa, je hao unaowaita masalia walihoji hayo majina au wewe ndo umekurupuka?.

Wewe ni "mulisya" wala huwezi kuwa tata mura kwa akili matope kama hii. Siku nyingine ujitahidi kufungua akili yako ili uelewe kinachoajadiliwa kuliko kukurupuka na kuandika utumbo.
Pamoja na kui-quote thread yangu lakini bado tu hujaelewa chanzo cha mimi kutoa ufafanuzi huu. Soma hapo niliandika nini.

Mwishoni mwa mwaka jana TUNTEMEKE aliwahi kuibuka na madai kama haya kwamba John Heche anatumia cheti cha ndugu yake, na kwamba hakuwahi kusoma chuo kikuu cha mtakatifu augustino (SAUT) cha mwanza. Leo tena katika thread iliyoanzishwa na mwanamasalia aliyetimuliwa Chadema bi. Juliana Shonza amejitahidi sana kutumia jina la Wegesa Charles Suguta ama Wegesa Suguta.
 
Last edited by a moderator:
Mwita Maranya, Heche ni ndugu yako mbona unajifanya unamjua sana. tata mura, kakufahamisha vizuri lakini unaleta ubishi.
 
Last edited by a moderator:
duh! kumbe huyu Mwita Maranya ndo john heche aka Wegesa Charles Suguta.tutaanza kuwajua mmoja baada ya mwingine
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom