Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.
 
HAMY-D umekuwa siku hizi mkuu,hongera!!

Kama hayo ndio aliyonena basi maCCM yanapandikiza na kukuza Maneno ya kinafiki tu!!

Nani asiyejua kuwa maCCM ndio yaliyopanda mbegu ya udini Tanzania na wakaupalilia na kuuwekea mbolea awamu hii ya Kikwete??!! Safari hii sijui watawalagai na nini waislamu maana wagombea wote wakristo!!!
 
Last edited by a moderator:

Maccm yanajaribu kila njia kupiga propaganda ili mradi tu wahakikishe azma ya Umma wa watanzania kufanya mabadiliko kupitia Ukawa inashindikana.

Hata hivyo wanachosahau wao ni kuwa linalopangwa na Mungu, binadamu hata afanyeje hawezi kuupangua mpango wa Mungu.

Watambue kuwa kila kinachotokea kuelekea uchaguzi mkuu kinafanyika kwa mapenzi ya Mungu.

Maccm wakumbuke hata huo muungano wa vyama kupitia Ukawa ni mpango wa Mungu baada ya kuwatia upofu na uziwi na kiburi cha kutotaka kukubaliana na maoni ya wananchi yaliyokuwemo kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba.

Upofu na uziwi mwingine ambao Mungu aliwapa maccm ni katika mchakato wa kumpata mgombea wao wa Urais, ambapo napo walipuuzia maoni ya wanaccm wengi ambao chaguo lao lilikuwa EL.

Sasa baada ya Ukawa kuona jiwe lililokataliwa na waashi na kulifanya jiwe lao kuu la pembeni, maccm hao hao tena wameendelea kuweweseka na kumfanyia propaganda zisizoisha huyo mtu waliyemuita kapi na oil chafu!

Hivi kama kweli Lowassa ni kapi, oil chafu na majina mengine mengi mabaya waliyompa Sisiem, hivi ilikuwaje hao hao Sisiem wamuundie timu ya watu 32 kupambana na huyomtu mmoja ambaye ni kapi hadi hivi sasa wamemuongeza mchezaji mwingine ambaye wamemvalisha jezi no. 33 ambaye ni Dr mla Mihogo?

Kwa kweli maji yamewafika shingoni magamba, kwa kuwa weshaona dalili zote za namna Umma wa watanzania ulivyojipanga kikamilifu kutumia 'vichinjio' vyao kwa maana ya vitambulisho vya kupigia kura 'kuwachinjilia' kwa mbali Sisiem kwa kupitia sanduku la kura ifikapo Oktoba 25 ya mwaka huu.
 
Last edited by a moderator:
CCM kweli wameishiwa. Jana wakati ninaangalia taarifa ya habari ya SAA 2:00 ucku nilimuona Mzee Makamba mishipa ya shingo imemtoka,sauti imekauka kwa kujikamua. Ooooh! Udini Udini" Udini uko wapi hapo?! Mbona kila kitu kipo waazi tu.
Walikuja na santuri ya Richmond. Imebuma
Wakaja na Mwakyembe. Amebuma
Wakaja na Dk Slaa. Amebuma
Sasa wanamalizia na Udini. Pia Umebuma.
Watanzania wanachohitaji ni maji,Elimu bora,Ajira kwa vijana,Umeme wa uhakika,Barbara za uhakika sio zinazojengwa Leo kesho zinanza kubonyea halafu inasingiziwa mipira pamoja na mambo meengi ya kimaendeleo. Wao wanachotaka ni kiongozi ambaye atasimamia maendeleo kwa spidi ya ajabu. Baaasi.
Hayo mambo ya dini wanawaachia wazeee kama Makamba ambao yao yanawaendea. Lakini wale choka mbaya wao wanataka mipango mkakati ya kuwanasua na umasikini tuu!!
 
Hatuta chagua mtu kwa u-lutheri wake au u-katoliki wake au u-sunni wake. Kubali umeteleza. na unakotupeleka siko.

Ameteleza wapi?! Au kuwaomba waumini wenzake wamuombee ndio ishakuwa kosa?
 
Angesema tu wamuombee basi......hii ya kusema ulutherani wangine watakuja na hoja ya kutaka Rais Msabato
 
Hebu ngoja tuwaulize hao maccm kati ya kauli hizi ni kauli zipi ambazo hakika zinaweza kulibomoa Taifa letu.

Kauli no. 1 ni kauli iliyowahi kutolewa na uvccm ya mkoa wa Pwani ikitolewa na spokesperson wao Riz-One kuwa kamwe Rais hatokuja kutoka mikoa ya kaskazini.

Kauli no. 2 ni iliyotolewa na Nape kuwa CCM ni lazima ishinde hata kama italazimika kushinda kwa goli la mkono.

Linganisha kauli hizo 2 za wanaccm 'wazito' na kauli ya EL kuwa nawaomba kura zenu wakristo wenzangu endapo tu mtaona ninafaa kuliongoza Taifa hili, tena kauli hiyo akiitoa kanisani kwenye ibada ya Jumapili alipokwenda kuabudu.
 
