Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Lowasa hata usemeje yaani hata unifanye nini .mimi nakupenda na nitakuchagua.hata ukinikataza nisikuchagua nasema nitaenda kushtaki ili nipate haki ya kukuchagua.kwani nina mahaba na wewe lowasa

Unaweza kufikiri unamfanyia Lowasa positive campaign kwa hayo maneno, but trust me, hii ni negative campaign.
 
Hatuta chagua mtu kwa u-lutheri wake au u-katoliki wake au u-sunni wake. Kubali umeteleza. na unakotupeleka siko.

Usinisee... Anakonipeleka ndipo. Nitamchagua Lowassa kwasababu anafaa kuwa kiongozi wangu. Hata kama Lipumba angeteuliwa and UKAWA ningempa kura yangu kwani ninaamini katika mabadiliko chanya.

Poleni maccm kwa propaganda nyingine iliyofail kabla hata hamjaanza kuitumia....
 
Hata awe na dini ya mashetani na akaomba tumchague kwasababu ya ushetani wake nitampa kura yangu
 
Kwa kuwa akili yako ni fupi ndio maana hakuna unachokijua sana sana umejivalisha ujinga kichwani na ndio maana umeandika upumbavu
Haya si maneno yangu, nimeyatoa kwenye hotuba ya Nyerere Baba wa Taifa hili.
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

kaka tupe source yako
 
njiwa sisi waislamu tunaojitambua ambao ni wapumbavu na malofa bado tupo naye na tutampa kura zetu. wewe na ccm wenzako kaeni naye mbali

hujitambui bado no wonder umejipa sifa ya upumbavu!... hongera .....!!!
 
Ccm wana Bahati mbaya.Ukawa inaundwa na Watanzania wenye itikadi tofauti kidini.Kama mnaanza tena na hoja hiyo mmechelewa. Tafuteni lingine.Wote wanaolikuza hili tokea awali Ni antiukawa.Kaeni kando na kura zenu.Mm Ni mwislamu Sitakaa nikakubaliana na uzandiki.Msitufanye wtt wadogo.Tuna uwezo wa kuchambua mambo.Go Lowasa Go.Tukutane o tober.Mmeliunda Miaka 50+ muda umefika,libebeni sasa.
 
Ufafanuzi mzuri "tunamuombea kwa imani atashinda;.Hata Maandiko Matakatifu yanasisitiza kwa mkristo kuwaombea

watu wote " Basi kabla ya mambo yote nataka dua na sala, na maombezi, na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu

wote, kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka..1Timotheo 2:1-2"
 
Na walaaniwe wote ambao wanamchafua rais wa amwamu ya tano wa j.m.t. Ndugu e.n.lowasa,
kila aupendaye ukawa aseme.amen.amen.amen.
Na wabarikiwe na mwenyezi mungu wote waupendao ukawa.
Kila mwenye pumzi aseme.amen.amen.amen.
 
Huo utetezi amekupa wewe mwenyewe au amejitetea wapi. Acheni uchochezi
 
Upo sahihi rais wetu lowasa achana na hawa ccm wanachonga sana Wewe mbele kwa mbele ukawa tupo imara hutuyumbishwi
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

Too late. Embe likishadondoka halirudishiki mtini. Mungu ni Mkubwa kuliko akili ya Lowasa. Malipo ni hapa hapa duniani. Natumia hayo maneno kumaanisha kuwaLowasa hakuongea kwa bahati mbaya kwa sababu aliongea akiwa eneo takatifu ambalo shetani hakai. Unless atuambie kuwa alikuwa hajaachana na shetani wakati akiingia kanisani.
 
HAMY-D umekuwa siku hizi mkuu,hongera!!

Kama hayo ndio aliyonena basi maCCM yanapandikiza na kukuza Maneno ya kinafiki tu!!

Nani asiyejua kuwa maCCM ndio yaliyopanda mbegu ya udini Tanzania na wakaupalilia na kuuwekea mbolea awamu hii ya Kikwete??!! Safari hii sijui watawalagai na nini waislamu maana wagombea wote wakristo!!!

Ni kweli nami nimpongeze Hammy D kwa kuueleza huu ukweli kama ulivyotolewa. Huo ndio u-great thinker tunaotaka kuuona kwenye majukwaa.Lowassa kama mgombea na muumini wa dhehebu hilo anayo haki ya kuwaomba waumini wenzie wamuombee na pia kumpa kura aweze kushinda. Wala sio kosa kusema wakati huu nao walutheri na waumini wa madhehebu mengine watoe raisi. Hapo hajaongelea udini wowote kwani ni kweli inapoangukia zamu ya nafasi ya wakristo mara zote amekuwa akitokea dhehebu moja tu. Yapo madhehebu mengi ya kikristo kwa idadi tofauti ya waumini ikiongozwa na kanisa katoliki kwa wingi wa waumini. Walutheri wanaweza kuwa wa pili na pengine wakifuatwa na Waangilikani.Uchaguzi wa mwaka 2010 Prof. Lipumba alikuwa akimnadi raisi Kikwete kwenye misikiti ya Dsm na hatimae kakiri mwenyewe msikiti wa Idrissa. Waumin wa misikiti ile ni waislamu. Lakini hilo wananchi wakaona ni sahihi kwani Kikwete kama muislam nae alitakiwa aombewe kura toka kwa waumin wenzie ingawa hata kwenye makanisa nako alikuwa akiombewa kura. Hivyo wote wanaomwandika na kumzungumza vibaya Lowassa kwenye majukwaa kuwa anaeneza udini wanatakiwa wapuuzwe kwani wananchi wa sasa hawadanganyiki tena. WAO WAJIHOJI JEE TEJIPANGA VIPI?
 
Last edited by a moderator:
pamoja na propaganda zote ccm dhidi ya ukawa inaonyesha wazi kuwa kitengo chao cha propaganda kimeshindwa kazi na ningewashauri waombe msaada USSR kama bado ipo kwa maana USSR ndio walikuwa mabingwa wa propaganda
 
Sasa wale wahenuaji wa CCM walitaka aseme Tanzania ilishawahi kuwa na Rais Mlutherani ?
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

Bado nasubiri ajenda ya Pili na ya Tatu. Tutajua tu na mtayasema wenyewe.
 
kuna Jehova na Allah nk....Ukweli waislamu na wakristo wanaabudu Mungu tofauti ila siasa za dunia zinapofusha na kudai Mungu ni mmoja. ..alichosema Lowassa ni sawa kwani toka uhuru nchi hii imekuwa na maraisi wakatoliki na waislamu na hii zamu ya waprotenstant kama chungu tema
 
Back
Top Bottom