Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Acheni kukuza ishu ndogo kuwa kubwa ...ktk kmapeni zake za hadhara mikutanoni hajaonyesha UDINI wowote...alipoenda kanisani kwake ndo kazungumzia kwamba yeye kwakulwa ni Mlutheri na yuko na walutheri wenzie basi kama wataona anafaa wampigie kura.....mimi sidhani kama hiyo kauli inaonyesha moja kwa moja kuwa ana Udini...ila angezungumza katika mikutano ambako kuna watu wa dini zote hapo isingependeza!!! unafikiri hata angekuwa Muisalamu kaingia msikitini asingeomba waumini wenzake wamwombee Dua?
 
Hakuna shida mzee....wanafiki watayakuza ila hayamuingii mtu maskioni.... Mbona JK ametoa nafas nyeti kwa waislam kuliko rais yoyote yule....unajua kama kuna movement ya Islamization of TZ...wachen uzuzu na unachoskia ......
 
Tutamchagua hivyo hivyo, hata akienda Milembe akasema mimi ni kichaa mwenzenu bado tutamchagua tu. CCM hamna jipya mwende mkakojoe mlale
 
Waharishe wajikojolee tuu.Mimi nimeamua kura yangu ni Lowasa tuu.Nyie ccm mtuambie ujinsia sio ubaguzi?chagua LOWASA chagua UKAWA.SAA ya mabadiliko ni sasa.
 
Lowasa hata usemeje yaani hata unifanye nini .mimi nakupenda na nitakuchagua.hata ukinikataza nisikuchagua nasema nitaenda kushtaki ili nipate haki ya kukuchagua.kwani nina mahaba na wewe lowasa
 
Tutamchagua hivyo hivyo, hata akienda Milembe akasema mimi ni kichaa mwenzenu bado tutamchagua tu. CCM hamna jipya mwende mkakojoe mlale

Hivi mnasikia mnachokiongea? Mnajiona mna akili timamu nyie? Mnaelewa kuwa tunamchagua rais wa Tanzania?
Hebu acheni kufanya hili suala la uchaguzi kama ushabiki wa Bobgo Star Search
Ukiweka rais kichaa tutaumia wote lakini utaumia we binafsi na marafiki zako. Maisha yenu hayataboreka sasa mtakuwa mmepata mabadiliko gani?
 
Waharishe wajikojolee tuu.Mimi nimeamua kura yangu ni Lowasa tuu.Nyie ccm mtuambie ujinsia sio ubaguzi?chagua LOWASA chagua UKAWA.SAA ya mabadiliko ni sasa.

Mabadiliko gani kama umesema mtu hata akijikojolea na kujiharishia. Hebu shirikisha ubongo wako. Huyo mtu atakusaidiaje kama rais?
Msifanye mzaha hapa si ushabiki wa Manchester United na Arsenal
 
ccm wameshikwa pabaya mwaka huu kila mbinu wanayojqribu inabuma , huyu jamaa anamvuto sana. mimi binafsi sijaona kibaya kwa sababu hajaomba kura ila ameomba wamwombee
 
Hata waseme nini, kura yangu ni kwa Lowasa. Hutaki unaacha.
 
video inajieleza , kasema waliopita walikuwa wakatoliki tena kawataja kwa majina na kusema sasa hivi walutheri wamchague yy, huyo ni mdini na huo ni mwendelezo wa usanii wake, hatufai hata kuongoza mtaa
 
CCM wana mengi ya kujivunia ya sasa na kihistoria. Wayatumie hayo kumnadi Magufuli kama Makongoro alivoahidi.
Lakini Ukanda, Ufisadi, Ugonjwa, Kununua CHADEMA na Sasa udini havisaidii kumstop lowassa
 
tuweni makini na staili ya kuomba kura kwa kutaka kuwafurahisha walioko mbele yako kwa wakati huo maana kufurahi kwa wachache walioko mbele yako kunaweza kuwaudhi wengi watakuja kusikia baadae.

na katika utendaji ndio tuwe makini zaidi

Huu ndio utetezi wa mgombea urais kupitia tiketi ya UKAWA kuhusu kauli yake aliyoitoa alipokuwa katika kanisa la Kilutheri huko Tabora. Nanukuu...

"Kwanza, niombe radhi kwa wale ambao kwa njia moja au nyingine wamekwazika kwa maneno ambayo yametafsiriwa na baadhi ya watu kuwa ni 'udini' wakati naongea na waumini mjini Tabora siku ya jumapili na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Pili, niseme kwa uwazi kabisa kuwa mimi sio mdini hata kidogo. Mimi ni mcha Mungu na mojawapo ya mambo ambayo imani yangu imenifundisha ni upendo kwa kila mtu bila kujali dini yake.

Tatu, mimi kama mgombea ni jukumu langu kuomba kura kwa kila Mtanzania bila kujali dini yake. Hili ni jambo ambalo mimi binafsi naliamini kwa dhati kabisa pamoja na chama changu.

Nne, naomba nifafanue nilichokisema na kumaanisha wakati wa Ibada. Lengo langu kuu lilikuwa ni kuomba waumini wenzangu waniombee kwa sala zao katika safari yetu ya kuikomboa Tanzania. Sikuwaambia wanichague au wanipigie kura kwa sababu mimi ni Mlutheri. Hapana. Nilichowaomba na wote mmesikia ni sala zao. Sijawaambia wamchague Mlutheri mwenzao. Ni kweli kwamba hakuna Mlutheri ambae amewahi kuwa rais. Sidhani kama nimesema uongo. Lakini nisisitize kwamba Ulutheri sio kigezo cha kuwa rais. Dini sio kigezo. Maombi yangu kwao waumini ni sala zao na hili jambo mtu yeyote mwenye imani anaruhusiwa kulifanya.

Nimalizie kwa kuwaomba radhi tena wale ambao wamekwazika kwa kauli yangu. Najua baadhi ya watu ambao wanapinga harakati zetu watajitahidi sana kuchochea na kulikuza jambo hili. Sababu zao tunazijua. Naomba muwapuuze tusonge mbele. Watanzania watachagua sio kwa sababu ya dini, ukanda, ukabila au jinsia. Watachagua kwa kuangalia uwezo wa mtu na utekelezaji wa ahadi kutokana na mipango ambayo tumeiweka." Mwisho wa kunukuu.
 
tahadhari kuna video inasambaa kwa kasi mitandaoni kuhusu udini wameedit lowasa akisema naomba kura za waluteri isikilizeni vizuri inasauti mbili zinatoka kwa pamoja aliyefanya kazi hiyo ni kijana mmoja anaitwa hamphrey mpole pole chama kitachukua hatua stahiki kukomesha uchochezi.sambaza ujumbe huu kwenye magroup mengine
 
Wao sasa hivi wanatafuta jinsi ya kujinasua na taarifa lowassa anafatiliwa kampeni xake xaid ya magufuli kwa karibu zaid.
 
Unajua Hawa Maccm ni kama hawajitambui; kwasababu wanaongea vi2 ambavyo wao wenyew hawana uhakika navyo.

hiyo inatokea kwasababu wao wanajing'atang'ata tu kutokana na kutokuwepo kwa E.L CCM, na washaona kuwa chaguo la watanzania ni E.L hivyo wanafanya kila njia ili wao wamchafue 2.

kwa kauli ya lowassa ilikuwa haimanish kama anachochea udini lakin alitaka wamwombee 2 kwa mungu maana yeye ashaona bila mungu kumsimamisha kipenzi cha watz taifa litakuwa pabaya.
 
Back
Top Bottom