Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

lowassa umeeleweka! mleta mara unalitakia taifa mema. heko
 
haa haa nasikia safar hii utamchagua dovutwa teh teh...ubaguzi mbaya sana.

Muhimu simchagui KKKT anaewaambia waumini wake kuwa Tanzania kuna ubaguzi wa dini na wamchaguwe yeye eti kwa sababu tu ni KKKT.

Lakini nikitazama listi iliyomfukuza Slaa na Lipumba wala sishangai, Mbowe, Mbatia, Lowassa. Hao wote ni wale wale tu.
 
tumesikia kuwa kuna video ya lowasa akiwa kanisani akiomba walutheli wampigie kura ili tanzania itawaliwe na yeye ambaye ni mlutheli na kutaka sasa zamu yao.
tuelezwe na wahusika kama ni kweli au imepangwa ili watanzania tujue ukweli.
tusipende kufichaficha haya mambo ni hatari.

tunaomba uhakika wa hili jambo
 
Ukweli ni kwamba, Lowassa ameonyesha chembe chembe za ubaguzi katika msingi wa udini ambazo anataka zitumike kama kigezo cha maombi kwa Mwenyezi Mungu na katika maamuzi ya wapiga kura.

Haijalishi aina gani ya spin na nguvu gani itatumika lakini ukweli utabakia pale pale, maneno ya Lowassa ni sumu kali kama wananchi watayakubali kwa vitendo.

Sasa unajiuliza, hivi huyu Mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu ya dini?

Huyu Mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni Mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa Taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba Mungu awape Rais kutoka dhehebu lao la kilutheri wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.

Nashindwa kuwaeleweni. Kwani ni uongo urais Tanzania tunapeana kwa zamu za udini kwa maana ya waisilamu na wakristu na japo halijawekwa rasmi kimaandishi lakini lipo tu vizuri kiutamaduni na wala halitupi shida? Sasa kuna ubaya gani walutheri nao wakapata nafasi hiyo sasa jambo ambalo hata wakatoliki hawatalinungunikia kabisa. Hata awamu ingine ya waisilamu nao wataangalia nani achukue. Kama mshia msuni nk mradi ana sifa za kuongoza. Kwa hali hiyo tusiipe tafsiri potofu ya udini kauli ya lowasa.
 
ni kawaida sana ya ccm kuwabagua watanzania wakati wa uchaguzi ili ccm ishinde. mzee makamba wamelikuza jambo hili dogo ili kuwatenganisha wakristo kwa malengo yao ya kisiasa.lowasa muda wote amekuwa rafiki wa wote. ushahidi wa matendo yake upo.chondechonde ccm taifa hili ni letu sote. mmekaa madarakani kwa muda wa kutosha....

nyie mnaona dogo .. hilo swala hivi kama angekuwa ni muislam amefanya hivyo maaskofu si wange andamana mwezi , na hii jamii forum si ingejaa nyie manyumbu kila kona au ndio mahaba kipenda roho
 
ni kweli alisema hvyo ni video ipo ni ushahidi tosha...wati wanaosema lowassa ni chaguo la Mungu wasije rudia tena ni dhambi kumsingizia Mungu sababu ya kumpigia mtu kampeni..ni vbaya kulitaja nina la Mungu ukishuhudia uongo fanyeni njia nyingne za kampeni ila sio kumsingizia Mungu
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

Ulimi hauna mfupa
 
tumesikia kuwa kuna video ya lowasa akiwa kanisani akiomba walutheli wampigie kura ili tanzania itawaliwe na yeye ambaye ni mlutheli na kutaka sasa zamu yao.
Tuelezwe na wahusika kama ni kweli au imepangwa ili watanzania tujue ukweli.
Tusipende kufichaficha haya mambo ni hatari.

Tunaomba uhakika wa hili jambo

ni kweli kabisa na ushaidi wa video upo...udini sio kitu kizuri hivi dini nyingine zitamfikiriaje...ni dhambi kubwa kwa mheshimiwa lowassa aungame kwa mungu
 
Nashindwa kuwaeleweni. Kwani ni uongo urais Tanzania tunapeana kwa zamu za udini kwa maana ya waisilamu na wakristu na japo halijawekwa rasmi kimaandishi lakini lipo tu vizuri kiutamaduni na wala halitupi shida? Sasa kuna ubaya gani walutheri nao wakapata nafasi hiyo sasa jambo ambalo hata wakatoliki hawatalinungunikia kabisa. Hata awamu ingine ya waisilamu nao wataangalia nani achukue. Kama mshia msuni nk mradi ana sifa za kuongoza. Kwa hali hiyo tusiipe tafsiri potofu ya udini kauli ya lowasa.

