Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

kwa hapa lazima nimtetee lowasa. aliyeteleza ni yule kiongozi wa ccm aliyechochea jambo dogo kama lile...
Acha kujitoa ufahamu. Unaona kusema "tangu nchi hii iumbwe haijawahi kuwa na rais mlutheri. Nyerere alikuwa Mkatoliki na Mkapa alikuwa Mkatoliki." Alikuwa sahihi?
Haimaanishi walutheri wasimchague Maguguli kwa sababu sio Mlutheri bali Mkatoliki?
Magufuli nae akiwaambia Wakatoliki wenzake nichagueni mm kwa sababu mimi ni Mkatoliki mwenzenu; itakuwaje?
Wagombea wenza nao wakiwahamasisha wapiga kura kwa imani zao matokeo yatakuwaje?
TUTAFAKARINI SOTE.
 
Hebu ngoja tuwaulize hao maccm kati ya kauli hizi ni kauli zipi ambazo hakika zinaweza kulibomoa Taifa letu.

Kauli no. 1 ni kauli iliyowahi kutolewa na uvccm ya mkoa wa Pwani ikitolewa na spokesperson wao Riz-One kuwa kamwe Rais hatokuja kutoka mikoa ya kaskazini.

Kauli no. 2 ni iliyotolewa na Nape kuwa CCM ni lazima ishinde hata kama italazimika kushinda kwa goli la mkono.

Linganisha kauli hizo 2 za wanaccm 'wazito' na kauli ya EL kuwa nawaomba kura zenu wakristo wenzangu endapo tu mtaona ninafaa kuliongoza Taifa hili, tena kauli hiyo akiitoa kanisani kwenye ibada ya Jumapili alipokwenda kuabudu.
Nafikiri na wewe unapotosha., nikisoma melezo hapo juu ya Lowassa na clip iliyosambazwa jana humu, hakuna sehemu aliyosema anaomba wakristu wenzake wampigie kura. Alichosema ni wamuombee - na labda kinachotia ukakasi ni kueleza kuwa walutheri hawajapata kuwa Rais wa nchi hii na hivyo akasisitizia walutheri wamuombee sana. Hii ndiyo inayotafasiriwa kuwa anaomba kura za walutheri! Ajabu ni kuwa mtu huyu mkewe ni Mkatoliki, kwahiyo mama naye atakwenda kwa Wakatoliki ili awaombe wampigie kura mmewe ili yeye awe first lady!
 
ni kweli kabisa na ushaidi wa video upo...udini sio kitu kizuri hivi dini nyingine zitamfikiriaje...ni dhambi kubwa kwa mheshimiwa lowassa aungame kwa mungu

Chama chake "kilimtakasa" kwa yale ya awali, na hili pia kitamtakasa.
........ wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii kwa sababu imefanywa migumu mioyo yao ......
 
Usinisee... Anakonipeleka ndipo. Nitamchagua Lowassa kwasababu anafaa kuwa kiongozi wangu. Hata kama Lipumba angeteuliwa and UKAWA ningempa kura yangu kwani ninaamini katika mabadiliko chanya.

Poleni maccm kwa propaganda nyingine iliyofail kabla hata hamjaanza kuitumia....
Huna hoja..kaa chini.
 
Mzee wetu kateleza tukubali ukweli ingawa unauma.
 
huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya ukawa kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la kilutheri huko tabora. Nanukuu...

"kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." mwisho wa kunukuu.

lowassa kwisha habari yake!!
 
Mzee wetu kateleza...ingawa ukweli unauma.
 
Mwenyekiti wa CCM Geita kasema sasa ni zamu ya kanda ya Ziwa si nongwa.
 
Mzee mm nampenda sana namkubali sana tu ila hapa ameteleza pengine inafaa awe anaandaliwa kwa maandishi cha kusema mbele za watu
 
Ameteleza wapi?! Au kuwaomba waumini wenzake wamuombee ndio ishakuwa kosa?

Hivi Nyerere aliposema hatutamchagua mtu kwa ukristo wake hukumuelewa..!!! yaani kwasababu waliotangulia walikuwa wakatoliki..sasa ni zamu ya lutherani. na sabato je..moravian..assemblies nao. orthodox je ?
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

hakuna deen wala Imani yeyote inayo kuletea pilau!
 
Keshaomba radhi lkn

Unajua LEBANON walianza hivihivi. madhehebu yamegawana madaraka mpaka kwenye katiba. lakini vita ipo palepale.
Askari wetu wa JWTZ wapo huko wanalinda usalama.huu mwaka wao wanane.
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.
Hakuna kosa, charity begins at home, hata mimi ningekuwa mgombea ningeanza kuomba kura kutoka kwangu mwenyewe, mke wangu, watoto wangu, familia yangu, ndugu zangu, rafiki zangu, mtaa wangu, kijiji changu, kata, wilaya, mkoa, chama changu, kanisani kwangu, dhehebu langu, dini yangu, wanaume wenzangu, rafiki za mke wangu na mwisho ndo ningeomba kura kutoka kwa watanzania wote mabibi na mabwana popote walipo. Sasa kwenda kuwaomba kura waumini wenzako kura kuna ubaya gani? Kinachotakiwa hapa ni kutoa majibu kwa wananchi kwanini hawana maji, dawa, barabara, umeme, ni maskini, elimu mbovu, n,k kwa miaka 54 ya uhuru basi, sio kupiga chenga za dini wala nini.
 
Back
Top Bottom