Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

Ufafanuzi kuhusu Ulutheri na Urais - Lowassa

tahadhari kuna video inasambaa kwa kasi mitandaoni kuhusu udini wameedit lowasa akisema naomba kura za waluteri isikilizeni vizuri inasauti mbili zinatoka kwa pamoja aliyefanya kazi hiyo ni kijana mmoja anaitwa hamphrey mpole pole chama kitachukua hatua stahiki kukomesha uchochezi.sambaza ujumbe huu kwenye magroup mengine

Huwezi kuwapotosha hata waliokuwepo kanisani.
Kosa lililofanyika ni kudhani kanisa zima wanamsapoti Lowassa.
Jambo la msingi na lankiungwana ni kukiri ulimi uliteleza na maombo iende mbele.
Mbona Mwapachu (shabiki wake mkubwa) keshakiri na kumwombea msamaha?
 
Hatari sana, watanzania uzuri wetu ni warahisi sana kulainika na maneno matamu ya wagombea.
 
Source ya haya majibu sio credible, yawezekana ni ya kutunga pia kama ilivyotengenezwa video clip ya uongo.
 
Hakuna shida mzee....wanafiki watayakuza ila hayamuingii mtu maskioni.... Mbona JK ametoa nafas nyeti kwa waislam kuliko rais yoyote yule....unajua kama kuna movement ya Islamization of TZ...wachen uzuzu na unachoskia ......

Wewe ndo mnafiki na mdini.
 
Mulianza na uislamu na ukiristo. Na sasa munataka kuwagawa watu kwa madhehebu? Watu hawawaelewi.

Dhambi ya ubaguzi hiyooo.....na nilishatabiri siku nyingi kuwa tunakoelekea itakuwa mchague huyu mweusi usimchague yule mweupe, itakuja hadi mrefu na mfupi....Mungu hawaachi wadhalimu hivi hivi....Tanzania oyeeeee...

Nangoja waraka
 
Hatuta chagua mtu kwa u-lutheri wake au u-katoliki wake au u-sunni wake. Kubali umeteleza. na unakotupeleka siko.

Kwa kuwa akili yako ni fupi ndio maana hakuna unachokijua sana sana umejivalisha ujinga kichwani na ndio maana umeandika upumbavu
 
Kila mbinu ya maji taka inayotumiwa mwaka huu inabuma, Mungu anasikia kilio cha wengi
 
Chadema ni chama kinachotaka kuanzisha vita vya udini serikali ilitahadharisha pasitokee aina yoyote ya siasa katika kanisa na misikiti pia mbona hili hukulisema?
 
CCM kweli wameishiwa. Jana wakati ninaangalia taarifa ya habari ya SAA 2:00 ucku nilimuona Mzee Makamba mishipa ya shingo imemtoka,sauti imekauka kwa kujikamua. Ooooh! Udini Udini" Udini uko wapi hapo?! Mbona kila kitu kipo waazi tu.
Walikuja na santuri ya Richmond. Imebuma
Wakaja na Mwakyembe. Amebuma
Wakaja na Dk Slaa. Amebuma
Sasa wanamalizia na Udini. Pia Umebuma.
Watanzania wanachohitaji ni maji,Elimu bora,Ajira kwa vijana,Umeme wa uhakika,Barbara za uhakika sio zinazojengwa Leo kesho zinanza kubonyea halafu inasingiziwa mipira pamoja na mambo meengi ya kimaendeleo. Wao wanachotaka ni kiongozi ambaye atasimamia maendeleo kwa spidi ya ajabu. Baaasi.
Hayo mambo ya dini wanawaachia wazeee kama Makamba ambao yao yanawaendea. Lakini wale choka mbaya wao wanataka mipango mkakati ya kuwanasua na umasikini tuu!!

Ukitanguliza mapenzi huwezi kuona kwa sababu mapenzi ni upofu.hata hivo ukweli siku zote hubaki ukweli
 
Hivi mnasikia mnachokiongea? Mnajiona mna akili timamu nyie? Mnaelewa kuwa tunamchagua rais wa Tanzania?
Hebu acheni kufanya hili suala la uchaguzi kama ushabiki wa Bobgo Star Search
Ukiweka rais kichaa tutaumia wote lakini utaumia we binafsi na marafiki zako. Maisha yenu hayataboreka sasa mtakuwa mmepata mabadiliko gani?

Tukiweka raisi asiyesikiliza ushauri mfano yule waziri wa bomoabomoa,masamaki ya kichina,kivuko used bila kusahau majumba ya wananchi hatuwezi kuja kupata hasara zaidi ya zile?Na deni la taifa haliwezi kuongezeka kweli?Na haya mambo ya kutokusikiliza ushauri na kukurupuka hayawezi kutugombanisha na majirani zetu?Nahitaji kujua.
 
Lowasa ni rais hata ingekuwaje
 
dhambi ya udini inakutafuna wee mzee, na mungu atakulani kwa nia mbaya uliyokua nayo katika nchi hii
 
Angesema tu wamuombee basi......hii ya kusema ulutherani wangine watakuja na hoja ya kutaka Rais Msabato

Tatizo hapa ni ccm kutafuta kila aina ya mbinu ili kufanikisha malengo yao! Nina uhakika jk alipoingia msikitini aliwaomba waislam wenzake wampigie kura..its nomal..ni muda wa wagombea kujipendekeza kuomba kura!..kuna wengine wanaongea hadi kilugha cha kwao..mpk wanapiga magoti..those are strategies..ninauhakika..jpili ijayo lowasa akiingia kanisa la wakatoliki atasema naombeni kura wakristo wenzangu..ijumaa inayofuata akiingia msikitini atawaomba waislam kuwa nimekuwa nikishirikiana nanyi bega kwa bega kujenga na kutoa michango mbalimbali misikitini..hizo ni mbinu tu za kivita yupo kwenye mapambano!..watanzania tusidanyike na hilo..tujihamasishe tuwatoe wakoloni weusi madarakani!
 
✊✊✊
tahadhari kuna video inasambaa kwa kasi mitandaoni kuhusu udini wameedit lowasa akisema naomba kura za waluteri isikilizeni vizuri inasauti mbili zinatoka kwa pamoja
 
Wasubili Moro ili wajue watu wamelipokeaje hili suala la udini..
 
dhambi ya udini inakutafuna wee mzee, na mungu atakulani kwa nia mbaya uliyokua nayo katika nchi hii

Hivi ww unalaani kama nani?
Lowasa tu ndio umemuona pamoja na kutoa maelezo?

Jipime kama uko sahihi kulaani maana hujui kesho yako?
 
watanzania hatuchagui Askofu wala mchungaji/padre
 
Back
Top Bottom