Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

CCM kama wabunge wao hawana cha kusema bali wanangojea mpinzani anene wapate hoja
 
Hata kama anaonekana kuteleza, huo ndo ukweli nchi sıo ya Waroma na Waislam peke yao na Anglikan.
 
kwahiyo unadhan ndo amepanga tuwaingize wezi waje watuibie rasilimali zetu? unaweza kuwaelezea watz hiyo mihela mingi ya kampeni Lowassa anaitoa wapi na atairudisha kwa utaratibu gan km sio kutoa vitalu vya gas n.k
Kwa hiyi na ninyi hizo fedha za kutusomba kutoka vijijini na posho mnayotupa kwenda kuhudhuria mikutano yenu na tishet na kofia mtazirudishaje ?!!
 
Mwanzo walianza kwamba ni Rais wa Kaskazini walipoona hoja hii hainunuliki na mafuriko yapo kila kona sasa wamedandia Ulutheri. Sasa hoja ni ulutheri what is next?
 
Hebu ngoja tuwaulize hao maccm kati ya kauli hizi ni kauli zipi ambazo hakika zinaweza kulibomoa Taifa letu.

Kauli no. 1 ni kauli iliyowahi kutolewa na uvccm ya mkoa wa Pwani ikitolewa na spokesperson wao Riz-One kuwa kamwe Rais hatokuja kutoka mikoa ya kaskazini.

Kauli no. 2 ni iliyotolewa na Nape kuwa CCM ni lazima ishinde hata kama italazimika kushinda kwa goli la mkono.

Linganisha kauli hizo 2 za wanaccm 'wazito' na kauli ya EL kuwa nawaomba kura zenu wakristo wenzangu endapo tu mtaona ninafaa kuliongoza Taifa hili, tena kauli hiyo akiitoa kanisani kwenye ibada ya Jumapili alipokwenda kuabudu.

Kauli tata zenye mwelekeo wa UDINI, UKANDA na UKABILA ambazo zimewahi kutolewa na Wasemaji wa Chama Tawala ni pamoja na kwamba CUF ni Chama cha Waislam (2005), CHADEMA Chama cha Wachaga (2010) na majuzi kwamba "Urais" hautatoka Kanda ya Kaskazini- Nashangaa jana wamekazania "Udini" wa Lowassa.
 
HAMY-D umekuwa siku hizi mkuu,hongera!!

Kama hayo ndio aliyonena basi maCCM yanapandikiza na kukuza Maneno ya kinafiki tu!!

Nani asiyejua kuwa maCCM ndio yaliyopanda mbegu ya udini Tanzania na wakaupalilia na kuuwekea mbolea awamu hii ya Kikwete??!! Safari hii sijui watawalagai na nini waislamu maana wagombea wote wakristo!!!

Sasa wewe ndo unachochea UDINI. TUMIA AKILI KUFIKILIA NA SIO MATAKO
 
Last edited by a moderator:
Hayo ya Lukuvi kayajengee hoja kwenye jimbo lake ambalo ni mgombea Ubunge.

Sisi hapa tunajadili mtu ambaye anatembea barabarani akiwaomba watanzania wote wamchague awe Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na Usalama wakati ana chembechembe za ubaguzi wa kidini.

Kwa fikra zako unataka kulinganisha madhara ya kumchagua Rais ambaye ni mbaguzi kwa msingi wa dini na kumchagua mbunge.

Kazi kweli kweli!

kuna watu hawakuwahi kutoa matamshi yoyote yanayoashiria udini lakini wameacha maafa makubwa ya upendeleo wa kidini nchi hii pekua historia vizuri
 
Hebu ngoja tuwaulize hao maccm kati ya kauli hizi ni kauli zipi ambazo hakika zinaweza kulibomoa Taifa letu.

Kauli no. 1 ni kauli iliyowahi kutolewa na uvccm ya mkoa wa Pwani ikitolewa na spokesperson wao Riz-One kuwa kamwe Rais hatokuja kutoka mikoa ya kaskazini.

Kauli no. 2 ni iliyotolewa na Nape kuwa CCM ni lazima ishinde hata kama italazimika kushinda kwa goli la mkono.

Linganisha kauli hizo 2 za wanaccm 'wazito' na kauli ya EL kuwa nawaomba kura zenu wakristo wenzangu endapo tu mtaona ninafaa kuliongoza Taifa hili, tena kauli hiyo akiitoa kanisani kwenye ibada ya Jumapili alipokwenda kuabudu.

Huna hoja wewe.
 
CCM na propaganda za dini ni hatari..Magufuli kila anakopita lazima asalimiane na Masista wa Kikatoliki walioandaliwa vizuri.. Nasema hili kufuatia picha mbali mbali na nyingine zimenukuliwa na Magazeti ya kila siku..Tuache kuwasha moto tusioweza kuuzima..

CCM ndio waliozungmza kanisani Tabora?
 
ukweli ni kwamba, lowassa ameonyesha chembe chembe za ubaguzi katika msingi wa udini ambazo anataka zitumike kama kigezo cha maombi kwa mwenyezi mungu na katika maamuzi ya wapiga kura.

Haijalishi aina gani ya spin na nguvu gani itatumika lakini ukweli utabakia pale pale, maneno ya lowassa ni sumu kali kama wananchi watayakubali kwa vitendo.

Sasa unajiuliza, hivi huyu mungu anawaumba binadamu kwa kuangalia madhehebu ya dini?

Huyu mungu anaweza kuruhusu na kukubaliana na fikra za kibaguzi kwa watoto wake wote.

Ni mungu gani huyu anayetoa baraka katika misingi ya kuligawa taifa lake.

Kwani hao ambao wanaomba mungu awape rais kutoka dhehebu lao la kilutheri wamebaguliwa au watapata nini zaidi ya madhehebu mengine.
c.c. Zitto zuberi kabwe
 
Angekuwa mdini ngelimuunga mkono muislamu jk kwa nguvu zote kumuingiza ikulu?
 
Mwanzo walianza kwamba ni Rais wa Kaskazini walipoona hoja hii hainunuliki na mafuriko yapo kila kona sasa wamedandia Ulutheri. Sasa hoja ni ulutheri what is next?
Kuhoji uraia.
 
Safii aseme asemavyo lakini akae akijua yeye ndio RAIS wa Tanzania.

Rais wa Tanzania kwa kura yako pekee yako? wewe umekuwa mtabiri au unavyoona watu wanavyosema midomoni basi unajua ndivyo wanavyowaza mioyoni mwao.usijekupata mshituko siku ya matokeo.
 
Back
Top Bottom