kwani walutheran sio wakristu , kwa hiyo na wasabato , waanglicana wapentecoste , wasunn , washiya nao walalamike ili nao watoe raisi
 
tumesikia kuwa kuna video ya lowasa akiwa kanisani akiomba walutheli wampigie kura ili tanzania itawaliwe na yeye ambaye ni mlutheli na kutaka sasa zamu yao.
tuelezwe na wahusika kama ni kweli au imepangwa ili watanzania tujue ukweli.
tusipende kufichaficha haya mambo ni hatari.

tunaomba uhakika wa hili jambo

Video ipo lkn ameomba msamaha kama kuna watu aliwakwaza
 
Amesema na hilo tuliliona siku nyingi, watu humu wakawa wanabisha lakini Mwenyeezi Mungu hamfichi mnafik, leo liko bayana.
 
Ni kweli kabisa video hiyo ipo nimeiona na kuisikiliza. Haya sasa yanadhihirisha malalamiko kuwa huenda baadhi ya viongozi wa dini wamehongwa ili kuwapa KKKT nguvu ha urais.
 
Angesema tu wamuombee basi......hii ya kusema ulutherani wangine watakuja na hoja ya kutaka Rais Msabato

Mbona nyie maccm mnapandikiza ukabila hawajawalalamikia? Hii SMS inayozunguka Usukumani ni ya nini kama siyo ukabila huo? SMS yenyewe inasema hivi nanukuu "Wasukuma oyeeeeeee!! Pigia kura yako ngosha. Hii ni zamu yetu WASUKUMA kuongoza Taifa, uwezo wa kushinda tunao na nia tunayo. Chagua MAGUFULI ili awe MSUKUMA wa kwanza kuwa RAIS wa TANZANIA. CCM OYEEEEEEEEEE!!! Tuma SMS hii kwa WASUKUMA wote waliomo kwenye cm yako!" Mwisho wa kunukuu. JE, huu siyo ukabila? hii ndo gia waliyoingia nayo ccm baada ya mbinu ovu kushindwa na Wasukuma wenzangu wamehadaika sijapata kuona! Basi kama ni habari ya zamu nasema hii ni zamu ya Walutheri, zamu ya Wamaasai, zamu ya kanda ya kaskazini!
 
tumesikia kuwa kuna video ya lowasa akiwa kanisani akiomba walutheli wampigie kura ili tanzania itawaliwe na yeye ambaye ni mlutheli na kutaka sasa zamu yao.
tuelezwe na wahusika kama ni kweli au imepangwa ili watanzania tujue ukweli.
tusipende kufichaficha haya mambo ni hatari.

tunaomba uhakika wa hili jambo
Hii hapa,
 
Last edited by a moderator:
nyie mnaona dogo .. hilo swala hivi kama angekuwa ni muislam amefanya hivyo maaskofu si wange andamana mwezi , na hii jamii forum si ingejaa nyie manyumbu kila kona au ndio mahaba kipenda roho
Ndiyo ni dogo na halina mantiki. Lowasa mmemuita kwa mambo mengi ya kusaidia bila kujali dini, dhehebu n.k na wala haitaji kura za KKKT kushinda, watu wote wapenda mabadilko alipo tupo
 
Muhimu simchagui KKKT anewaambia waumini wake kuwa Tanzania kuna ubaguzi wa dini na wanmchaguwe yeye eti kwa sababu tu ni KKKT.

Lakini nikitazama listi iliyomfukuza Slaa na Lipumba wala sishangai, Mbowe, Mbatia, Lowassa. Hao wote ni wale wale tu.

haa haa ila utamchagua dovutwa teh teh ubaguzi mbaya sana...
 
Nashindwa kuwaeleweni. Kwani ni uongo urais Tanzania tunapeana kwa zamu za udini kwa maana ya waisilamu na wakristu na japo halijawekwa rasmi kimaandishi lakini lipo tu vizuri kiutamaduni na wala halitupi shida? Sasa kuna ubaya gani walutheri nao wakapata nafasi hiyo sasa jambo ambalo hata wakatoliki hawatalinungunikia kabisa. Hata awamu ingine ya waisilamu nao wataangalia nani achukue. Kama mshia msuni nk mradi ana sifa za kuongoza. Kwa hali hiyo tusiipe tafsiri potofu ya udini kauli ya lowasa.[/kwani walutheran sio wakristu , kwa hiyo na wasabato , waanglicana wapentecoste , wasunn , washiya nao walalamike ili nao watoe raisi
 
Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.

hayo maelezo yako tuwekee clip hapa tujue
 
Back
Top Bottom