Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ni sawa na mambo yaliyomkuta Mitt Romney na ile 47%, au a bundle full of women. Hapo hata wa spin vipi, jamaa amechemsha.
Ukiusoma kwa makini hata utetezi wake eti ameanza kuwalaumu wanaomwambia amepotoka.

Hivi anadhani kama asingeyasema haya maneno yenye mlengo wa kuligawa taifa katika mlengo wa imani za dini, hizi hoja za kumweleza kama amepotoka zingetoka wapi?

Hii ni sawa na kukuta mlango wa nyumba uko wazi, halafu unaingia na kuiba, lakini baada ya kukamatwa unaanza kuwalaumu wenye nyumba kwa kuacha mlango wazi!

Kazi kweli kweli.
 
Hatuta chagua mtu kwa u-lutheri wake au u-katoliki wake au u-sunni wake. Kubali umeteleza. na unakotupeleka siko.

Wewe na wenzio msiojitambua ndio mnaoleta uchochezi wa kidini, na hamtafanikiwa..!!
 
CCM kweli wameishiwa. Jana wakati ninaangalia taarifa ya habari ya SAA 2:00 ucku nilimuona Mzee Makamba mishipa ya shingo imemtoka,sauti imekauka kwa kujikamua. Ooooh! Udini Udini" Udini uko wapi hapo?! Mbona kila kitu kipo waazi tu.
Walikuja na santuri ya Richmond. Imebuma
Wakaja na Mwakyembe. Amebuma
Wakaja na Dk Slaa. Amebuma
Sasa wanamalizia na Udini. Pia Umebuma.
Watanzania wanachohitaji ni maji,Elimu bora,Ajira kwa vijana,Umeme wa uhakika,Barbara za uhakika sio zinazojengwa Leo kesho zinanza kubonyea halafu inasingiziwa mipira pamoja na mambo meengi ya kimaendeleo. Wao wanachotaka ni kiongozi ambaye atasimamia maendeleo kwa spidi ya ajabu. Baaasi.
Hayo mambo ya dini wanawaachia wazeee kama Makamba ambao yao yanawaendea. Lakini wale choka mbaya wao wanataka mipango mkakati ya kuwanasua na umasikini tuu!!

haa haa mzee makamba yupo kwenye mradi wake wa kuhakikisha mwanao january ana ukwaa uwaziri na si kingine. hoja feki ya udini hutumiwa na ccm kila wakati wa uchaguzi kwa lengo la kujipatia kura.
 
Ameteleza wapi?! Au kuwaomba waumini wenzake wamuombee ndio ishakuwa kosa?

mkuu kwa ccm wakiomba waombewe sio dhambi. dhambi wakisema wapinzani. nikikumbuka ya lukuvi na waislamu sina hamu na ccm. lowasa juuu..
 
Hebu ngoja tuwaulize hao maccm kati ya kauli hizi ni kauli zipi ambazo hakika zinaweza kulibomoa Taifa letu.

Kauli no. 1 ni kauli iliyowahi kutolewa na uvccm ya mkoa wa Pwani ikitolewa na spokesperson wao Riz-One kuwa kamwe Rais hatokuja kutoka mikoa ya kaskazini.

Kauli no. 2 ni iliyotolewa na Nape kuwa CCM ni lazima ishinde hata kama italazimika kushinda kwa goli la mkono.

Linganisha kauli hizo 2 za wanaccm 'wazito' na kauli ya EL kuwa nawaomba kura zenu wakristo wenzangu endapo tu mtaona ninafaa kuliongoza Taifa hili, tena kauli hiyo akiitoa kanisani kwenye ibada ya Jumapili alipokwenda kuabudu.

mkuu umesahau ile ya lukuvi? tukiruhusu muungano wa serikali tatu zanzibar itakuwa nchi ya kiislamu. sina hamu na ccm kamwe...
 
kwahiyo unadhan ndo amepanga tuwaingize wezi waje watuibie rasilimali zetu? unaweza kuwaelezea watz hiyo mihela mingi ya kampeni Lowassa anaitoa wapi na atairudisha kwa utaratibu gan km sio kutoa vitalu vya gas n.k

haa haa je ccm hiyo mihela ya kampeni nao wanaitoa wapi?
 
Ukweli ni kwamba, Lowassa ameonyesha chembe chembe za ubaguzi katika msingi wa udini ambazo anataka zitumike kama kigezo cha maombi kwa Mwenyezi Mungu na katika maamuzi ya wapiga kura.

Haijalishi aina gani ya spin na nguvu gani itatumika lakini ukweli utabakia pale pale, maneno ya Lowassa ni sumu kali kama wananchi watayakubali kwa vitendo.

Sasa unajiuliza, hivi huyu Mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu ya dini?

Huyu Mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni Mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa Taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba Mungu awape Rais kutoka dhehebu lao la kilutheri wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.

haa haa yale yaliyotamkwa na lukuvi ni sawa? haa haa eti lowasa alipokuwa ccm si mdini. baada ya kwenda upinzani ni mdini. nimeamini ccm wameishiwa sera.
 
ni kawaida sana ya ccm kuwabagua watanzania wakati wa uchaguzi ili ccm ishinde. mzee makamba wamelikuza jambo hili dogo ili kuwatenganisha wakristo kwa malengo yao ya kisiasa.lowasa muda wote amekuwa rafiki wa wote. ushahidi wa matendo yake upo.chondechonde ccm taifa hili ni letu sote. mmekaa madarakani kwa muda wa kutosha....
 
Hakika Lowassa ni chaguo la Mungu vikwazo anavyopitia ni vingi sana,Baba tupo pamoja sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!
 
haa haa yale yaliyotamkwa na lukuvi ni sawa? haa haa eti lowasa alipokuwa ccm si mdini. baada ya kwenda upinzani ni mdini. nimeamini ccm wameishiwa sera.
Hayo ya Lukuvi kayajengee hoja kwenye jimbo lake ambalo ni mgombea Ubunge.

Sisi hapa tunajadili mtu ambaye anatembea barabarani akiwaomba watanzania wote wamchague awe Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama wakati ana chembechembe za ubaguzi wa kidini.

Kwa fikra zako unataka kulinganisha madhara ya kumchagua Rais ambaye ni mbaguzi kwa msingi wa dini na kumchagua mbunge.

Kazi kweli kweli!
 
haa haa nasikia safar hii utamchagua dovutwa teh teh...ubaguzi mbaya sana.
Tatizo ni kwamba, ametamka hayo maneno katika sehemu mahsusi, kwa watu wa dhehebu maalumu. Tofauti na Mkapa aliyetamka malofa mbele ya kadamnasi ya watu wa madhehebu yote pale Jangwani. Nina uhakika anajutia yale aliyotamka, kwanza hakuwa na sababu ya kuyasema hayo.
 
Anajaribu kupingana na ushahidi wa video??
 
CCM na propaganda za dini ni hatari..Magufuli kila anakopita lazima asalimiane na Masista wa Kikatoliki walioandaliwa vizuri.. Nasema hili kufuatia picha mbali mbali na nyingine zimenukuliwa na Magazeti ya kila siku..Tuache kuwasha moto tusioweza kuuzima..

ni kweli mkuu hata swala la Dr Slaa kuna minong'ono!!!!
 
Back
Top Bottom