Maccm yanajaribu kila njia kupiga propaganda ili mradi tu wahakikishe azma ya Umma wa watanzania kufanya mabadiliko kupitia Ukawa inashindikana.

Hata hivyo wanachosahau wao ni kuwa linalopangwa na Mungu, binadamu hata afanyeje hawezi kuupangua mpango wa Mungu.

Watambue kuwa kila kinachotokea kuelekea uchaguzi mkuu kinafanyika kwa mapenzi ya Mungu.

Maccm wakumbuke hata huo muungano wa vyama kupitia Ukawa ni mpango wa Mungu baada ya kuwatia upofu na uziwi na kiburi cha kutotaka kukubaliana na maoni ya wananchi yaliyokuwemo kwenye Rasimu ya Tume ya Warioba.

Upofu na uziwi mwingine ambao Mungu aliwapa maccm ni katika mchakato wa kumpata mgombea wao wa Urais, ambapo napo walipuuzia maoni ya wanaccm wengi ambao chaguo lao lilikuwa EL.

Sasa baada ya Ukawa kuona jiwe lililokataliwa na waashi na kulifanya jiwe lao kuu la pembeni, maccm hao hao tena wameendelea kuweweseka na kumfanyia propaganda zisizoisha huyo mtu waliyemuita kapi na oil chafu!

Hivi kama kweli Lowassa ni kapi, oil chafu na majina mengine mengi mabaya waliyompa Sisiem, hivi ilikuwaje hao hao Sisiem wamuundie timu ya watu 32 kupambana na huyomtu mmoja ambaye ni kapi hadi hivi sasa wamemuongeza mchezaji mwingine ambaye wamemvalisha jezi no. 33 ambaye ni Dr mla Mihogo?

Kwa kweli maji yamewafika shingoni magamba, kwa kuwa weshaona dalili zote za namna Umma wa watanzania ulivyojipanga kikamilifu kutumia 'vichinjio' vyao kwa maana ya vitambulisho vya kupigia kura 'kuwachinjilia' kwa mbali Sisiem kwa kupitia sanduku la kura ifikapo Oktoba 25 ya mwaka huu.

kwahiyo unadhan ndo amepanga tuwaingize wezi waje watuibie rasilimali zetu? unaweza kuwaelezea watz hiyo mihela mingi ya kampeni Lowassa anaitoa wapi na atairudisha kwa utaratibu gan km sio kutoa vitalu vya gas n.k
 
Mbona nawe hujiulizi hayo mabilioni kwa mabilioni ya shilingi yanayotumika kwenye kampeni za kumnadi Magufuli nayo yametoka wapi wakati mabango maelfu kwa maelfu aliyoyasambaza nchi nzima yeye Magufuli wakati anajinadi kuwa yeye ni mtu muadilifu sana?
 
Ukweli ni kwamba, Lowassa ameonyesha chembe chembe za ubaguzi katika msingi wa udini ambazo anataka zitumike kama kigezo cha maombi kwa Mwenyezi Mungu na katika maamuzi ya wapiga kura.

Haijalishi aina gani ya spin na nguvu gani itatumika lakini ukweli utabakia pale pale, maneno ya Lowassa ni sumu kali kama wananchi watayakubali kwa vitendo.

Sasa unajiuliza, hivi huyu Mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu ya dini?

Huyu Mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni Mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa Taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba Mungu awape Rais kutoka dhehebu lao la kilutheri wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.
 
CCM na propaganda za dini ni hatari..Magufuli kila anakopita lazima asalimiane na Masista wa Kikatoliki walioandaliwa vizuri.. Nasema hili kufuatia picha mbali mbali na nyingine zimenukuliwa na Magazeti ya kila siku..Tuache kuwasha moto tusioweza kuuzima..
 
Ni sawa na mambo yaliyomkuta Mitt Romney na ile 47%, au a bundle full of women. Hapo hata wa spin vipi, jamaa amechemsha.
 
CCM na propaganda za dini ni hatari..Magufuli kila anakopita lazima asalimiane na Masista wa Kikatoliki walioandaliwa vizuri.. Nasema hili kufuatia picha mbali mbali na nyingine zimenukuliwa na Magazeti ya kila siku..Tuache kuwasha moto tusioweza kuuzima..
It is very true.

Maccm kwa uroho wao wa kutaka kuitawala nchi hii milele, wako tayari kuanzisha propaganda yoyote chafu hata kama wakijua propaganda hizo zinaweza kuliangamiza Taifaletu.

Mbona mwaka 2005 wakati Askofu Kilaini alipowasihi watanzania wote wamchague Kikwete kwa kuwa ni chaguo la Mungu, hatukuwahi kumsikia mwanaccm yeyote akinyanyua mdomo wake kumkemea Askofu Kilaini kutokana na kauli yake hiyo potofu?
 
Back
Top Bottom